KINANA AFANYA MAKUBWA MANYONI, AZINDUA NYUMBA YA KISASA YA MFUGAJI ALIYEZINDUKA KWA SERA ZA CCM Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman ...
KINANA AFANYA MAKUBWA MANYONI, AZINDUA NYUMBA YA KISASA YA MFUGAJI ALIYEZINDUKA KWA SERA ZA CCM
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa
hadhara uliofanyika leo, Mei 20, 2014, kwenye Viwanja vya Stendi mjini
Manyoni, akiwa katika siku yake ya pili ya ziara ya siku nane mkoani
Singida, kwa lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza
kero za wananchi huku akijadiliana nao njia ya kuzitatua mkoani humo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano huo leo
Wananchi wakishangilia kwenye mkutano huo
Katibu
Mkuu wa CCM, Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Kijiji cha Heka Azimio, zaidi ya kilometa 20 kutoka mjini
Manyoni leo Mei 20, 2014.
Katibu
Mkuu wa CCM, Kinana akimkaribisha jukwaani Mbunge wa Manyoni Mashariki
kapten Mstaafu John Chiligati kuwaeleza ananchi alivyosimamia
utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo lake hususan kijiji hicho cha
Heka katika kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo ya umeme na maji
Wanachama 28 waliopewa kadi zao za CCM na Kinana kwenye mkutano huo wa Kijiji cha Heka Azimio, wakila kiapo
Kinana akipewa zawadi ya zana za asili na mzee mmoja wa Kijiji cha Heka, wilayani Manyoni.
Katibu
Mkuu wa CCM, Kinana akimpa tofali fundi aliposhiriki ujenzi wa maabara
ya shule ya sekondari Heka, Manyoni, Mei 20, 2014 wakati wa ziara hiyo
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Msindai (kushoto) akimpatia tofali Nape
ili kumpatia fundi wakati wa kushiriki kwenye ujenzi wa chumba cha
maabara ya shule hiyo ya Heka
Nape akimpatia fundi tofali kwenye kushiriki ujenzi wa chumba hicho cha maabara katika shule hiyo ya Heka, Mei 20, 2014
Kinana akizindua nyumba ya mpya ya kisasa ya mfugaji Jonase Mihangwa wa Kijiji cha Heka,
wilayani Manyoni ambaye amekuwa miongoni mwa wafugaji wa kuigwa kwa kuamua kuuza
sehemu ya mifugo yake kubadilisha maisha yake ikiwemo kujenga nyumba hiyo ya kisasa yenye umeme wa mionzi ya
jua.
Mihangwa (kulia) akienda kumuonyesha Kinana nyumba yake duni ya zamani
alimokuwa akiishi kabla ya uamuzi wake wa kuuza sehemu ya mifugo yake na
kujenga nyumba ya kissa
Kinana akiangalia mifungo ya Mfugaji Mihangwa iliyobakia baada ya kuuza
mingine kwa ajili ya kujenga nyumba ya kisasa. Mihangwa anasema aliamua
kuuza ng'ombe 200 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ya kisasa.
Kinana akishiriki ujenzi wa Uwanja wa Jumbe ambao umefanyiwa ukarabati na Mbunge wa Manyoni, Kapteni (mstaafu) John Chiligati
Kinana
(wa pili kushoto) akishiriki mazoezi na vijana wanaoshiriki michuano ya
UMISETA kwenye Uwanja huo wa Jumbe, alipowatembelea kuwaona na kushiriki
ujenzi wa Uwanja huo, Mei 20, 2014
Kinana (wa pili kushoto) akishiriki mazoezi na vijana wanaoshiriki
michuano ya UMISETA kwenye Uwanja huo wa Jumbe, alipowatembelea kuwaona
na kushoriki ujenzi wa Uwanja huo, Mei 20, 2014
Kinana (wa pili kushoto) akishiriki mazoezi na vijana wanaoshiriki
michuano ya UMISETA kwenye Uwanja huo wa Jumbe, alipowatembelea kuwaona
na kushoriki ujenzi wa Uwanja huo, Mei 20, 2014
Mwanachama
wa CCM ktk Shina mamba tisa tawi la CCM Mwembeni Manyoni, Mchungaji
Daniel Makavu akisoma risala kwa Kinana (wa tatu kushoto), aliyefika kwa
balozi wa shina namba tisa akiwa katika ziara hiyo mjini Manyoni
Kinana akimpongeza Balozi wa Shina la CCM la Mwembeni, Manyoni Mjini,
Daud Mwimbwa alipokwenda kumtembelea na kuambiwa wanachama wote wa shina
hilo wamelipia ada zote hivyo kuwa wanachama hai. Kinana alimpongeza na
kumwalika kwenye kikao cha juu cha chama hicho kitakachofanyika Mbeya hivi karibuni, kwenda kueleza mbinu
alizozitumia kuwashawishi wanachama wake kulipia ada kitendo ambacho
katika ziara zake zote alizozifanya nchini hakijawahi kutokea kwa balozi
zingine. (Picha zote na Bashir Nkoromo)
COMMENTS