Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonyesho ya tano ya Sekta ya Makazi kwa mwaka 201...
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonyesho ya tano ya Sekta ya Makazi kwa mwaka 2015 Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Msanifu Majengo kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba Maendeleo ya Makazi, Julius Ndege, Ofisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Iman Kajula waandaaji wa maonyesho hayo, Ofisa Masoko wa EAG Group, Helen Mangare na Richard Ryaganda, Ofisa Masoko wa EAG Group.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akisaini kitabu cha wageni kabla ya kufungua maonyesho hayo. Anayeshuhudia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Iman Kajula.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Iman Kajula (katikati), akiteta jambo na DC Makonda (kushoto) na Msanifu Majengo kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba Maendeleo ya Makazi, Julius Ndege.
Ofisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Vicent Ngaile (kulia), akimuelekeza jambo DC Makonda baada ya kutembelea banda la shirika hilo.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Dege Eco Village, Ahzari Marik akimpatia maelezo kuhusu mradi wa nyumba za kampuni hiyo, Mhe. Makonda alipotembelea banda la kampuni hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Masaimara Gardening, Murwa Kihore Simindei, akizungumza na DC Makonda alipotembelea banda lao.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ivan Amulike, akimuelekeza jambo DC Makonda katika maonyesho hayo. Wa nne kulia ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, Tumaini Iddi Setumbi na (kushoto) Ofisa Ardhi, Brenda Kuringe. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
COMMENTS