WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI MBADALA BENKI YA DUNIA, KANDA YA AFRIKA

Na. WFM- Washngton DC Mikutano ya Bodi ya Magavana ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia kwa mwaka 2018 imeanza ...




Na. WFM- Washngton DC
Mikutano ya Bodi ya Magavana ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia kwa mwaka 2018 imeanza rasmi mjini Washington D.C. Katika mikutano hiyo kutakuwa na Magavana, Mawaziri wa Fedha, Sekta Binafsi pamoja na Wanataaluma mbalimbali kuweza kujadili  hali ya uchumi wa dunia pamoja na kupunguza umasikini.
Katika mikutano hiyo Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe, kuhusu maendeleo ya hali ya uchumi wa Tanzania huku akisisitiza kwamba ni wakati mzuri sasa wa kusemea hali ya uchumi wetu kwa nguvu zote.
Akiendelea kutoa ufafanuzi Dkt Mpango alieleza hatua ambazo Serikali imezifanya ili kuweka mazingira mazuri katika sekta binafsi, na kwamba Serikali imeandaa mpango kazi wa kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji katika Taifa la Tanzania.
Pia Waziri Mpango alielezea miradi mikubwa ambayo nchi imeanza kuitekeleza, ikiwamo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa na Ujenzi wa Bwawa  kubwa la kuzalisha Umeme wa Megawati 2100 la ‘Steigler's Gorge’ katika Maporomoko ya Maji ya Mto Rufiji.
Kupitia miradi hiyo ambayo Serikali imepanga kuifanikisha kwa wakati Dkt. Mpango alimuomba Bw. Bvumbe kuendelea kuzungumza na uongozi wa Benki ya Dunia ili uweze kutusaidia katika kuwezesha uwekeza katika miradi hiyo.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe alisema kuwa anaipongeza Tanzania kwa jitihada inazozionesha hasa katika kupambana na rushwa na ametutia moyo tuendelee na juhudi zetu za kuimarisha uchumi wetu hususani katika sekta ya kilimo na pia amefurahishwa na hatua mbalimbali zinazofanya kwa ajili ya kuendeleza sekta ya viwanda.
Mwisho
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
Washington D.C

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wakwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kwa  Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe (hayumo pichani) kuhusu  mpango kazi wa kuboresha uwekezaji Tanzania.  Kushoto kwake ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha Dkt. Yamungu Kayandabila.


Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe (kulia) akimsikiliza kwa makini Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayumo pichani) wakati wa majadiliano ya namna ya kuendeleza miradi ya maendeleo nchini Tanzania, kushoto kwake ni Mshauri wa Mkurugenzi huyo Bw, Zarau Kibwe.


Picha ya pamoja ya wajumbe walioshiriki majadiliano ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe kuhusu uboreshaji wa sekta binafsi, miradi ya maendeleo, ukuaji wa uchumi pamoja na sekta ya ukuaji wa viwanda. Wanaopeana mikono kulia Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)kushoto Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe. Kutoka kulia ni Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha Dkt. Yamungu Kayandabila, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere, wa pili kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga na wa pili kushoto ni Mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, kanda ya Afrika Bw, Zarau Kibwe.




COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI MBADALA BENKI YA DUNIA, KANDA YA AFRIKA
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI MBADALA BENKI YA DUNIA, KANDA YA AFRIKA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiQfTqzHxpVOWEmzt4AF7ArbYJYhLypI-eh-T_uxv3k0m9uWaqlKpAn6reuyJJMvPcdYH4Tllx75ZqjMSd5ZuxR6TKnlOD8vae4PyvJTRMwaVqNE-TyS4TAz0KzGmeLYpnb6x7GCOId5BA/s640/IMG_2027.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiQfTqzHxpVOWEmzt4AF7ArbYJYhLypI-eh-T_uxv3k0m9uWaqlKpAn6reuyJJMvPcdYH4Tllx75ZqjMSd5ZuxR6TKnlOD8vae4PyvJTRMwaVqNE-TyS4TAz0KzGmeLYpnb6x7GCOId5BA/s72-c/IMG_2027.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/waziri-wa-fedha-na-mipango-akutana-na.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/waziri-wa-fedha-na-mipango-akutana-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy