Mbuzi wakitimua mbio ili kumpata mshindi wa shindano lililopewa jina la ‘The Kilitime Stakes’ lililodhaminiwa kampuni ya Bia Tanza...
|
Mbuzi wakitimua mbio ili kumpata mshindi wa shindano lililopewa jina la ‘The Kilitime Stakes’ lililodhaminiwa kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakati wa mashindano ya mwaka huu ya mbio za mbuzi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. |
|
Washiriki wa shindano la mavazi wakijinadi ili kujaribu bahati zao. Mbio za mwaka huu zilikuwa na kauli mbiu ya ‘Bollywood’ambayo ni kiwanda cha filamu cha India, hivyo washiriki wengi walivaa mavazi yenye asili ya watu wa nchi hiyo |
|
Mbuzi wakimalizia mbio zilizoitwa ‘The CBA Sparkers’ wakati wa mashindano hayo zilizodhaminiwa na benki ya CBA. |
|
Mbuzi wakitimua mbio ili kumpata mshindi wa shindano lililopewa jina la ‘The Digital Life’ lililodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo wakati wa mashindano ya mwaka huu ya mbio za mbuzi jijini Dar es Salaam. |
|
Meneja Masoko Msaidizi wa Kampuni ya Toyota Tanzania, Eliavera Timoth akikabidhi cheti kwa Mwakilishi wa Shule ya Mt. Paulo ya Kibaigwa, Wilfred Muhogolo, ambao ni baadhi ya wanufaika wa fedha zilizopatikana katika mashindano ya mwaka huu ya mbio za mbuzi. |
|
Mbuzi wakishindana katika mbio za ‘the Toyota value+ grand national’ wakati wa mashindano ya mwaka huu ya mbio za mbuzi za hisani jijini Dar es Salaam. Mbio hizo zilikuwa na madhumuni ya kukusanya fedha ili kusaidia watu wenye mahitaji. |
|
Mwenyekiti wa kamati ya Mbio za Mbuzi, Karen Stanley akihojiwa na waandishi wa habari wakati wa mashindano hayo. |
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania, Roberto Jarrin (wa tatu kulia) akikabidhi cheti kwa mwakilishi wa asasi ya KidzCare, Diana Alex wakati wa mashindano ya mwaka huu ya mbio za mbuzi za hisani jijini Dar es Salaam. TBL ilikuwa wadhamini wa mbio hizo zenye madhumuni ya kukusanya fedha ili kusaidia watu wenye mahitaji. Wengine kutoka (kulia) ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Kushilla Thomas. |
COMMENTS