MHANDISI METHEW MTIGUMWE AWASHUKURU WADAU WOTE WALIOSHIRIKI MAONESHO YA KILIMO NA SHEREHE ZA WAKULIMA –NANE NANE MWAKA 2017

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (Kilimo) Mhandisi Methew Mtigumwe   Na Mathias Canal, Dar es salaam Katibu Mkuu Wi...


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (Kilimo) Mhandisi Methew Mtigumwe
 
Na Mathias Canal, Dar es salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (Kilimo) Mhandisi Methew Mtigumwe anawashukuru wananchi, wadau wa kilimo na Taasisi mbalimbali kwa kushiriki Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima – Nane Nane mwaka 2017, ambapo maadhimisho kwa ngazi ya Ki-Taifa yalifanyika katika Uwanja wa Maonyesho ya Kilimo wa Ngongo, Manispaa ya Lindi.

Aidha, maadhimisho ya Ki-Kanda yalifanyika katika viwanja vya maonyesho ya John Mwakangale –Mbeya; Mwalimu J.K. Nyerere –Morogoro; Themi – Arusha; Nzuguni - Dodoma; na Nyahongolo – Mwanza.

Akizungumza na mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Mhandisi Mtigumwe amesema kuwa Maonesho ya mifugo sanjari na Maonesho ya Kilimo yametoa changamoto na kuleta mapinduzi katika Ufugaji, Uvuvi, na Kilimo na kutoa ajira hususani kwa vijana kwa kuwaongezea zaidi kipato na kuondoa umasikini. 

Mtigumwe alisema kuwa Wizara, taasisi/Makampuni ya umma na binafsi, Mabenki na wadau wote wa kilimo na mifugo wataendelea kuwasaidia wakulima na wafugaji hapa nchini ili kuongeza uzalishaji kuwezesha upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda vinavyokusudiwa kuanzishwa.

''Ni matumaini yangu  kuwa elimu ya matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wadau wengi kwa muda mfupi imetolewa ipasavyo lakini pia wadau walijionea na kujifunza huduma zitolewazo na serikali, mashirika ya umma na binafsi''

''Katika Maonesho hayo Teknolojia/Bidhaa mbalimbali zilionyeshwa ikiwa ni pamoja na zana za Kilimo, Mbegu bora za mazao mbalimbali, Uzalishaji wa mazao katika mazingira yaliyodhibitiwa ambapo pia Taasisi za kitafiti zilionyesha teknolojia mbalimbali za kuongeza tija zenye ukinzani dhidi ya magonjwa mbalimbali, Utengenezaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo, Uboreshaji wa viasilu ili kupata mifugo na mazao ya kilimo yanayostahimili hali ya hewa kutokana na maeneo walipo wananchi wanaohitaji kujihusisha na ufugaji na kilimo na udhibiti wa magonjwa'' Alisema Mtigumwe
   
Teknolojia na Bidhaa zingine zilizoonyeshwa ni pamoja na uzalishaji bora wa mazao ya nafaka, ubunifu wa teknolojia rahisi za kutotoa mayai, Kuongeza thamani mazao ya mifugo, Makampuni ya mawasiliano, ambapo Taasisi za elimu zilionyesha ubunifu wa kumsaidia mfugaji, Tiba za asili, Wasindikaji wakubwa na wadogo wa mazao ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Asali, na Nta.

Sikukuu ya wakulima inayofahamika kuwa Nanenane husherekewa nchini kote kuanzia 1 Agosti mpaka tarehe 8 Agosti kila mwaka. Sherehe hiyo inatayarishwa na kuratibiwa na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kuhusisha Taasisi, Wizara na mtu mmoja mmoja wanaoshughulika na kilimo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MHANDISI METHEW MTIGUMWE AWASHUKURU WADAU WOTE WALIOSHIRIKI MAONESHO YA KILIMO NA SHEREHE ZA WAKULIMA –NANE NANE MWAKA 2017
MHANDISI METHEW MTIGUMWE AWASHUKURU WADAU WOTE WALIOSHIRIKI MAONESHO YA KILIMO NA SHEREHE ZA WAKULIMA –NANE NANE MWAKA 2017
https://2.bp.blogspot.com/-_t2zvshN7b4/WYyvHNxxLjI/AAAAAAAAFXk/D0aBAu6blUMDxGvl66bscYRi64xjZ5AtACLcBGAs/s640/1.JPG
https://2.bp.blogspot.com/-_t2zvshN7b4/WYyvHNxxLjI/AAAAAAAAFXk/D0aBAu6blUMDxGvl66bscYRi64xjZ5AtACLcBGAs/s72-c/1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/mhandisi-methew-mtigumwe-awashukuru.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/mhandisi-methew-mtigumwe-awashukuru.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy