SAID BAHANUZI AWAPA ULAJI AL-AHLY AIONDOSHA YANGA MASHINDANONI KWA KUKOSA PENATI AL-AHLY WALIVYOPONEA KWENYE TUNDU LA SINDANO KUI...
SAID BAHANUZI AWAPA ULAJI AL-AHLY AIONDOSHA YANGA MASHINDANONI KWA KUKOSA PENATI
AL-AHLY WALIVYOPONEA KWENYE TUNDU LA SINDANO KUITOA YANGA KWA PENATI 4-3
Mchezo wa raundi ya pili wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya wenyeji Al Ahly imemalizika usiku huu, huku
Mabingwa hao wa Afrika wakitokea kwenye tundu la sindano baada ya kupata ushindi wa penati 4-3.
Katika dakika 90, Ahly walishinda kwa bao 1-0 lililofungwa katika dakika ya 70.
Katika mikwaju ya penati, Mabeki Mbuyu Twite na Oscar Joshua walikosa baada ya penalti zao kupanguliwa.
Kipa
Deo Munishi aliswazisha makosa yao baada ya kupangua penalti 2.
Ilikuwa ni zamu ya Said Bahanuzi ambaye kama angefunga, basi Yanga
ingefuzu.
Lakini
mkwaju aliopiga ulitoka nje na baada ya hapo, Ahly wakamalizia penati
moja na kufuzu kwenye hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika. (Kwa
hisani ya Salehjembe)
SAID BAHANUZI AWAPA ULAJI AL-AHLY AIONDOSHA YANGA MASHINDANONI KWA KUKOSA PENATI
Penati
pekee iliyotoka nje ya milingoti mitatu iliyopigwa na Said Bahanuzi,
iliwawezesha Al-Ahly kuendelea na mtindo wa penati moja moja baada ya
wao kukosa penati mbili zilizochezwa na kipa wa yanga, Deogratius
Munishi, huku Yanga wakitegemea matokeo ya wapigaji wao waliokuwa
wamesalia, Oscar Joshua, aliyepiga na kupanguliwa na kipa na Said
Bahanuzi aliyekuwa ndiye tegemeo la kuwanyanyua mashabiki wa Soka
waliokuwa wamekti pembezoni mwa Tv zao na wengine wakisikiliza kupitia
redioni.
Wapigaji
wa Yanga walikuwa ni Nadir Haroub, Didier Kavumbagu, Emmanuel Okwi,
ambao wote walipata. Wengine ni Oscar Joshua, aliyekosa baada ya kipa
kuucheza na Said Bahanuzi, aliyetoa nje kabisa mpira huo.
Al-
Ahly wao walikosa penati ya 4 na ya 5, na baada ya mtindo wa kupigiana
penati moja moja, wao walipata, Yanga wakakosa baada ya mpigaji wake
Mbuyu Twite, kukosa penati ya kwanza katika mtindo ya penati moja moja.
Bao
la Al-Ahly lilifungwa katika dakika ya 70, na kufanya mchezo huo kuwa
sare ya bao 1-1, na hadi dakika 90 zinamalizika Al-Ahly 1 Yanga 0,
lakini wakijivunia bao la nyumbani jambo ambalo liliamua mikwaju ya
penati.
Shukrani za pekee na hongera zimfikie Kipa wa Yanga, Deo Munishi, aliyeweza kuokoa michomo miwili ya penati.
COMMENTS