Huyu ndio mrembo wa Kitanzania alietangazwa mshindi wa taji la “Miss Commonwealth Africa” huko London Uingereza. Mtanzania, Malkia Kas...
Huyu
ndio mrembo wa Kitanzania alietangazwa mshindi wa taji la “Miss
Commonwealth Africa” huko London Uingereza.
Mtanzania, Malkia Kassu ( wa tatu kulia) akiwa na washindi wenzake – wote wamevalia taji na kubeba vikombe vya ushindi.
Mashindano ya 2013 yalifanyika London Jumamosi Novemba 26 na kwa mara ya kwanza yalikuwa na mshiriki toka Tanzania.
Malkia Kassu (jina la kuzaliwa Mulki Kassu Miraj) alichaguliwa malkia wa Tanzania na bara zima la Afrika.
Wateuzi wa ushindi huo hawakuangalia tu sura, bali tabia, fikra,
hamasa na msimamo wa kimaendeleo wa mhusika ambapo washindani walitoka
mataifa mbalimbali duniani.
“Ninataka kuiwakilisha nchi yangu na kuwasaidia wenye maisha magumu,
niifanye dunia iwe mahali pazuri zaidi. Nafahamu si kazi rahisi ila nina
hakika kila mmoja wetu akijumuika na mwenzake mabadiliko mema zaidi
yatafanyika. Tanzania ni nchi ya amani na ninaamini amani na mapenzi
vyaweza kuongezeka katika jumuiya zetu.” – Kassu
Kutoka
kushoto ni mdhamini, Ali Sungura, Balozi wa Tanzania Uingereza , Mhe. Peter Kallaghe, Aisha Mohammed na Afisa Ubalozi Allen
Kuzilwa
Malkia Kassu
Malkia Kassu akipongezwa na marafiki, Andrew Matt na Aisha Mohammed.
Malkia Kassu akiwa na mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul a.ka 'Diamond Platnumuz'karibuni.

Stori imeandaliwa na Frank Eyembe.
 |
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Maaskofu wa Kanisa la Anglican nchini wakati alipowasili
kwenye Kanisa Kuu la Anglican la Njombe kuhudhuria mazishi ya Askofu wa
Dayosisi ya South West Tanganyika, John Andrew Simalenga. |
 |
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa
heshima za mwisho kwa Askofu John Andrew Simalenga katika mazishi ya Askofu
huyo wa Dayosisi ya South West Tanganyika ya Kanisa la Anglican yaliyofanyika Njombe. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglican nchini,
Dk Jacob Chimeledya. |
 |
Mwili wa Askofu wa John Andrew Simalenga
ukiteremshwa kaburini na wachungaji. |
 |
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
na Spika wa Bunge Anne Makinda wakishiki katika Ibada ya mazishi. |
 |
Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda akiweka udongo katika kaburi la Askofu huyo. |
 |
Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu. | |
|
|
|
|
|
|
 |
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akizungumza katika ibada ya mazishi ya Askofu wa Kanisa la Anglican
Dayosisi ya South West Tanganyika, John Andrew Simalenga yaliyofanyika Njombe
Novemba 28, 2013. (Picha na PMO)
 |
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, akisoma hituba yake ya
uzinduzi rasmi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA), miaka 10 ya mapinduzi katika Sekta ya Mawasiliano Tanzania,
yaliyozinduliwa rasmi leo katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. |
 |
Baadhi ya viongozi na wadau wakifuatilia matuki katika sherehe za maadhimisho hayo. |
 |
Makamu wa Rais wa
Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Prof John Nkoma, wakati alipotembelea katika
chumba cha Mtambo wa Kufuatilia Mawasiliano ya Simu (Telecommunicatins Traffic
Monitoring System) baada ya kufungua rasmi Sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho hayo. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, Prof Makame Mbarawa. |
 |
Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka
kwa Mkurugenzi msaidizi chumba cha mtambo wa kufuatilia mawasiliano ya Simu
(Telecommunicatins Traffic Monitoring System) Sunday Richard, wakati
alipotembelea chumba hicho. |
 |
Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal (katikati) akizungumza na Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Prof John Nkoma (kulia) na Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa, nje ya Jengo la
Mawasiliano baada ya kutembelea Chumba cha Mtambo wa Kufuatilia Mawasiliano ya
Simu (Telecommunicatins Traffic Monitoring System) baada ya kufungua rasmi
Sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho. |
 |
Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo. |
 |
Picha ya pamoja na Mkamu wa Rais Dk Bilal. (Picha
na OMR)
CCM YAFANYA KUFURU TUNDUMA JIONI HII, MAELFU WAFURIKA MKUTANONI, WAMBEBA NAPE JUU KWA JUU
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutumia maelfu ya wananchi katika
Uwanja wa Shule ya Msingi Mwaka, mjini Tunduma, wilayani Momba, jioni
hii, Nov 28, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya
CCM, kusikiliza kero za wananchi na kuzungumza nao njia ya kuzitatua,
katika mkoa wa Mbeya.
Wananchi
wakiwa wamembeba Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa
mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika
uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani
Mbeya, leo.
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye 'akihutoa dozi' alipohutubia
katika mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika
uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani
Mbeya.
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akitoa 'dozi' katika mkutano
mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika uwanja wa
shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya.
Dk Asha-Rose Migiro akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano uliofanyika uwanja wa shule ya Mwaka, Tunduma.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk Asha-Rose Migiro (katikati mwenye miwani) akiselebuka na wananchi kwenye mkutano, Uwanja wa shule ya Mwaka, Tunduma leo.
|
|
COMMENTS