Ofisa Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh, akiteta jambo na mmliki wa duka la Vodacom, Ricky Renson,...
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, Elihuruma Ngowi na Upendo Happiness Macha wakifungua shampeni kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom lililoko Mzambarauni, Gongolamboto. |
Vodacom continues to bring services closer to customers
· Opens 67th shop at Gongo la Mboto
Dar es Salaam, 23rd August, 2013 … Vodacom Tanzania continued to bring customer care services to its customers in a move aimed at giving efficient and effective services across the country.
Today, the Vodacom has opened its 67th customer care shop at Gongo la Mboto, Dar es Salaam, and this makes it the telecommunications company with the highest number of shops in the market.
Speaking during the launch of the shop, Vodacom Tanzania Chief Officer Sales and Distribution, Hassan Saleh, said that the company will continue opening as many shops as possible in order to reduce congestion in the already existing shops. Some of the company's shops in Dar es Salaam are situated at, among others, Mlimani City Mall, Ohio Street, RDK Victoria, Samora Avenue, and Ali Hassan Mwinyi Road.
The services to be offered in the new shop, Saleh, include Internet activation, device sales and configuration, M-Pesa and after sales support.
"Our customer base has experience a tremendous growth, and we are therefore looking for ways of bringing services closer to the people so as to avoid congestion and wastage of time," said Saleh, adding that, "The opening of this outlet will not only help in main services available, but it is also an employment opportunity for Tanzanians."
So far, according to Saleh, Vodacom has given direct employment to over 500 individuals and over 30,000 Tanzanians indirectly. Plans are also underway to open shops at Kimara, Msimbazi, and Kigogo.
Vodacom yasogeza zaidi huduma kwa wateja
Agosti 23, 2013 …KATIKA kukidhi haja ya utoaji wa huduma kwa wateja nchini, Kampuni ya Vodacom Tanzania imeendelea kupanua wigo wa huduma zake kwa kufungua duka jipya (Vodashop) katika eneo la Gongo lamboto jijini Dar es Salaam.
Ufunguzi wa duka hilo ni katika harakati za kuendelea kusogeza huduma za mawasiliano karibu na wateja na kufanya mauzo ya bidhaa mbalimbali za mtandao huo kuwa karibu zaidi ikiwemo huduma za kutuma na kupokea fedha (M-PESA), Intaneti, sambamba na vifurushi mbalimbali.
Akizungumzia wakati wa uzinduzi wa maduka hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rene Meza, alisema Vodacom ni kampuni pekee ambayo imeendelea kuongoza kwa kuwa na maduka mengi ya mauzo na huduma kwa wateja kwa kufikisha maduka 67 kwa jijini Dar es Salaam huku ikitarajia kufungua maduka mengine zaidi.
Aliongeza kuwa ili kufanikisha azma ya kukidhi mahitaji ya huduma kwa wateja wa kampuni hiyo --Vodacom Tanzania imeamua kuongeza idadi ya maduka yake jijini Dar es Salaam kufikia 24 kutokana na mahitaji makubwa zaidi.
"Ukuaji wa huduma kwa kampuni ya Vodacom umekuwa mkubwa sana, huduma kama ya M – Pesa sasa imepanuka kwa kasi ambapo kwa sasa kampuni yetu inatoa huduma kwa watanzania zaidi ya milioni 20. Hivyo, kufuatia mafanikio haya tunalazimika kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya uhakika kwa wateja wetu," alisema Bw. Meza, na kuongeza kuwa, "Kuongoza katika sekta ya mawasilaino kuna changamoto zake,hivyo ni lazima tuhakikishe tunaendana na kasi ya ukuaji wa huduma zetu ili kuendana na ongezeko la watu wa aina mbalimbali."
Aidha Bw. Meza alisema kuwa kufunguliwa kwa duka hilo hivi sasa si tu kunaboresha upatikanaji wa huduma bali ni fursa pekee ya kuendelea kupanua wigo wa ajira kwa watanzania.
"Ufunguzi wa duka hili unatoa fursa ya ajira kwa Watanzania. Halikadhalika ufunguzi huu umejumuisha ajira kwa wafanyakazi zaidi ya 10 ambao watatoa huduma kwa wateja wetu hivyo ni hatua kubwa tumetengeneza ajira kwa wafanyakazi wapya. Hadi kufikia sasa, Vodacom imetoa ajira za moja kwa moja kwa wafanyakazi 500 na wengine zaidi ya 30,000 wenye ajira zisizo za moja kwa moja," alisema.
Kufuatia uzinduzi wa duka hilo la huduma za mawasiliano ya simu maeneo ya Gongolamboto, Kampuni ya Vodacom iko mbioni kufungua maduka mengine katika maeneo ya Kimara, Kigogo, na Msimbazi hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Upanuzi huu wa wigo wa huduma za mawasiliano ya simu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania unafuatia uwekezaji kwenye mfumo wa mawasiliano wa 3G na 4G mfumo ambao unaotumia teknolojia mpya ya mawasiliano kazi iliyofanywa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
COMMENTS