TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA (TEWW) KUENDELEA KUWA KITOVU CHA KUTOA ELIMU BORA.

Taasisi ya Elimu ya Watu wazima yaendelea Kujizatiti katika kutoa elimu bora kwa wale waliokosa elimu katika mfumo rasmi ili waweze kuch...




Taasisi ya Elimu ya Watu wazima yaendelea Kujizatiti katika kutoa elimu bora kwa wale waliokosa elimu katika mfumo rasmi ili waweze kuchangia katika kujenga uchumi wa Viwanda.
Kaimu Mkurugenzi wa TEWW Dkt. Kassimu Nihuka amesema hayo leo jijini Dar es Salaam, wakati wa kufunga warsha ya uandaaji wa mihtasari ya Fizikia na kemia iliyowashirikisha walimu wa masomo hayo kutoka baadhi ya shule za sekondari za jijini Dar es Salaam
 “Katika kuboresha utoaji wa Elimu ya Sekondari nje ya mfumo rasmi ilishakamilisha uandishi wa mihtasari ya masomo ya Hisabati, Biolojia, Uraia, Historia, Jiografia, Kiswahili na Kiingereza na ambayo inatumika katika vituo vinavyotoa elimu ya Sekondari nje ya mfumo rasmi mikoa yote nchini. “ Alisisitiza Dkt. Nihuka
Kupitia jukumu la kutoa elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi TEWW imesajili jumla ya vituo 547, kati ya hivyo 93 vinaendeshwa na TEWW na vingine 454 vinaendeshwa na wadau. Jumla ya wanafunzi 10,420 wakiwemo wanawake 6,074 (58.3%) na wengine 4,346 (41.7%) wanaume wanasoma elmu ya sekondari nje ya mfumo rasmi nchi nzima kwa kutumia mitaala iliyoandaliwa na TEWW.
Ili kuwajengea wanafunzi msingi wa masomo ya sayansi hususani Fizikia na Kemia, TEWW imeandaa mitaala ya masomo haya itakayotumika katika kutoa elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi. Kwa sasa wanafunzi wetu wa sekondari wanasoma masomo saba likiwemo somo la bailojia pamoja na Hesabu. Uandaaji wa mitaala ni moja ya majukumu ya TEWW kisheria.
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Namba 12 ya mwaka 1975 na kupewa majukumu mbalimbali.Pamoja na majukumu mengine, Taasisi inajukumu la kutoa elimu ya sekondari kwa njia ya ujifunzaji huria na masafa pamja na mafunzo ya jioni pamoja na kuandaa mitaala kwa ajili ya kutoa elimu nje ya mfumo rasmi.
Mkuu wa Idara ya Elimu Masasa (TEWW), Baraka Kionywaki akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari juu ya umuhimu wa kuwekeza katika masomo ya fikizia na kemia katika elimu nje ya mfumo rasmi nchini tanzania. Kulia ni Kaimu  Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt. Kassimu Nihuka. (Picha na TEWW)


Wataalamu wa Uandaaji wa Mitaala ya masomo ya Fikizia na Kemia wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu  Wazima (TEWW) Dkt. Kassimu Nihuka (hayupo pichani) Jijini Dar es Salaam.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA (TEWW) KUENDELEA KUWA KITOVU CHA KUTOA ELIMU BORA.
TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA (TEWW) KUENDELEA KUWA KITOVU CHA KUTOA ELIMU BORA.
https://3.bp.blogspot.com/-Krjn1jJWuTI/WtBU6W2XA1I/AAAAAAABFX4/iDAN3QAVqU8bn589VNr2FJcdcfC39GkkwCLcBGAs/s640/1%2B%252813%2529.JPG
https://3.bp.blogspot.com/-Krjn1jJWuTI/WtBU6W2XA1I/AAAAAAABFX4/iDAN3QAVqU8bn589VNr2FJcdcfC39GkkwCLcBGAs/s72-c/1%2B%252813%2529.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/taasisi-ya-elimu-ya-watu-wazima-teww.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/taasisi-ya-elimu-ya-watu-wazima-teww.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy