Wana CCM na wananchi wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora, wakiwa wamefunga njia kuzuia msafara wa Waziri Mkuu wa zama...
Wana
CCM na wananchi wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora, wakiwa wamefunga njia
kuzuia msafara wa Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh.
Edward Lowassa, Juni 12, 2015, ili msafara huo usimame, na awasalimie.
Mh. Lowassa, alikuwa mkoani Tabora kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada
ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais wa Taznzania kupitia
CCM kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Jumla
ya wana CCM elfu 13,332, wamemdhamini Mh. Lowassa, na kuweka rekodi mpya
tangu aanza ziara za kutafuta wadhamini kanda ya Ziwa. (Picha zote na
K-VIS MEDIA)
Wana
CCM na wananchi wa wilaya Nzega, wakiwa wamefunga barabara kuu ya
Singida Shinyanga, wakitaka msafara wa Mh. Lowassa, usimame ili
awasalimie wakati msafara wake ulielekea wilayani humo kwa n ia ya
kutafuta wana CCM wa kumdhamini.
Mh. Lowassa, akiwapungia maelfu ya wana
CCM waliofurika viwanja vya ofisi za chama hicho wilayani Nzega. Jumla
ya wana CCM 3816, wilayani nhumo walimdhamini. Wana CCM 13,332
walijitokeza kumdhamini
Wana
CCM wakiwa amejawa na furaha, wakati Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa
Monduli, Mh. Edward Lowassa, alipokuwa akitoa shukrani kwa wana CCM wenzake kwenye
ofisi za chama hicho wilaya ya Tabora mjini, baada ya kupata wadhamini
Mh. Lowassa, akiwashukuru wananchi wa Tabora, waliojitokeza kumdhamini kwenye ofisi za CCM wilaya ya Tabora mjini Juni 12, 2015
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli,
Edward Lowassa, akisalimiana na mzee huyu wa mkoani Tabora ambaye alikuwa
miongoni mwa maelfu ya wana CCM na wananchi wa Tabora, waliofurika ofisi za CCM
wilaya ya Tabora mjini wakati Mh. Lowassa, alipofika kutafuta wana CCM wa
kumdhamini baada ya kuchukua fomu zan kuomba kuteuliwa kuwania urais wa
Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Jumla ya
wana CCM elfu 13,332, wamemdhamini Mh. Lowassa, na kuweka rekodi mpya tangu
aanza ziara za kutafuta wadhamini kanda ya Ziwa
Maelfu
ya wana CCM na wananchi wengine wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora, wakiwa
wamefurika kwenye viwanja vya ofisi za CCM wilayani humo Juni 12, 2015, wakati
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduki, Mh. Edward Lowassa, alipowasili
kutafuta wadhamini, baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania
urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
COMMENTS