MHE. JANUARY MAKAMBA ATEMBELEA DARASA LA KISWAHILI DMV Naibu Waziri wa mawasiliano, sayansi na teknologia, Mhe. Janu...
MHE. JANUARY MAKAMBA ATEMBELEA DARASA LA KISWAHILI DMV
Naibu
Waziri wa mawasiliano, sayansi na teknologia, Mhe. January Makamba
akiongozana na Afisa Ubalozi Mindi Kasiga siku ya Jumamosi Dec 7, 2013
College Park Maryland, siku alipotembelea darasa la Kiswahili DMV.
Mhe.
January Makamba akisalimiana na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania mara
tu alipoingia kwenye darasa hilo Jumamosi Dec 7, 2013 College Park,
Maryalnd.
Mhe.
January Makamba akipata historia fupi ya darasa hilo kutoka kwa rais wa
Jumuiya Iddi Sandaly (wapili toka kushoto) siku ya Jumamosi Dec 7, 2013
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia alipotembelea darasa
hilo College Park Maryland.
Mhe. January Makamba akisalimiana na wazazi wa watoto wa darasa la kiswahili DMV.
Mhe.
January Makamba akipata maelezo kuhusiana na watoto wa darasa la
kiswahili DMV kutoka kwa katibu wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Amos
Cherehani (kulia koti jeusi).
Watoto wa darasa la kiswahili DMV wakitoa salamu kwa mhe. January Makamba (hayupo pichani)
Mhe.
January Makamba pamoja na Afisa Ubalozi Mindi Kasiga, Rais wa Jumuiya
Iddi Sandaly na mwalimu mkuu wa darasa la kiswahili wakiwa wamesimama
wakati watoto wa darasa la kiswahili waliopkuwa wakiimba wimbo wa taifa.
Watoto
wa darasa la kiswahili wakimwimbia mgeni wao Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba wimbo wa Taifa.
Juu
na chini baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV, watoto wa
darasa la kiswahili na wazazi wakimsikizliza Mhe. January Makamba
(hayupo picha) alipokua akiwathimilia hadithi watoto wa darasa la
kiswahili DMV.
Darasa...
MVUA YA SAA CHACHE JIJINI DAR HATARI TUPU MAENEO YA TABATA
Kutokana
na mvua iliyonyesha jijini Dar es Salaam, mida ya mchana wa jana baadhi ya
maeneo yameathirika na mvua hiyo hususan eneo la Tabata, ambako baadhi
ya nyumba zimezungukwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa iliyonyesha
muda mchache uliopita jijini hapa.
RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI KUTOKA UFARANSA
Rais
Dk Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni wakati aliposimama
kwa muda katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini
Nairobi akiwa njiani kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano
unaohusu Amani na usalama na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Bara la
Africa na Ufaransa. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya,
Balozi Amina Mohamed na Afisa itifaki.
Rais
Dk Jakaya Kikwete akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Kenya, Balozi Amina Mohamed katika uwanja wa
ndege wa Kimataifa Jomo Kenyata Nairobi, Kenya alipokuwa akirejea nyumbani akitokea Paris
Ufaransa ambapo alihudhuria mkutano uliohusu Amani, Usalama na
Ushirikiano wa kiuchumi kati ya Ufaransa na bara la Afrika.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Mec Sadik akimkaribisha Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere muda mfupi baada y kuwasili akitokea Paris Ufaransa
ambapo alihudhuria Mkutano wa Amani,Usalama na Ushirikianokati ya Afrika
na Ufaransa uliomalizika jana. (Picha na Freddy Maro)
MECHI YA KILIMANJARO STARS NA HARAMBEE STARS KUPIGWA MACHAKOS
Mechi
ya kwanza ya nusu fainali ya michuano ya mwaka huu ya Kombe la Chalenji
kati ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) na wenyeji Kenya (Harambee
Stars) itapigwa Uwanja wa Machakos.
Kwa
mujibu wa ofisa wa CECAFA, Amir Hassan mechi hiyo itachezwa Uwanja wa
Machakos ulioko takribani kilometa 64 kutoka jijini Nairobi. Mechi hiyo
itachezwa Jumanne (Desemba 10 mwaka huu) kuanzia saa 10 kamili jioni na
itaoneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha SuperSport
kupitia chaneli ya SS9.
Kilimanjaro
Stars imetinga hatua hiyo baada ya kuivua ubingwa Uganda (The Cranes)
kwa mikwaju 3-2 ya penalti katika mechi ya robo fainali ya michuano hiyo
iliyochezwa jana Uwanja wa Aga Khan katika Jiji la Mombasa.
Hadi
dakika 90 za kawaida zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana mabao
2-2. Mabao ya Kilimanjaro Stars yalifungwa na Mrisho Ngasa wakati katika
mikwaju ya penalti walofumania nyavu ni Amri Kiemba, Athuman Idd na
nahodha Kelvin Yondani.
COMMENTS