RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUNGUA KIWANDA CHA SIGARA CHA MANSOOR INDUSTRIES LTD KILICHOPO KINGOLWIRA MOROGORO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz ...

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425

OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Machi, 2018 amefungua kiwanda cha kutengeneza sigara cha Philip Morris Tanzania Limited kilichopo Kingolwira Mkoani Morogoro na kuagiza viongozi wote nchini kuwalinda na kuwavutia wawekezaji.
Pamoja na agizo hilo Mhe. Rais Magufuli amewahakikishia wawekezaji wote wanaojenga viwanda kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao kuhakikisha viwanda hivyo vinakuwa na tija ili wakulima waweze kupata masoko ya uhakika ya mazao yao, Watanzania kupata ajira na Serikali kupata kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
“Niwaombe wawekezaji msisite, endeleeni kujenga viwanda vya kutosha katika nchi hii, niwaombe viongozi na watendaji wenzangu katika Serikali kuanzia Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa wilaya  mpaka Wakurugenzi mtengeneze mazingira mazuri ya kusaidia wawekezaji kuwekeza, sisi viongozi ndani ya Serikali kamwe tusije kuwa chanzo cha kuzuia wawekezaji kuwekeza” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli ameipongeza kampuni ya Philip Morris Tanzania Limited kwa uwekezaji wa kiwanda hicho uliogharimu Shilingi Bilioni 65 na kampuni ya Mansoor Industries Limited kwa uendeshaji wa kiwanda.
Meneja Mkuu wa kampuni ya Philip Morris Tanzania Bi. Dagmara Piasecka amesema uamuzi wa kampuni hiyo kuwekeza hapa nchini ni uthibitisho wa mtazamo na imani ya muda mrefu iliyonayo kwa Tanzania kutokana na kuwepo kwa mazingira mazuri ya biashara, amani na utulivu, ukuaji mzuri wa uchumi na sera nzuri ya viwanda inayosimamiwa vizuri na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mansoor Industries Limited Mhe. Mansoor Shanif Hirani amesema kiwanda hicho kilichoanza kujengwa mwaka 2017 kina uwezo wa kutengeneza sigara Milioni 400 na kulipa kodi kiasi cha Shilingi Bilioni 12 kwa mwaka, kimetoa ajira kwa watu 224 na kitaingiza fedha za kigeni kwa kuuza sigara ndani na nje ya nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe amesema mkoa huo wenye viwanda zaidi ya 3,000 unaendelea na kampeni kubwa ya ujenzi wa viwanda vingine 300 katika mwaka huu.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amemhakikishia Mhe. Rais Magufuli kuwa ujenzi wa viwanda unaendelea vizuri katika nchi nzima na amebainisha kuwa vipo viwanda vingi vilivyokamilika na vimeanza uzalishaji.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amejibu ombi la kupatiwa maji lililotolewa na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Aziz Abood kwa kumhakikishia kuwa Serikali itafanyia kazi tatizo la uhaba wa maji kwa ajili ya wakazi wa Mji wa Morogoro na maendeleo ya viwanda.
Katika mkutano huo Mhe. Rais Magufuli amesikiliza kero ya wafanyabiashara ndogondogo kunyang’anywa bidhaa zao na Manispaa ya Morogoro kwa madai ya kuendesha shughuli zao katika maeneo yasiyoruhusiwa, na ameiagiza manispaa hiyo kuacha kuwanyanyasa na badala yake waboreshe mazingira yao na kuepusha hatari ya milipuko ya magonjwa.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Morogoro

15 Machi, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage mara baada ya kufungua kiwanda cha Sigara cha Mansoor Industries ltd kilichopo chini ya leseni ya Phillip Morris Tanzania katika eneo la Kingolwira mkoani Morogoro. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Phillip Morris Tanzania Dagmara Piasecka akipiga makofi, wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe pamoja na Mmiliki wa kiwanda cha Sigara Mansoor Shanif Hirani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Tumbaku inayotumika katika utengenezaji wa Sigara hizo za Marlboro mara baada kufungua kiwanda hicho cha Sigara mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mojawapo ya hatua katika utengenezaji wa Sigara mara baada ya kufungua kiwanda hicho mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mojawapo ya vifungashio vya Sigara hizo kiwandani hapo mara baada ya kukifungua.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Msanii mkongwe Selemani Msindi au Afande Selle mara baada ya kuhutubia wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Msanii mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle mara baada ya kutoa burudani ya mziki na kutangaza rasmi kuhamia katika Chama cha Mapinduzi CCM katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Chifu Kingalu Mwanabanzi wa Kabila la Waluguru wa Morogoro mara baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi waliofika katika kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.

Msanii mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle akipongezwa na baadhi ya wananchi mara baada ya kuimba wimbo wake wa Mimi ni Msanii katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe mara baada ya kuzindua kiwanda cha Sigara mkoani Morogoro.

Msanii mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle akitumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia mfanyabiashara mdogo (Machinga) wa  Mama Havintoshi ambaye aliwasilisha kero yake ya kunyanyaswa wakati akifanya biashara zake katika stendi ya daladala ya mjini Morogoro.

Mfanyabiashara mdogo (Machinga) wa  Mama Havintoshi ambaye aliwasilisha kero yake ya kunyanyaswa wakati akifanya biashara zake katika stendi ya daladala ya mjini Morogoro akichangiwa fedha na wadau mbalimbali mara baada ya kero yake kupatiwa ufumbuzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Msanii mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle mara baada ya kutoa burudani ya mziki na kutangaza rasmi kuhamia katika Chama cha Mapinduzi CCM katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mmiliki wa kiwanda hicho cha Sigara Mansoor Shanif Hirani mara baada kufungua kiwanda hicho. (PICHA NA IKULU)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425

OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Machi, 2018 amefungua kiwanda cha kutengeneza sigara cha Philip Morris Tanzania Limited kilichopo Kingolwira Mkoani Morogoro na kuagiza viongozi wote nchini kuwalinda na kuwavutia wawekezaji.
Pamoja na agizo hilo Mhe. Rais Magufuli amewahakikishia wawekezaji wote wanaojenga viwanda kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao kuhakikisha viwanda hivyo vinakuwa na tija ili wakulima waweze kupata masoko ya uhakika ya mazao yao, Watanzania kupata ajira na Serikali kupata kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
“Niwaombe wawekezaji msisite, endeleeni kujenga viwanda vya kutosha katika nchi hii, niwaombe viongozi na watendaji wenzangu katika Serikali kuanzia Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa wilaya  mpaka Wakurugenzi mtengeneze mazingira mazuri ya kusaidia wawekezaji kuwekeza, sisi viongozi ndani ya Serikali kamwe tusije kuwa chanzo cha kuzuia wawekezaji kuwekeza” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli ameipongeza kampuni ya Philip Morris Tanzania Limited kwa uwekezaji wa kiwanda hicho uliogharimu Shilingi Bilioni 65 na kampuni ya Mansoor Industries Limited kwa uendeshaji wa kiwanda.
Meneja Mkuu wa kampuni ya Philip Morris Tanzania Bi. Dagmara Piasecka amesema uamuzi wa kampuni hiyo kuwekeza hapa nchini ni uthibitisho wa mtazamo na imani ya muda mrefu iliyonayo kwa Tanzania kutokana na kuwepo kwa mazingira mazuri ya biashara, amani na utulivu, ukuaji mzuri wa uchumi na sera nzuri ya viwanda inayosimamiwa vizuri na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mansoor Industries Limited Mhe. Mansoor Shanif Hirani amesema kiwanda hicho kilichoanza kujengwa mwaka 2017 kina uwezo wa kutengeneza sigara Milioni 400 na kulipa kodi kiasi cha Shilingi Bilioni 12 kwa mwaka, kimetoa ajira kwa watu 224 na kitaingiza fedha za kigeni kwa kuuza sigara ndani na nje ya nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe amesema mkoa huo wenye viwanda zaidi ya 3,000 unaendelea na kampeni kubwa ya ujenzi wa viwanda vingine 300 katika mwaka huu.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amemhakikishia Mhe. Rais Magufuli kuwa ujenzi wa viwanda unaendelea vizuri katika nchi nzima na amebainisha kuwa vipo viwanda vingi vilivyokamilika na vimeanza uzalishaji.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amejibu ombi la kupatiwa maji lililotolewa na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Aziz Abood kwa kumhakikishia kuwa Serikali itafanyia kazi tatizo la uhaba wa maji kwa ajili ya wakazi wa Mji wa Morogoro na maendeleo ya viwanda.
Katika mkutano huo Mhe. Rais Magufuli amesikiliza kero ya wafanyabiashara ndogondogo kunyang’anywa bidhaa zao na Manispaa ya Morogoro kwa madai ya kuendesha shughuli zao katika maeneo yasiyoruhusiwa, na ameiagiza manispaa hiyo kuacha kuwanyanyasa na badala yake waboreshe mazingira yao na kuepusha hatari ya milipuko ya magonjwa.
Mhe. Rais Magufuli amerejea Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Morogoro

15 Machi, 2018

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUNGUA KIWANDA CHA SIGARA CHA MANSOOR INDUSTRIES LTD KILICHOPO KINGOLWIRA MOROGORO
RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUNGUA KIWANDA CHA SIGARA CHA MANSOOR INDUSTRIES LTD KILICHOPO KINGOLWIRA MOROGORO
https://lh6.googleusercontent.com/s45TZxYk4TvJVF2WBFP1hB653Oep3NIeaqfRqxhPCbC5_1OHAmOIRRZsD_nUTz5zFXivTOYaCaeuybeZulUMZPj-AZp6SaHiKVOtgbRNvTKp-1rsMOOhk3iP-If3njM2o5cRQsiXR3bXMa3i2w
https://lh6.googleusercontent.com/s45TZxYk4TvJVF2WBFP1hB653Oep3NIeaqfRqxhPCbC5_1OHAmOIRRZsD_nUTz5zFXivTOYaCaeuybeZulUMZPj-AZp6SaHiKVOtgbRNvTKp-1rsMOOhk3iP-If3njM2o5cRQsiXR3bXMa3i2w=s72-c
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/rais-mhe-dkt-magufuli-afungua-kiwanda_15.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/rais-mhe-dkt-magufuli-afungua-kiwanda_15.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy