MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA MABALOZI WA SAUDI ARABIA, IRELAND NA MOROCCO KWA NYAKATI TOFAUTI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Balozi wa Ireland nchini...




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Balozi wa Ireland nchini Mhe. Paul Sherlock, Ikulu jijini Dar Es Salaam.
Balozi alizungumzia masuala mbalimbali yakiwemo kuwawezesha wanawake katika nafasi za kisiasa, Masuala ya Mimba za utotoni na namna ya kukabiliana na vifo wakati wa kujifungua.
Kwa upande wake Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliiomba nchi ya Ireland kuendelea kusaidia Tanzania katika kutoa elimu ya uzazi ili kupunguza Vifo vya akina mama na watoto wakati wa kujifungua.
Wakati huo huo Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amkutana na kuzungumza na Balozi wa Morocco nchini Mhe. Abdelilah Benryane mwenye makazi yake mjini Nairobi,Kenya.
Katika mazungumzo yao, Balozi wa Morocco alimpatia taarifa ya utekelezaji wa yote yaliokubaliwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco na kumueleza Makamu kwamba utekelezaji wa mambo hayo umefikia hatua nzuri.
Kwa upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais alimpongeza Balozi kwa kusimamia utekelezaji huo ndani ya muda mfupi.
Makamu wa Rais alimueleza Balozi huyo wa Morocco kuwa uhusiano uliopo kati ya nchi mbili hizi ni wa kudumu na utasaidia katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo katika nchi hizi.
Mwisho Kabisa Makamu wa Rais alikutana na kuzungumza na Balozi wa Sausi Arabia Mhe. Mohammed Almalik.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia Mhe.Mohammed Almalik(kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Saudi Arabia Mhe.Mohammed Almalik mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Ireland nchini Mhe. Paul Sherlock alimtembelea Makamu wa Rais ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam. 



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Morocco Mhe. Abdelilah Benryane (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam. 





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Morocco Mhe. Abdelilah Benryane (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo, Ikulu jijini Dar es Salaam. 












COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA MABALOZI WA SAUDI ARABIA, IRELAND NA MOROCCO KWA NYAKATI TOFAUTI DAR ES SALAAM
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA MABALOZI WA SAUDI ARABIA, IRELAND NA MOROCCO KWA NYAKATI TOFAUTI DAR ES SALAAM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjaWGceqQTFhOzrBjrxEV0Y9DEDr4o6hziNbDEQI8VvZgSaqVn4-3ZxonTgHDugg6FMB2lVhNyvFMin3zNOxKk1zGL7z20rwDElJSbu7A_GGbe17RJnppnmfZ0lrVgYnbADH0ICAa9llZM/s640/2+%25283%2529.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjaWGceqQTFhOzrBjrxEV0Y9DEDr4o6hziNbDEQI8VvZgSaqVn4-3ZxonTgHDugg6FMB2lVhNyvFMin3zNOxKk1zGL7z20rwDElJSbu7A_GGbe17RJnppnmfZ0lrVgYnbADH0ICAa9llZM/s72-c/2+%25283%2529.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/makamu-wa-rais-mhe-samia-akutana-na.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/makamu-wa-rais-mhe-samia-akutana-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy