DK. KIGWANGALLA AMALIZA MGOGORO WA HIFADHI NA WANANCHI WILAYANI RUFIJI

Na Hamza Temba (WMU) -  Rufiji, Pwani .................................................................................... Wazi...





Na Hamza Temba (WMU) -  Rufiji, Pwani
....................................................................................

Waziri wa Maliasili na
Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amemaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya
miaka minne baina ya Hifadhi ya Msitu wa Utete maarufu kama Msitu wa Kale na vitongoji
vinavyopakana na hifadhi hiyo vya Siasa, Nyawanje, Kindwitwi na Utunge katika
wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.

Dk. Kigwangalla amemaliza
mgogoro huo kwa kumuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania,
Prof. Dos Santos Silayo kuunda timu ya wataalamu watakaoshirikiana na wataalamu
wa mkoa wa Pwani na wilaya ya Rufiji kwa ajili ya kufanya tathmini ya eneo
lenye mgogoro na kuanzisha mchakato wa kisheria wa kurekebisha mipaka ya eneo
hilo na hatimaye kuligawa kwa wananchi.

Dk. Kigwangalla ametoa
agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Utete,
wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua
migogoro baina ya hifadhi na wananchi mkoani humo.

“Nimejiridhisha kwamba
hakutokuwa na madhara yeyote yale, kama tutamega eneo la msitu wa Hifadhi
kidogo ambalo wananchi wamekuwa wakilima miaka yote hii na kulirusha kwa
wananchi kwa ajili ya shughuli za kilimo kuliko kuendelea kulihifadhi wakati
wananchi wanakosa mahala pa kupata riziki yao.

“Naagiza Mtendaji Mkuu
wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, uunde timu ya wataalam waje
washirikiane na wataalam wa mkoa na wilaya, wafanye tathmini kwenye lile eneo
ambalo wananchi wamekuwa wakilima kabla hata msitu haujawa ‘gazerted’
(haujatagazwa) kuwa hifadhi ili muone ni kwa kiasi gani mnaweza mkamega eneo na
kulirudisha kwa wananchi ili waweze kuendelea na kilimo,” aliagiza Dk.
Kigwangalla.

Ameagiza pia kamati
hiyo ifanye tathmini ya eneo la chemchem ambalo ni sehemu ya hifadhi hiyo ambalo
limevamiwa kwa kiasi kikubwa na makazi ya wananchi ili waweze kurekebisha
mipaka yake na hatimaye wananchi wabaki na eneo lao la makazi na eneo litakalobakia
liendelee kuhifadhiwa.

“Kamati hiyo pia ije
ifanye tahtmini inawezaje kuhamisha mipaka ya hifadhi ili kupisha zile nyumba
ambazo zimeshajengwa pale kwa sasa na hapo sasa wananchi wawe hawana mgogoro na
hifadhi, waishi kwenye eneo lao na waiache hifadhi upande wa pili, lakini sasa
waishi kwa mujibu wa sheria kuliko ilivyo hivi sasa tunavyowachukulia kama
wavamizi;” alisema Dk. Kigwangalla.

Aidha Dk. Kigwangalla
ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kutafuta eneo mbadala la
msitu ambalo ni mali ya vijiji likabidhiwe kwa Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania ili liweze kuhifadhiwa ikiwa ni fidia ya eneo hilo la Hifadhi ya Msitu
wa Utete litakalokabidhiwa kwa wananchi kwa ajili ya kilimo na makazi.

Mbali na maagizo hayo Dk.
Kigwangalla ameagiza pia wananchi waliolima kwenye bonde katika Hifadhi hiyo
wasiondolewe katika msimu huu wa kilimo wakati zoezi la uwekaji wa mipaka
likiwa linaendelea.

Hifadhi ya Msitu wa
Utete ilianzishwa kwa tangazo la Serikali Na. 1cap 132p 1351 la tarehe 1
Oktoba, 1957 ikiwa na jumla ya ekari 2,346. Desemba 2015 msitu huo ulipimwa
tena na kuchorewa ramani.

Wananchi wanaozunguka
hifadhi hiyo wamedai kuwepo katika baadhi ya maeneo hayo ya hifadhi hata kabla
ya kuanzishwa kwa hifadhi hiyo, hivyo wameiomba Serikali iwamegee maeneo katika
hifadhi hiyo ili waweze kuendeleza shughuli zao za kilimo na makazi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo kuhusu kivutio cha utalii cha Chemchem
ya Maji ya Moto yanayofikia nyuzi joto 75 katika Msitu wa Hifadhi wa Chemchem wakati
wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika
Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akijadili jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya
Rufiji, Rajab Mbonde na Mbunge wa Rufiji, Mohammed Mchengerwa kuhusu mgogoro wa
mpaka wa Hifadhi ya Msitu wa Utete na vijiji jirani wakati wa ziara yake ya kutatua
migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi wilayani humo mkoani Pwani jana
ambapo alitoa maelekezo kadhaa ya kufanywa ili kumaliza mgogoro huo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Rufiji,
Rajab Mbonde kuhusu mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Msitu wa Utete na vijiji
jirani wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya
hifadhi wilayani humo mkoani Pwani jana ambapo alitoa maelekezo kadhaa ya kufanywa
ili kumaliza mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Rufiji, Mohammed Mchengerwa. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Utete katika wilaya ya Rufiji
Mkoani Pwani kuhusu mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Msitu wa Utete na vijiji
jirani wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya
hifadhi wilayani humo mkoani Pwani jana ambapo alitoa maelekezo kadhaa ya kufanywa
ili kumaliza mgogoro huo.
Baadhi ya wananchi walioshiriki mkutano huo.
Baadhi ya wananchi walioshiriki mkutano huo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DK. KIGWANGALLA AMALIZA MGOGORO WA HIFADHI NA WANANCHI WILAYANI RUFIJI
DK. KIGWANGALLA AMALIZA MGOGORO WA HIFADHI NA WANANCHI WILAYANI RUFIJI
https://i.ytimg.com/vi/Z3NPD1SDkJo/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/Z3NPD1SDkJo/default.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/dk-kigwangalla-amaliza-mgogoro-wa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/dk-kigwangalla-amaliza-mgogoro-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy