MPINA ALIA NA WANAODANGANYA CHAPA

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye kofia) akimshika mkia ng’ombe kuangalia kama amepigwa chapa alipotembelea mnada wa Ki...

 Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye kofia) akimshika mkia ng’ombe kuangalia
kama amepigwa chapa alipotembelea mnada wa Kizota nje kidogo ya mji
wa Dodoma leo ambapo ametoa tathimini ya upigaji chapa unaoendelea
nchini.
 Naibu Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega(aliyenyosha mkono)akimwonyesha  Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye kofia) chapa ya mifugo alipotembelea
mnada wa Kizota nje kidogo ya mji wa Dodoma leo ambapo wametoa tathimini
ya upigaji chapa unaoendelea nchini.Nyuma yake ni Kaimu Katibu Mkuu
wa Mifugo Bi. Selina Lyimo, wakwanza kushoto mwenye shati la kitenge
ni Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Ugani wa Wizara Dkt. Angelo
Mwilawa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi anayeshughulikia  Sekta
ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo akishiriki zoezi la upigaji chapa
mifugo mkoani Kigoma hivi karibuni. Tarehe ya mwisho kitaifa ya uhitimishaji
wa kupiga chapa mifugo yote nchini iliyotolewa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa
Kasim Majaliwa Majaliwa ni 31/3/2018.


Na. John
Mapepele, Dodoma



Waziri
wa  Mifugo na Uvuvi
Mheshimiwa, Luhaga Mpina
ametoa onyo kali kwa viongozi wa Serikali katika Halmashauri zote nchini
wanayoihujumu operesheni maalum ya kitaifa ya kupiga chapa  mifugo inayoendelea nchi
nzima kwa kutoa
taarifa za uongo zinazoonesha kuwa mifugo mingi imepigwa chapa tofauti na hali
halisi ambapo amesema Wizara yake itapita kila Wilaya kufanya tathmini ya
kina  baada ya tarehe ya mwisho ya
upigaji chapa kitaifa iliyotolewa na Mheshimiwa Waziri Mkuu, Marchi 31
mwaka  huu ambapo
watendaji watakaobainika
kudanganya sheria zitachukua mkondo wake.



Aidha ametoa
maelekezo kwa Wakuu wote
wa Mikoa na Wilaya kote nchini kuhakikisha kwamba mifugo yote inatakiwa iwe
imepigwa chapa hadi tarehe ya mwisho iliyopangwa na kusiwe na
visingizio  vyaaina
yoyote ikiwa ni utekelezazi wa Sheria
ya Utambuzi,Usajili na Ufuatiliaji  wa
Mifugo Namba 12 ya Mwaka 2010 na kanuni zake za mwaka 2011.



Maelekezo
hayo  aliyatoa jana akiwa
Naibu Waziri wake Mhe.
Abdalah Ulega na Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi walipotembelea mnada wa
upili wa Kizota pembeni kidogo wa mji wa Dodoma kutoa tathmini ya zoezi la
upigaji chapa nchini kabla ya siku ya mwisho
ya upigaji chapa mifugo yote nchini ambayo ni tarehe
31/3/2018.



Waziri Mpina alisema,
kulingana  na takwimu
ambazo Wizara imeletewa
hadi
tarehe 11
Machi, 2018
inaonyesha
kwamba,  jumla ya
ng’ombe 16,744,355
kati ya
17,390,090
sawa na asilimia 96.3 ya
ng’ombe wote nchini
wamepigwa chapa.
Aidha, jumla
ya Punda 51,494
wamepigwa chapa nchini.






“Hivi
karibuni nilitembelea mnada wa Pugu nikaangalia idadi ya mifugo iliyopigwa
chapa hawafiki hata asilimia tano, lakini leo hapa sote tumeshuhudia idadi ya
mifugo wote waliopigwa chapa katika mnada huu wa Kizota ni chini ya asilimia
mbili. Minada hii ndiyo mikubwa nchini ukianzia wa Pugu na huu ni wa Kizota ni
wa pili kwa hiyo inadhihirisha kwa uhakika kabisa kuwa kuna udanganyifu mkubwa
unaofanywa na watendaji wasio waaminifu wanaopotosha taarifa.”
Alisistiza
Mpina



Alisema
wilaya nyingine zimeleta takwimu ambazo zinaonyesha zimepia chapa mifugo kwa
zaidi ya asilimia elfu moja ambapo amezionya kutojiingiza katika matatizo kwa
kuendelea kudanganya.



Aidha
alisema tathmini ya jumla kuanzia mwezi Disemba
2017
hadi tarehe 11
Marchi, 2018

inaonyesha kwamba, Halmashauri 85 zimepiga
chapa kwa asilimia 100
na zaidi;
Halmashauri 86
zimepiga chapa kati ya asilimia 50 na 100, na Halmashauri 4 zimepiga chapa chini ya
asilimia 50.



Alizitaja
Halmashauri hizo kuwa ni Kasulu, Madaba, Arusha na Meru, ambapo
alisema  Halmashauri
zilizobaki ni miongoni mwa Halmashauri zenye ng’ombe wengi wa maziwa nchini
wanaotarajiwa kuvishwa hereni. Halmashauri hizo ni Manispaa ya Ubungo, Temeke,
Moshi, Kinondoni na Ilala.



Alisema
Halmashauri zingine zenye ng’ombe wengi wa maziwa kuliko wanaochungwa ni
Rungwe, Busokelo na Kibaha.



Alisema
tathmini ya zoezi la chapa tangu kuongezwa kwa muda kutoka tarehe
31 Januari, 2018
hadi sasa inaonyesha
ongezeko la Halmashauri 14
zilizopiga
chapa mifugo zaidi ya asilimia 100
na kupungua kwa Halmashauri 8 zilizopiga
chapa kati ya asilimia 50
– 100
na
kupungua kwa Halmashauri
25
zilizopiga
chapa chini ya asilimia
50.



“Napenda
kutoa  maelekezo kwa
wafugaji kwamba
mifugo yote ipigwe chapa  popote ilipo
ilimradi ni ya Tanzania
ili kuepuka
migogoro isiyo ya lazima
baada ya tarehe
ya mwisho iliyopangwa na Serikali ambayo ni mwisho wa mwezi huu
na  ninaomba ieleweke
kuwa visingizio
vyoyote  havitakubalika’
Alisisitiza
Waziri Mpina.



Akielezea
umuhimu wa zoezi hilo, Mpina alisema kwamba kukamilika kwa zoezi hilo kutasaidia
kutambua mifugo yote iliyopo nchini ili kukidhi mahitaji  ya biashara katika masoko ya
ndani na
nje  ya nchi,kudhibiti
magonjwa ya mifugo
na kudhibiti wizi wa mifugo na usafirishaji holela.



Aidha
kutasaidia  kuepusha  migogoro inayoendelea maeneo
mbalimbaili
nchini  baina ya
wafugaji,wakulima pamoja
na watumiaji wengine wa raslimali ardhi na kutawezesha Serikali kupata idadi
sahihi ya mifugo iliyonayo ili kupanga kupanga mipango
inayotekelezeka  na
kuleta mapinduzi katika sekta hiyo.



Alisema  Zoezi
la upigaji chapa ni endelevu kwa mifugo
ambapo alisema ng’ombe na punda wanaotimiza
miezi sita wanatakiwa kupiga chapa.






Awamu ya kwanza ya zoezi
la upigaji chapa ng’ombe na punda nchini ilianza rasmi tarehe 14 Desemba, 2016 kufuatia
Agizo la
Mheshimiwa Waziri Mkuu na ilitarajiwa kukamilika tarehe Desemba 31, 2017.  Tathmini iliyofanywa baada ya
kukamilika
awamu hiyo ya Desember, 2017
ilionyesha jumla ya ng’ombe 7,401,661
sawa na asilimia 38.5 ya lengo
walikuwa wamepigwa chapa. Kutokana na kiwango kidogo cha ng’ombe waliokuwa
wamepigwa chapa wakati huo, Waziri wa Mifugo, Mheshimiwa Luhaga Mpina aliongeza
muda wa kukamilisha zoezi hili hadi tarehe 31
Januari, 2018
. Hadi kufikia tarehe 31
Januari, 2018
jumla ya ng’ombe 15,192,565
sawa na asilimia 87.4 walikuwa wamepigwa chapa.






Aidha jumla ya punda 6,944 walikuwa wamepigwa chapa kati ya
punda 572,353
wanaotarajiwa kupigwa
chapa nchini. Pia, jumla ya ng’ombe wa maziwa 58,214 walikuwa
wamevishwa hereni kati ya ng’ombe wa maziwa 782,995 wanaotarajiwa
kuvishwa hereni.
Pamoja na muda huo kuongezwa, Halmashauri nyingi zilikuwa bado hazijakamilisha
zoezi hili kikamilifu. Kutokana na mapungufu mbalimbali yaliyojitokeza Mh.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kasim
Majaliwa Majaliwa
alilazimika kuongeza muda zaidi mpaka tarehe 28 Machi, 2018 na
kuziagiza Mamlaka ya Serikali za Mitaa kusimamia
zoezi hili kikamilifu kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kumpa  taarifa ya Utekelezaji ifikapo
Machi 31, mwaka
huu.






Wakati huo huo, Waziri
Mpina alisema kuwa  Wizara itafanya
mageuzi makubwa ya kupanua kiwanda cha machinjio ya nyama  cha Dodoma(TMC) ili kiweze
kukidhi mahitaji
ya sasa  ya mifugo ambapo
kumekuwa na
ongezeko kubwa ya mifugo nchini.






Mmoja wa wafanyabiashara
wa mifugo Shabani zuberi, alimweleza
Waziri kuwa  kwa
sasa  gharama ya
uchinjaji wa nyama katika
machinjio ya kiwanda hicho ni juu ukilinganisha na machinjio nyingine nchini
ambapo ni shilingi elfu ishirini   kwa
ng’ombe mmoja  na
kwamba  nyama kwa ajili
ya soko la ndani inanyimwa
sehemu ya kugandishia tofauti na nyama inayosafirishwa kwenda nje ya nchi suala
ambalo linawafanya wapate  hasara
kubwa  nyama ikishindwa
kuuzika katika
siku husika kutokana na kukosa sehemu ya kugandishia.






Akijibu hoja hizo, Mpina
aliielekeza menejimenti ya kiwanda hicho kukaa na Wizara na kuangalia namna
bora ya kuweka gharama ya uchinjaji itakayoendana na hali halisi ya bei la
soko.






Aidha alikiagiza kiwanda
kuanza mara moja kutoa huduma ya kugandisha na kuhifadhi nyama  ya walaji wa ndani ambapo pia
alitoa wiki
mbili kuhakikisha huduma ya maji inaletwa na kiwanda hicho katika machinjio ya
Kizota.Alisisitiza kuwa Mnada wa Kizota utaboreshwa na Serikali kwa kuwa
unaingiza milioni 624 kwa mwaka   hivyo
ukiboreshwa miundo mbinu yake utaongeza mapato yake.






“Hatuwezi kuwajali watu
kutoka nje ya nchi na usiwajali wananchi wako wa ndani ya nchi, naamuru kwamba
TMC wapeni huduma ya kugandisha
nyama
wateja wenu wa soko la ndani” alisistiza Mpina.






Alimpongeza
Naibu Waziri, Abdalah Ulega kwa juhudi anazozifanya  za kuhakikisha minada yote
nchi inakuwa  na
miundombinu bora ambapo awali Mhe. Ulega alitembelea mnada wa
Kizota  na kujadiliana na
wadau wa mnada huo
kuhusiana na mambo mbalimbali.



Naye
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo Selina
Lyimo alimshukuru Waziri Mpina kwa maelekezo aliyoyatoa kwa Wizara na
kumhakikishia kwamba yatatekelezwa mara moja ili kuleta mageuzi  na mapinduzi makubw a katika
sekta.



Aidha
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti Mafunzo na Ugani,Angelo Mwilawa
amesema  Idara yake
itaendelea kuratibu tafiti
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo hususan kwenye eneo la malisho na
uzalishaji wa mbegu bora za mifugo ili wafugaji waweze kufuga
kisasa

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MPINA ALIA NA WANAODANGANYA CHAPA
MPINA ALIA NA WANAODANGANYA CHAPA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhmarRxsE6g3z3PXB_RQCP4Er9r5UU-EpyqUdniBzuhBXb6iwoGgB_7Mpez84Q3Kl5nTd4oqmpv_o5Wirg0pEE0vI4HXMCYUHA3xKxbHfDgVjGpiwgm4OPxdNgAgBcPsxwfND0dl6h9btc/s640/aaa.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhmarRxsE6g3z3PXB_RQCP4Er9r5UU-EpyqUdniBzuhBXb6iwoGgB_7Mpez84Q3Kl5nTd4oqmpv_o5Wirg0pEE0vI4HXMCYUHA3xKxbHfDgVjGpiwgm4OPxdNgAgBcPsxwfND0dl6h9btc/s72-c/aaa.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/mpina-alia-na-wanaodanganya-chapa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/mpina-alia-na-wanaodanganya-chapa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy