Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewashauri hospitali ya CCBRT kufikisha ujumbe wa Fistula kati...
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewashauri hospitali ya CCBRT kufikisha ujumbe wa Fistula katika kila wilaya hapa nchini hata kwa kutumia radio jamii.
Makamu wa Rais amesema hayo leo alipofanya ziara katika hospitali hiyo iliyopo Msasani jijini Dar Es Salaam.
Makamu wa Rais amesema inasikitisha kuona asilimia kubwa ya wagonjwa wa Fistula ni wasichana wadogo.
Makamu wa Rais ameipongeza Hospitali ya CCBRT kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa wote.
Hospitali ya CCBRT ina miaka 25 kwenye huduma na imekuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa kutoka makundi maalum kwa mfano: walemavu, wasioona, viziwi na sasa inapokea wagonjwa zaidi ya wagonjwa700 kwa siku.
Makamu wa Rais ametoa wito kwa CCBRT na Serikali kuelekeza nguvu kwenye kuzuia kwa kutoa elimu ili wasichana wajue na waelewe elimu ya uzazi na kuwawezesha.
Mwisho, Makamu wa Rais alitoa shukrani kwa kazi kubwa inayofanywa na hospitali ya CCBRT hapa nchini na kuahidi kuendelea kuwa Balozi wa Fistula.
Mapema kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais Kuhutubia, Waziri wa ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alisema anaipongeza CCBRT kwa kutoa huduma bila faida na kusema wapo kwenye mpango wa kufanya mazungumzo yatakayoiwezesha CCBRT kuwa kituo kikuu cha kutoa huduma kwa wagonjwa wa Fistula nchini.
COMMENTS