WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) YAFANYA ZIARA NA WAANDISHI WA VYOMBO VYA HABARI

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) YAFANYA ZIARA NA WAANDISHI WA VYOMBO VYA HABARI KUJIONEA UTUNZAJI WA MISITU YA CHOME, SHENGENA-...

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) YAFANYA ZIARA NA WAANDISHI WA VYOMBO VYA HABARI KUJIONEA UTUNZAJI WA MISITU YA CHOME, SHENGENA-KILIMANJARO.

Waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja katika hifadhi ya Msitu Asilia wa Amani, uliopo Muheza Mkoani Tanga wakati wa ziara ya waandishi hao iliyolenga kuwajengea uwezo katika uandishi wa habari za Misitu yenye Mazingira Asilia pamoja na Utalii ikolojia. Waliokaa kutoka (kushoto) ni Afisa Habari  wa Idara ya Habari (Maelezo) Frank Mvungi, Afisa Misitu Mkuu wa wakala wa huduma za Misitu Tanzania, Charles Ngatigwa (katikati) na Mwandishi wa habari wa kituo cha  televisheni Chanel ten, Kibwana Dachi (kulia).

 

Meneja wa Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS)  kanda ya Kaskazini, Cuthbert Mafupa akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) waliotembelea hifadhi ya Chome kujionea hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kutunza misitu pamoja na mafanikio yaliyofikiwa katika utunzaji wa hifadhi ya msitu wa Mazingira asilia wa chome (Shengena) ikiwemo kupanda miti katika maeneo yaliyoathika na uvunaji haramu wa rasilimali za msitu huo.




Jengo la kihistoria lililojengwa na wakoloni wa kijerumani mnamo mwaka 1902 katika hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia wa amani uliopo Muheza Mkoani Tanga, Jengo  hilo ni moja ya vivutio vikubwa katika hifadhi hiyo.

Prof. Vicky Mckinley ambaye ni Mtafiti kutoka chuo Kikuu cha Roosevelt kilichopo Chicago, Illinois nchini Marekani akipongeza juhudi za Serikali ya Tanzania katika kutunza hifadhi ya Msitu wa mazingira asilia wa Amani uliopo Wilayani Muheza Mkoani Tanga, wakati wa ziara ya waandishi hao

Sehemu ya maporomoko ya maji katika hifadhi ya Msitu wa asili ya amani iliyopo Wilayani Muheza Mkoani Tanga ambayo imekuwa kivutio kwa watalii wanaotembelea eneo hilo.

Baadhi ya aina za vipepeo wanaopatikana katika hifadhi ya Amani Mkoani Tanga ambao pia wamekuwa moja ya miradi ya kuwaongezea kipato wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo kwa kuanzisha vikundi vya kufuga vipepeo hao inayowasasaidia wananchi kujipatia mahitaji yao ya kila siku kwa kuviuza katika nchi za ulaya na Amerika.

Sehemu ya Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia wa Chome uliopo Same Mkoani Kilimanjaro.

Msaidizi wa Misitu Mkuu ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Zigi katika hifadhi ya Msitu wa asili Amani, Mlega Sossele akiwaeleza waandishi wa habari hawapo pichani jinsi wananchi wanavyonufaika na Msitu huo kwa kuwatengea asilimia 20 ya mapato yanayopatikana kwa ajili ya miradi ya maendeleo.


Moja ya Bustani za Miti zilizoanzishwa na wananchi katika kijiji cha Chome ikiwa ni hatua mojawapo ya kupambana na uharibifu wa mazingira na kujiongezea kipato kwa kuuza miti hiyo ambayo huuzwa kwa wastani wa shilingi 300 hadi 500 kwa mti mmoja kutegemea na aina ya mti. (Picha Frank Mvungi-Maelezo)




 Kibao kionesha eneo la Hifadhi ya Mazingira ya Asili ya Chome Shengena Wilaya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro.
 Meneja wa Usimamizi Endelevu wa Mazingira asilia Chome,William Nambiza akiwaonesha waandishi eneo lilillovamiwa na wachimbaji Madini na baadae walifanikiwa kuwaondoa, kwa siku walikuwa wanaingia zaidi ya 600,000 wakichanganyika na wa nchi jirani.
 Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari waliofanya ziara ya kuona mazingira ya mto Chome ambalo ni chanzo cha maji yanayokwenda mto Saseni na kutoa maji kwa wakazi wa Same na kumwaga maji Bonde la umwagiliaji Ndungu, Ruvu na Pangani.
  Meneja wa Usimamizi Endelevu wa Mazingira asilia Chome,William Nambiza akiwaonesha waandishi miti waliyopanda eneo la machimbo ya madini ya msitu wa Chome.
 Meneja wa Usimamizi Endelevu wa Mazingira asilia Chome,William Nambiza akiwaonesha waandishi eneo lilillovamiwa na wachimbaji Madini na baadae walifanikiwa kuwaondoa, kwa siku walikuwa wanaingia zaidi ya 600,000 wakichanganyika na wa nchi jirani.
 Sehemu ya msitu wa Chome ambayo ilichomwa moto na wachimbaji Madini.
 Sehemu ya Msitu wa Chome ulivyonawiri.
 Sehemu ya mpaka ya msitu wa Chome na zilizokuwa na zisizokuwa za msitu wa hifadhi upande wa kulia.
 Sehemu ya mpaka wa Msitu.
 Sehemu ya Mto Saseni.
  Sehemu ya Mto Saseni.

Sehemu ya mashamba ya wananchi wanaoishi karibu na mto Saseni.


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA

TAARIFA YA HIFADHI YA MAZINGIRA ASILI CHOME

 UTANGULIZI.

Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia wa Chome (Shengena) ni msitu wa Serikali Kuu unaosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania katika Wizara ya Maliasili na Utalii. Msitu huu ulitangazwa kwa mara ya kwanza kuwa Msitu wa Hifadhi mwaka 1951 kwa tangazo la Serikali Na. 125 la tarehe 25/05/1951. Ikafuatiwa na tamko la marekebisho kwa tangazo la Serikal Na 303 la tarehe 20/06/1958.

 Hifadhi hii ina ukubwa wa eneo la Ha 14,283 na  urefu wa mpaka wa Km 67. Hifadhi inazungukwa na vijiji 27 vilivyoko katika kata 11.

Katika kuhakikisha kuna usimamizi mzuri Msitu huu umegawanyika katika safu tano za usimamizi ambazo ni Chome, Suji, Mamba miyamba, Bombo na Mbaga.

MALENGO
Kutokana na mpago kazi wake hifadhi hii ina malengo yafuatayo:

1 Kutunza mazingira asili, mfumo wa ikologia katika uasilia wake.
2 Kuimarisha uhifadhi wa baianowai na mtawanyiko wake.
3 Kuimarisha mfumo wa ekolojia.
4 Kulinda mmomonyoko wa udongo na maporomoko ya ardhi na miamba.
5 Kuimarisha mafunzo na tafiti mbalimbali.
6 Kushirikisha jamii na wadau wote katika kulinda, kuhifadhi na kuendeleza uhifadhi.
7 Kuelimsha jamii inyozunguka hifadhi njia mbadala ya kupunguza umaskini.
HALI YA AWALI YA HIFADHI

Hali ya Msitu huu ilikuwa na chnagamoto kubwa za uhifadhi ambazo ni kama zifuatavyo;-
•       Uchimbaji wa madini ndani ya hifadhi
•       Uchomaji moto
•       Upasuaji wa mbao
•       Uchungiji wa mifugo
•       Ushiriki mdogo wa wananchi katika kulinda hifadhi hii.
•        
 KUPADISHWA HADHI KUWA  YA MAZINGIRA ASILIA
 Kuna sababu nyingi za kimsingi na za kitaalam zilizopelekea serikali kupandisha hadhi ya uhifadhi wa misitu huo kuwa hifadhi ya mazingira asilia.
SABABU HIZO NI KAMA IFUATAVYO:-
       Iligundulika kuwa eneo hili lina bio-anuwai nyingi za mimea na wanyama ambao  ni adimu, ndwele na wanaopatikana eneo hili tu.
       Eneo hili linatunza maumbile ya asili na  kuboresha hali ya hewa na kuhifadhi gesi ukaa kuvuta mawingu yanayoleta mvua za mara kwa mara.
•       Ni tanki la maji kwa wakazi wanaozunguka hifadhi hii.
•       Ni kivutio kwa watalii na hivyo utalii wa ekolojia unaendelezwa.
•       Ni sehemu maalum kwa tafiti za ekolojia ya misitu ya tropiki.

HALI YA HIFADHI BAADA KUPANDISHWA HADHI

Hatua hii ya kuupandisha Msitu na kuwa Hifadhi ya mazingira asili kwa kiasi kikubwa imepunguza kwa kiasi kikubwa changamoto zilizokuwa zinaikabili hifadhi hii ambapo shughuli za uchimbaji wa madini zimepungua,kutoka watu zaidi ya 40 kwa siku na kuwa na wastani wa mtu mmoja hadi 4 kwa siku.matukio ya moto yamepungua pamoja na mifugo. Wananchi wameelewa umuhimu wa utunzaji wa hifadhi.
Ili kuhakikisha kuwa uhifadhi unaendelea na hatimaye kufikia malengo tajwa hapo juu hifadhi hii inafanya shuguli zifuatazo;

•       Kufanya Doria shirikishi ndani na nje ya Hifadhi kwa kushirikiana na kamati za maliasili za vijiji
•       Kuimarisha mpaka wa hifadhi kwa kusafisha na kupanda miti.
•       Kurejesha maeneo yaliyoharibiwakwa kufukia mashimo yaliyoachwa wazi na wachimbaji madini haramu, kurudisha mikondo ya maji kwenye njia za asili na kupanda miti
•       Kuandaa na kusafisha njia za kitalii
•       Kuwasaidia wanavijiji kuanzisha bustani za miti ya asili kwaajili ya kupanda mashambani
•       Kuwawezesha wanavijiji wanazunguka hifadhi kuanzisha miradi midogomidogo ya kujiongezea kipato mfano ufugaji nyuki,
•       Kuanzisha Kamati za Maliasili za vijiji ili kuongeza ushiriki wa jamii zinazozunguka hifadhi hii.

USHIRIKI WA TAASISI NA MASHIRIKA MENGINE KATIKA UHIFADHI
Katika kuhakikisha kuwa hifadhi hii inatekeleza majukumu yake kikamilifu hifadhi inashirikiana na taasisi na mashirika mbali mbali kama;-

•       Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
•       Ofisi ya mkuu wa wilaya Same
•       Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Same.
•       Ofisi ya mkuu wa kituo cha polisi Same
•       Mfuko wa hifadhi ya milima ya Tao la mashariki (EAMCEF)
•       Shirika la Kuhifadhi Misitu Tanzania (TFCG)
•       Serikali na halmashauri za vijiji
•       Wananchi wanaozunguka hifadhi


MAFANIKIO

Kwa kushrikiana na wadau wengine pamoja na serikali za vijiji mafanikio yafuatayo yamepatikana  kipindi cha mwaka 2012 – 2014)

•       Kwa kufanya doria shirikishi tumefanikiwa kuwaondoa wachimbaji wa madini ndani ya hifadhi ambao walikuwa takribani 2000 na kufanikiwa kukamata zana mbalimbali wanazotumia katika uchimbaji kama mashine za kusukumia maji (water pump) 20 Beleshi 30 Surulu10 n.k
•       Upasuaji mbao umepungua ambapo kutokana na doria hizo misumeno 10  pamoja na wahalifu walikamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria pia mazao mbalimbali ya misitu yalikamatwa ikiwemo milango 160 pamja na mbao vpande 100
•       Jumla ya wahalifu 54 walikamatwa 16 kati yao wamehukumiwa vifungo vya kati ya mwaka mmoja hadi miwili. 29 wamelipa faini 9 kesi zao bado zipo mahakamani.
•       Kuuongeza ushiriki wa wananchi kwa kuanzisha Kamati za Maliasili za vijiji kwa kila kijiji.ambazo jumla yao ni kamati 27.
•       Kuwaondoa wavamizi wa hifadhi ambao walivamia kwa lengo la kulima au kuweka makazi ndani ya hifadhi.
•       Kuimarisha mpaka wa hifadhi kwa kupanda miti na kuweka mabango ili kuzuia uvamizi wa hifadhi.
•       Kuwawezesha wananchi kuanzisha bustani zao za miti ili kupanda katika mashamba yao.
•       Matukio ya moto yaliyowahi kutokea yamepungua kutoka matukio 5 kwa mwaka hadi tukio moja kwa siku.
•       Idadi ya mifugo imezidi kupungua kutoka wastani wa ngombe 50 hadi wastani wa ngombe watano wanaoingia ndani ya hifadhi.                                                         

CHANGAMOTO

•       Upungufu wa rutuba katika mashamba ambao unasababisha jamii kutovuna mazao ya kutosha kukidhi mahitaji yao.
•       Mtandao wa wafanyabiashara wa mazao ya  misitu hasa mbao zinazokamatwa na miti comphour(mkulo) kwa kutengenezea milango , vitanda n.k.
•       Kwa ujumla wake ni matumizi dhidi ya uhifadhi. (Kwa hisani ya Muhidini Michuzi)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) YAFANYA ZIARA NA WAANDISHI WA VYOMBO VYA HABARI
WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) YAFANYA ZIARA NA WAANDISHI WA VYOMBO VYA HABARI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhCI6O28a7ZF2YEZDrCGF4AdT5T3i7yDu-JpPmk7QHwXB4G-QawuJEpqti_5VSBiR_qYGfmUVp5RzfpPmzGiNCfDpApl6jjmsuLIIDF3tjEz8IjO5L2zD-F_20erPBwJ0l_3HZ0sXANbmw/s1600/2.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhCI6O28a7ZF2YEZDrCGF4AdT5T3i7yDu-JpPmk7QHwXB4G-QawuJEpqti_5VSBiR_qYGfmUVp5RzfpPmzGiNCfDpApl6jjmsuLIIDF3tjEz8IjO5L2zD-F_20erPBwJ0l_3HZ0sXANbmw/s72-c/2.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2014/05/wakala-wa-huduma-za-misitu-tanzania-tfs.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2014/05/wakala-wa-huduma-za-misitu-tanzania-tfs.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy