KAMANDA KOVA AMUANIKA KINARA WA WIZI WA MABENKI, SILAHA, MEN O YA TEMBO NA WIZI BENKI YA BARCLAYS TAWI LA KINONDONI DSM. Kamanda wa ...
KAMANDA KOVA AMUANIKA KINARA WA WIZI WA MABENKI, SILAHA, MEN O YA TEMBO NA WIZI BENKI YA BARCLAYS TAWI LA KINONDONI DSM.
Baadhi ya mali za wizi zaanikwa. |
Baadhi ya mali za wizi zaanikwa. |
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akiongea na waandishi wa habari. |
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akionesha meno ya tembo yaliyokamatwa. |
Kamanda Suleiman Kova akionesha moja ya magari yalikamtwa kwa makosa ya uhalifu. |
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS
RELEASE
14/05/2014
POLISI
WAMGUNDUA KINARA WA MTANDAO WA WIZI
KATIKA MABENKI JIJINI D’SALAAM (PICHA YAKE YATOLEWA HADHARANI)
ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum
D’Salaam limefanikiwa kumbaini mtuhumiwa mhimu ambaye ni kinara wa mtandao wa
wizi katika mabenki ambaye anajulikana kwa jina la RONALD S/O MOLLEL umri miaka
37, mfanyabishara na mkazi wa Kimara Bonyokwa Jijini D’salaam.
Mtuhumiwa huyu amekimbilia
mafichoni mara baada ya tukio la ujambazi katika Tawi la Benki ya Barclays Kinondoni lililotokea tarehe 15/4/2014 ambapo
majambazi walifanikiwa kupora kiasi kikubwa cha fedha T.Shs.390,220,000/= , USD 55,000/= na EURO 2150/=. Aidha sasa imefahamika kwamba mtuhumiwa huyu
ni mume wa mtuhumiwa wa kwanza katika tukio la Barclays Benki aitwaye ALUNE D/O
KASILILIKA @ ALUNE D/O MOLLEL , miaka 28,
Mkazi wa Kimara Bonyokwa ambaye ni Meneja wa Benki Tawi la Barclays
Kinondoni. Mtuhumiwa Mollel anatafutwa
kwa kila hali kwa vile yeye ndiye alikuwa kinara wa kupanga tukio hilo la Barclays
na mara baada ya tukio ametoroka na kiasi kikubwa cha fedha hizo zilizoibiwa.
Zipo taarifa za kuaminika
kuwa mtuhumiwa huyu amekuwa akipanga na kushiriki kikamilifu katika matukio
mbali mbali ya uhalifu mkubwa ikiwa ni pamoja na kuongoza vikundi vya majambazi
vilivyowahi kupora katika mabenki mbali mbali katika kipindi cha mwaka mmoja
uliopita. Mtuhumiwa huyo ni hatari kwani
ana mtandao na watumishi muhimu katika matawi mbali mbali ya mabenki kwa lengo
la kufanikisha uhalifu katika mabenki hayo.
Jeshi la Polisi limelazimika
kutoa picha yake hadharani kwa kutumia dhana ya ulinzi shirikishi ili mtuhumiwa
huyu akionekana akamatwe na taarifa zitolewe katika kituo chochote cha Polisi
ikiwa ni lengo la polisi kupambana na uhalifu katika dhamira ya kuzuia uhalifu,
kulinda maisha na mali za wananchi.
Zawadi nono ya fedha taslim itatolewa kwa siri kwa mtu yeyote atakayetoa
taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu. Pamoja na maelezo hayo mtuhumiwa mwenyewe
sasa anapewa fulsa ya kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kabla ya
kukamatwa kwa njia nyingine.
Kinara anayetuhumiwa kufanya wizi katika mabenki anajulikana kwa jina la RONALD S/O MOLLEL umri miaka 37, mfanyabishara na mkazi wa Kimara Bonyokwa. |
MAJAMBAZI WATATU WAKAMATWA NA SILAHA 2 NA SARE
ZA JESHI.
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum D’Salaam mnamo tarehe 13/05/2014 limefanikiwa kuwakamata
majambazi watatu wakiwa na silaha mbili aina ya Shot gun na risasi 12, Redio
Call 1 na sare za Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ). Mafanikio haya
yametokana na msako mkali unaoendelea jijini D’Salaam. Majina ya majambazi hayo ni kama ifuatavyo:-
1.
Isi-Hakka s/o
Salehe
2.
Alex s/o
Andrew
3.
Odinga s/o
Swalehe
Majambazi
hao walikamatwa maeneo ya Chamazi katika Mkoa wa Kipolisi Temeke baada ya
kupata taarifa kutoka kwa wananchi.
Jambazi mmoja alikamatwa ndani ya gari aina ya Hiace (daladala) na
wengine wawili ndani ya nyumba baada ya jambazi wa kwanza kuelekeza wenzake
walipo. Polisi walifanya upekuzi katika
nyumba hiyo na kufanikiwa kupata vitu hivyo.
Uchunguzi bado unaendelea na watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani
baada ya upelelezi kukamilika.
POLISI
JIJINI DAR ES SALAAM WAFUMUA MTANDAO WA MAKOSA YA UVUNJAJI KWA KUKAMATA MAJAMBAZI
SUGU 15 NA VITU MBALIMBALI.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum
kwa kutumia kikosi maalum cha Kiintelijensia (special intelligence task force)
limefanikiwa kuufumua mtandao unaojihusisha na ujambazi jijini Dar es Salaam
ikiwemo kuhusika na uvunjaji na kisha kupora mali mbalimbali zikiwemo nyumba za
ibada.
Katika oparesheni hiyo
iliyoanza tarehe 29/04/2014, wamekamatwa majambazi sugu wawili ambao baada ya
kuhojiwa waliwataja wenzao wengine kumi
na tatu (13) wanaoshirikiana nao katika matukio ya ujambazi na kufanya
idadi yao kufikia kumi na tano.
Watuhumiwa waliokamatwa na
kutaja mtandao mzima ni SHABAN S/O
MAFURU, Miaka 36, Mkazi wa Magomeni na ABDALLAH
S/O HUSSEIN, Miaka 52, Mkazi wa Tabata Mawenzi, ambao wote walikutwa kwenye
gari namba T259 ADB, T/RAV rangi ya Silver wakiwa wamepakia vitu mbalimbali vya
wizi kama ifuatavyo:
·
Moving Camera - 4.
·
Stand mbili za Moving Camera.
·
Desk-top computer – 2
·
Deki mbili za DVD.
Inasemekana mali hizi
walizokutwa nazo watuhumiwa hawa ziliibwa katika ofisi za ISLAM INTERNATIONA LTD zilizopo maeneo ya mabibo jijini Dar es
Salaam.
Baada ya kukamatwa kwa
watuhumiwa hao kumi na tano walihojiwa na kukiri kuhusika katika matukio kadhaa
ya uvunjaji na uporaji kama ifuatavyo:
·
Tukio la tarehe 01/05/2014 maeneo ya REGENT
ESTATE katika ofisi za NAIRO ambapo walivunja na kuiba viyoyozi (Air Condition)
120 na vitu vingine.
·
Tarehe 22/04/2014 huko maeneo ya Mwenge
katika duka SAMSUNG, walivunja na kuiba TV Set zipatazo nane (8) na simu za
mkononi mbalimbali.
·
Tarehe 17/04/2014 maeneo ya MASAKI walivunja
Supermarket iitwayo SHIREJEES na kupora fedha TSh. 19,000,000/= (Millioni kumi
na tisa), Monitor mbili za Computer, LCD TV Set mbili, na pombe kali za aina
mbalimbali.
·
Pia wamekiri kuvunja Makanisa mawili moja ni
lile la K.K.K.T Usharika wa Magomeni
na kupora pesa taslim Tsh. 8,000,000/=. Kanisa lingine walilokiri kuvunja ni
lile la AICT ambapo walipora Tsh 500,000/=, Desk-top Computer mbili aina ya DELL, Laptop mbili aina ya DELL, na Projctor
moja aina ya Sony.
·
Wamekiri kuhusika katika uvunjaji kwenye
ofisi za Shule ya Sekondari ya LOYOLA iliyoko Mabibo na kuiba DOLLA ZA
KIMAREKANI zipatazo 8000 na Shillingi za Kitanzania 9,000,000/=
Watuhumiwa wengine
waliokamatwa wanaounda mtandao huu ni kama ifuatavyo:
·
FLORIAN S/O PHILOMON @ K.K, Miaka 35, Mkazi
wa Manzese.
·
MATOKE S/O MAGERE, Miaka 30, Mkazi wa Kigogo
Kintinku.
·
RASHID S/O MUSSA @ GAIDI, Miaka 42, Mkazi wa
Kariakoo Mchikichini.
·
ATHUMAN S/O SALEHE @ KIDINYU, Miaka 30, Mkazi
wa Magomeni Makuti.
·
AZIZI
S/O SAID FADARI, Miaka 38, Mkazi wa Kiwalani Minazi Mirefu
·
IBRAHIMU S/O KINGU, Miaka 50, Mkazi wa Temeke
Mikoroshini.
·
THOMAS S/O KIMAMBI, Miaka 33, Mkazi wa Ubungo
External.
·
JOSEPH S/O JOSEPH THOMAS, Miaka 32, Mkazi wa
Kimara Stop Over.
·
STEPHANO S/O SAMWEL @ LIKONGO, Miaka 37,
Mkazi wa Mburahati Mianzini.
·
NICKO S/O NUSULUPIA HAULE @ NICK BUTY, Miaka
31, Mkazi wa Mburahati Mianzini.
·
KUDRA S/O MOHAMED, Miaka 30, Mkazi wa Ubungo.
·
HAMISI S/O SALUM SALEHE, Miaka 31, Mkazi wa
Kimara Rombo.
·
MOHAMED S/O RASHID, Miaka 30, Mkazi wa Kimara
Rombo.
WATUHUMIWA
2 WAKAMATWA NA MENO 25 YA KIBOKO NA 1
AKAMATWWA NA VIPANDE 8 VYA MENO YA TEMBO AMBAVYO NI NYARA ZA SERIKALI
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum limefanikiwa kukamata vipande zaidi ya ishirini (20)
vinavyodhaniwa kuwa ni meno ya Tembo vilivyokuwa vimehifadhiwa nadni ya mfuko
maarufu kwa jina la kiroba. Tukio hili lilitokea tarehe 30/04/2014 katika
kiwanda cha Nondo Steel Master kilichopo eneo la Mbozi Road (W) kipolisi
Chang’ombe (M) kipolisi Temeke baada ya Polisi kupokea taarifa kuwa katika
kiwanda hicho kuna mfuko wa kiroba wenye bidhaa hiyo umefichwa.
Baada ya taarifa hizo askari
kikosi cha Upelelezi walifika kiwandani hapo na kwa kushirikiana na Mkurugenzi
wa Kiwanda hicho aitwaye HITESH S/O PATEL walifanya upekuzi. Katika upekuzi huo
polisi walifanikiwa kukamata vipande 25 vya meno yadhaniwayo kuwa ni ya KIBOKO
vikiwa vimehifadhiwa ndani ya mfuko wa kiroba ukiwa umefichwa kwenye Roll
ambayo ni Malighafi maalum ya kutengenezea nondo. Kwa mujibu wa taarifa ya
maafisa wa wanyamapori ni kwamba kwa idadi ya vipande hivyo 25 ni sawa na
VIBOKO 6 waliouawa ambapo meno ya Kiboko mmoja yana thamani ya Dolla za Kimarekani 1500 sawa na
Shilingi za Kitanzania zaidi ya (Millioni
Mbili Laki Nne na Sabini na Tano) Tshs.2,475,000. Hivyo kwa idadi ya VOBOKO
sita thamani yake ni sawa na shilingi za kitanzania THS; 14,850,000/= (million kumi na nne, mia nane na hamsini elfu tu).
Katika tukio hilo, polisi
inawashikilia watu wawili ambao ni RASHID S/O ABDALLAH, Miaka 19, mwingine ni
HEMED S/O JUMA @ KASIMU, Miaka 25. Washitakiwa hao watafikishwa mahakamani
kujibu shitaka linalowakabili pindi upelelezi utakapokamilika.
Aidha katika tukio lingine mnamo
tarehe 5/5/2014 huko maeneo ya Tabata Kisiwani karibu na uwanja wa Twiga Mkoa
wa Kipolisi Ilala, Polisi wamefanikiwa kumkamata MUSA S/O LUCAS KIFARU akiwa
naa vipande 8 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogram 13.5 ambavyo thamani
yake T.Shs.49,500,000/= vikiwa vimehifadhiwa kwenye begi lenye rangi ya blue na
nyeusi. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa .
TAARIFA
ZA UKAMATAJI WA MAKOSA KITENGO CHA USALAMA BARABARANI KANDA MAALUM KUANZIA
01/05/2014 HADI SASA.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum
kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani liliendesha oparesheni kamambe kukamata
makosa yanayohusisha uvunjaji wa sheria mbalimbali za usalama barabarani ili
kuhakikisha watumiaji wote wa barabara wanazingatia sheria hizo. Makosa hayo ni
pamoja na haya yafuatayo:
·
Ubovu wa Magari,
·
Obstraction,
·
Kuzidisha Abiria,
·
T.L.A,
·
Kukatisha Route,
·
Uendeshaji wa hatari,
·
Kutotii Amri,
·
Matumizi mabaya ya barabara,
·
Kutokuwa na Leseni, nk.
Aidha katika oparesheni hiyo
vyombo mbalimbali vya usafiri yakiwemo Magari, Pikipiki, Bajaji na vingine
vilikamatwa na kutozwa tozo kulingana na makosa kwa kila chombo kama ifuatavyo:
MGAWANYO
WA MAKOSA NGAZI YA KI-MIKOA
JUMLA YA MAKOSA - ILALA
|
JUMLA YA MAKOSA TEMEKE
|
JUMLA YA MAKOSA KINONDONI
|
JUMLA KUU
|
3066
|
2399
|
4630
|
10095
|
MGAWANYO
WA TOZO NGAZI YA KI-MIKOA
JUMLA YA TOZO
ILALA
|
JUMLA YA TOZO TEMEKE
|
JUMLA YA TOZO KINONDONI
|
JUMLA KUU
|
Tshs 82,200,000/=
|
65,850,000/=
|
125,580,000/=
|
273,630,000/=
|
Aidha, taarifa ya Kikosi cha
Usalama barabarani Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam ya ukamataji wa makosa
ya Usalama Barabarani kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Januari 2014 ni kama
ifuatavyo:
1.
Idadi
ya magari yaliyokamatwa - 64,785
2.
Idadi
ya pikipiki zilizokamatwa - 17,082
3.
Jumla
ya Makosa yaliyokamatwa - 84,474
4. Fedha za TOZO zilizopatikana Tsh: 2,534,220,000/=
S.H.
KOVA
KAMISHNA
WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
COMMENTS