WIZARA YA KAZI NA AJIRA YAKANUSHA KUTOKUWEPO KWA UPUNGUZWAJI WA MAFAO YA PENSHENI YA PSPF NA LAPF

WIZARA YA KAZI NA AJIRA YAKANUSHA KUTOKUWEPO KWA UPUNGUZWAJI WA MAFAO YA PENSHENI YA PSPF NA LAPF   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usim...

WIZARA YA KAZI NA AJIRA YAKANUSHA KUTOKUWEPO KWA UPUNGUZWAJI WA MAFAO YA PENSHENI YA PSPF NA LAPF


 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka.
 Kamishna wa Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Saul Kinemela (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akikanusha taarifa zilizotolewa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT), zilizodai Serikali ina mpango wa kupunguza mafao ya Pensheni ya Wanachama wa Mifuko ya LAPF na PSPF. Kulia ni Kamishna wa Kazi Msaidizi, David Kanali na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Juma Muhimbi.
 Kamishna wa Kazi Msaidizi, David Kanali, Juma Muhimbi, akitoa ufafanuzi kwa wanahabari.
 Meneja Uhusiano na Uhamasishaji  wa SSRA, Sarah Kibonde Msika akimkaribisha Kamishna wa Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Saul Kinemela, kuzungumza na wanahabari.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
 Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya SSRA wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wakurugenzi wa SSRA wakiptia taarifa hiyo ya kukanusha taarifa iliyotolewa na CWT.
 Wakurugenzi wa Idara mbalimbali wa SSRA wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka (kushoto) ni Mkurugenzi wa Matekelezo na Uandikishaji, Lightness Mauki, Mkurugenzi wa Tehama, Carina Wangwe, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani, Peter Mbelwa na Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Rasilimali Watu, Mohamed Nyasama.
Mkurugenzi wa Sheria wa SSRA, Ngabo Ibrahim (katikati), akiandika taarifa hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka na Meneja Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
(Imeandaliwa na www.habari za jamii.com)

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imekanusha tamko liliotolewa na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisiza Elimu (THTU) na Chama cha Walimu  Tanzania (CWT) la kudai kwamba kuna mpango wa kupunguza Mafao ya Pensheni ya wanachama mifuko ya LAPF na PSPF.

Akizungumza  Dar es Salaam Kamishna wa Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Saul Kinemela alisema taarifa hizo sio za kweli ambazo kwa namna nyingine zinalenga kupotosha umma.

''Tunaomba wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii na umma kwa ujumla kuwa  kinachoendelea ni  majadiliano na wadau wa sekta ya hifadhi ya jamii yenye lengo la kuboresha mafao ya wastaafu'' alisema Kinemela.

Alisema kuwa Chama cha Walimu Tanzania ( CWT) na THTU wakiwa ni wadau sekta ya hifadhi ya jamii wanayo haki ya kikatiba ya kukutana na kujadiliana masuala mbalimbali yakiwamo ya sekta ya hifadhi ya jamii.

Alisema Serikali inachukua fursa hiyo kuwatoa hofu wastaafu na wanachama wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii.

''Tunaomba wadau wote wa mifuko  ya hifadhi ya jamii kuwa watulivu na kujiepusha na maneno yoyote ya upotoshwaji na mwisho kuwachanganya wanachama na hivyo kupunguza ufanisi wa kazi na utendaji,'' alisema Kinemela. 





COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WIZARA YA KAZI NA AJIRA YAKANUSHA KUTOKUWEPO KWA UPUNGUZWAJI WA MAFAO YA PENSHENI YA PSPF NA LAPF
WIZARA YA KAZI NA AJIRA YAKANUSHA KUTOKUWEPO KWA UPUNGUZWAJI WA MAFAO YA PENSHENI YA PSPF NA LAPF
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjilWicTeYImbPbnJYI2BrPk2qIoBPoViAw2SPGuZ0VQ8hkWDzi2V8TsA7kGz1HEolcy8yvnXfSKE7BYTMz9zpmj5thrIHR5HxZh_cANuuLlRhycrIGCNInsV0tl8Exsyg2XLlRWZcCoKJS/s1600/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjilWicTeYImbPbnJYI2BrPk2qIoBPoViAw2SPGuZ0VQ8hkWDzi2V8TsA7kGz1HEolcy8yvnXfSKE7BYTMz9zpmj5thrIHR5HxZh_cANuuLlRhycrIGCNInsV0tl8Exsyg2XLlRWZcCoKJS/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2014/07/wizara-ya-kazi-na-ajira-yakanusha.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2014/07/wizara-ya-kazi-na-ajira-yakanusha.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy