Januari 28, 2013: Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Edmund Sengondo Mvungi (katikati) akibadilishana mawazo na Makamishina wa...
Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyekuwa akipatiwa matibabu nchini Afrika
Kusini amefariki dunia leo..
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Assaa Rashid leo jioni (Jumanne, Novemba 12, 2013), Dk Sendongo Mvungi majira
ya saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini akiwa katika Hospitali ya
Milpark.
“Kwa
masikitiko makubwa, Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dk
Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo
jijini Johannesburg nchini
Afrika Kusini amefariki dunia leo (Jumanne, Novemba 12, 2013) saa 8:30 mchana
kwa saa za Afrika ya Kusini,” amesema Rashid katika taarifa yake fupi ya
awali na kuongeza:
“Taratibu
za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika Kusini kuja nchini kwa
mazishi zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa kesho (Jumatano, Novemba 13,
2013),” ameongeza.
Marehemu
Dk Mvungi alisafirishwa siku ya Alhamisi, Novemba 7, 2013 kwenda nchini
Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa
Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba,
wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani
usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.
Katika
taarifa yake, Tume pia imewaomba watanzania wote kuungana na familia, ndugu,
jamaa na marafiki wa marehemu Dk Mvungi katika kuomboleza msiba huo.
Habari zilizotufikia zinasema kwamba Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengodo Mvungi amefariki
katika hospitali ya MillPark huko Afrika ya kusini alkokuwa akipata
matibabu majira ya saa 9.30 leo alasiri.
Dk Mvungi alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Novemba 3 2013, mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Katika tukio hilo watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walimvamia Dk Mvungi na kumkatakata kwa mapanga hatimaye kumwibia fedha taslimu kiasi ambacho hakikutajwa, Komputa mpakato na simu za mkononi 2 na bastola.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova alisema wanawashikilia watuhumiwa kadhaa waliowakamata na misokoto 17 ya bangi, lita 15 za pombe ya gongo ambapo zoezi hilo limewashirikisha polisi na raia wema na kuakikisha watuhumiwa wote wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni (RPC) Camilius Wambura, Dk Mvungi aliyekuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), alijeruhiwa vibaya sehemu za kichwani na kitu chenye ncha kali.
Kamanda Wambura alisema kuwa watu 6 wanasadikiwa kutekeleza zoezi la uvunjaji wa nyumba ya Dk Mvungi, majira ya saa 7 za usiku wakidai awape fedha wakati alipokataa walimpiga na mapanga ambapao kati ya watu sita waliokuwepo nyumbani siku hiyo ni marahemu Dk Semvungi pekee aliyejeruhiwa.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Nchini Jaji mstaafu Joseph Warioba amethibitisha kufariki kwa Dk Sengondo mvungi mida ya saa 9.30 kwenye hospitali ya Milpark Afrika Kusini.
Taratibu za kuurejesha mwili wa Dk Mvungi zinaendelea kufanywa na ubalozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini.
Mpaka sasa watu 9 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuhusika na tukio la mauwaji ya Dk huyo aliyeondoka wakati bado nguvu, maarifa, taaluma na mchango wake mkubwa ulikuwa unahitajika kwa Taifa letu.
Tutaendelea kuwajuza zaidi kuhusiana na msiba huo.
'Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe'

COMMENTS