MHE. JANUARY MAKAMBA ATEMBELEA DARASA LA KISWAHILI DMV NA RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI KUTOKA UFARANSA

MHE. JANUARY MAKAMBA ATEMBELEA DARASA LA KISWAHILI DMV  Naibu Waziri wa mawasiliano, sayansi na teknologia, Mhe. Janu...

MHE. JANUARY MAKAMBA ATEMBELEA DARASA LA KISWAHILI DMV

 Naibu Waziri wa mawasiliano, sayansi na teknologia, Mhe. January Makamba akiongozana na Afisa Ubalozi Mindi Kasiga siku ya Jumamosi Dec 7, 2013 College Park Maryland, siku alipotembelea darasa la Kiswahili DMV.
 Mhe. January Makamba akisalimiana na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania mara tu alipoingia kwenye darasa hilo Jumamosi Dec 7, 2013 College Park, Maryalnd.
 Mhe. January Makamba akipata historia fupi ya darasa hilo kutoka kwa rais wa Jumuiya Iddi Sandaly (wapili toka kushoto) siku ya Jumamosi Dec 7, 2013 Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia alipotembelea darasa hilo College Park Maryland.
 Mhe. January Makamba akisalimiana na wazazi wa watoto wa darasa la kiswahili DMV.
 Mhe. January Makamba akipata maelezo kuhusiana na watoto wa darasa la kiswahili DMV kutoka kwa katibu wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Amos Cherehani (kulia koti jeusi).
 Watoto wa darasa la kiswahili DMV wakitoa salamu kwa mhe. January Makamba (hayupo pichani)
 Mhe. January Makamba pamoja na Afisa Ubalozi Mindi Kasiga, Rais wa Jumuiya Iddi Sandaly na mwalimu mkuu wa darasa la kiswahili wakiwa wamesimama wakati watoto wa darasa la kiswahili waliopkuwa wakiimba wimbo wa taifa.
 Watoto wa darasa la kiswahili wakimwimbia mgeni wao Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba wimbo wa Taifa.
 Juu na chini baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV, watoto wa darasa la kiswahili na wazazi wakimsikizliza Mhe. January Makamba (hayupo picha) alipokua akiwathimilia hadithi watoto wa darasa la kiswahili DMV.
 
Darasa...

MVUA YA SAA CHACHE JIJINI DAR HATARI TUPU MAENEO YA TABATA

Kutokana na mvua iliyonyesha jijini Dar es Salaam, mida ya mchana wa jana baadhi ya maeneo yameathirika na mvua hiyo hususan eneo la Tabata, ambako baadhi ya nyumba zimezungukwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa iliyonyesha muda mchache uliopita jijini hapa. 
 
Mkazi wa Tabata akikatiza katikati ya maji ambapo eneo hili njia inayotumiwa na wakazi wa maeneo ya Tabata kila siku, ambapo leo njia hii imefurika maji kutokana na mvua kubwa.

RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI KUTOKA UFARANSA

Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni wakati aliposimama kwa muda katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi akiwa njiani kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano unaohusu Amani na usalama na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Bara la Africa na Ufaransa. Kulia  ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Balozi Amina Mohamed na Afisa itifaki.
Rais Dk Jakaya Kikwete akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Balozi Amina Mohamed  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa Jomo Kenyata Nairobi, Kenya alipokuwa akirejea nyumbani akitokea Paris Ufaransa ambapo alihudhuria mkutano uliohusu Amani, Usalama na Ushirikiano wa kiuchumi kati ya Ufaransa na bara la Afrika.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Mec Sadik akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere muda mfupi baada y kuwasili akitokea Paris Ufaransa ambapo alihudhuria Mkutano wa Amani,Usalama na Ushirikianokati ya Afrika na Ufaransa uliomalizika jana. (Picha na Freddy Maro)

MECHI YA KILIMANJARO STARS NA HARAMBEE STARS KUPIGWA MACHAKOS

Mechi ya kwanza ya nusu fainali ya michuano ya mwaka huu ya Kombe la Chalenji kati ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) na wenyeji Kenya (Harambee Stars) itapigwa Uwanja wa Machakos.

Kwa mujibu wa ofisa wa CECAFA, Amir Hassan mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Machakos ulioko takribani kilometa 64 kutoka jijini Nairobi. Mechi hiyo itachezwa Jumanne (Desemba 10 mwaka huu) kuanzia saa 10 kamili jioni na itaoneshwa moja kwa moja  na kituo cha televisheni cha SuperSport kupitia chaneli ya SS9.

Kilimanjaro Stars imetinga hatua hiyo baada ya kuivua ubingwa Uganda (The Cranes) kwa mikwaju 3-2 ya penalti katika mechi ya robo fainali ya michuano hiyo iliyochezwa jana Uwanja wa Aga Khan katika Jiji la Mombasa.

Hadi dakika 90 za kawaida zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 2-2. Mabao ya Kilimanjaro Stars yalifungwa na Mrisho Ngasa wakati katika mikwaju ya penalti walofumania nyavu ni Amri Kiemba, Athuman Idd na nahodha Kelvin Yondani.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MHE. JANUARY MAKAMBA ATEMBELEA DARASA LA KISWAHILI DMV NA RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI KUTOKA UFARANSA
MHE. JANUARY MAKAMBA ATEMBELEA DARASA LA KISWAHILI DMV NA RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI KUTOKA UFARANSA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEggD69zZJLq1lt89OnCJMplN4agyhg1Jt8i0wf3d-oX0d1R7LbehI8M1wo0I80zaJtzj1Puu1_3qcc6JtSiFXuMpygIaMRoO64omLwo3QWKjQk0Gx4Kqr-agP18qiUDfjSCn376nE2D17J-/s640/IMG_1318.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEggD69zZJLq1lt89OnCJMplN4agyhg1Jt8i0wf3d-oX0d1R7LbehI8M1wo0I80zaJtzj1Puu1_3qcc6JtSiFXuMpygIaMRoO64omLwo3QWKjQk0Gx4Kqr-agP18qiUDfjSCn376nE2D17J-/s72-c/IMG_1318.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2013/12/mhe-january-makamba-atembelea-darasa-la.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2013/12/mhe-january-makamba-atembelea-darasa-la.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy