MAHAKAMA YAIMARISHA HAKI ZA WATOTO KWA VITENDO

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akikata utepe kuzindua Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) leo jijini Mbeya. Hii ni Maha...






Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akikata utepe kuzindua Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) leo jijini Mbeya. Hii ni Mahakama ya Pili ya Watoto nchini Tanzania baada ya ile iliyoko Kisutu Jijini Dar es salaam. Mahakama hii imejengwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF).

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) leo jijini Mbeya. Katikati ni Mwakilishi wa UNICEF nchini, Stephanie Shanler na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali (kushoto).

Mwakilishiwa UNICEF nchini, Stephanie Shanler akizungumza wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Mahakama hiyo.

……………………………………

Na Lydia Churi-Mahakama

Mahakama ni moja kati ya Mihimili mitatu ya dola wenye jukumu la msingi la kutoa haki sawa kwa wote na kwa wakati. Mhimili huu hufanya kazi ya kutafsiri Sheria mbalimbali zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwapatia wananchi haki. Kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano, Mahakama ya Tanzania imeendelea kusimamia haki za Watoto kama zilivyo haki nyingine wanazostahili kuzipata wananchi wa Tanzania.


Utekelezwaji wa haki za Watoto zilizoainishwa katika mikataba mbalimbali ya kikanda na Kimataifa na kupewa nguvu ya kisheria kupitia Sheria ya Mtoto namba 21yamwaka2009,kunahitajiushirikianobainayaTaasisina wadau wa haki za watoto. Katika kulinda haki za watoto wa Tanzania, hivi karibuni, Mahakama ya Tanzania ilizindua Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) katika jiji la Mbeya na kufanya idadi ya Mahakama hizo kufikia mbili hapa nchini. Mahakama nyingine ya Watoto iko Kisutu jijini Dar es Salaam.

Maendeleo Endelevu hupatikana kwakuzingatia misingi ya hakiza Watoto

Kwa kutambua umuhimu wa watoto kuwa ni uhai wa taifa lolote, Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) ilichukua hatua za makusudi kuhakikisha haki za kisheria za watoto zinalindwa kwa kujenga jengo la Mahakama ya Watoto jijini Mbeya. Jengo hili linakuwa ni la pili maalum kujengwa kwa shughuli za Mahakama ya watoto pekee kwa Tanzania bara. Akizindua jengo hilo hivi karibuni, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alisema endapo haki za Watoto zitadharauliwa kwa mapanayakesasa,basi azma ya maendeleo endelevu ya nchi hapo baadaye, itakuwa hatarini.


Akinukuu andiko la Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), kuwa“Maendeleo Endelevu yanaanza na kukamilika kwa misingi ya watoto kuwa salama, wawe ni wenye afya bora na waliopata elimu bora” (Sustainable Development starts and ends with safe, healthy and well-educated children- UNICEF, May 2013). Katika neno lake la utangulizi katika andiko hilo, Anthony Lake, Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF aliandika kuwa: Haki za watoto na afya yao njema, lazima ipewe kipaumbele katika maandalizi ya ajenda ya maendeleo endelevu ya baada ya mwaka2015. Uwekezaji kwa manufaa ya watoto ni njiaborayakufutaumaskini, kuongeza kasi ya kuchanua kwa manufaa kwa wote.” Alisema andiko hilo linatukumbusha kuwa ustawi wa Watanzania unaanza na Ustawi wa watoto.

Ustawi wa watanzania unaanza na ustawi wa watoto
Kaimu Jaji Mkuu aliendelea kusema kuwa maana ya ustawi wa watanzania unaanza na ustawi wa watoto ni kwamba tayari Katiba imetamka kuwa lengo kuu na jukumu la Serikali ni ustawi wa wananchi na ustawi huo wa wananchini lazimaujengewe misingi imara ya ustawi wa watoto wa leo.


Alisema jamii ya watanzania bado inayo mengi ya kufanya ili kuendeleza asilimia 50 ya wananchi wake ambao wana umri wa miaka 18 na chini ya miaka hiyo. Alisema, kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwezi Agosti mwaka 2012, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa na idadi ya watu milioni 44,928,923 na kati ya hao, watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0 hadi 17ni asilimia 50.1

Mikataba ya Haki za Watoto iliyoridhiwa na Tanzania

Kutungwa kwa Sheria ya Mtoto namba 21 ya mwaka 2009 nchini Tanzania kunatokana na mikataba mbalimbali ya kimataifa inayotambua na kulinda haki za Watoto ambayo Tanzania iliridhia. Baadhi ya Mikataba hiyo ni Mkataba wa Kimataifa wa Hakiza Mtoto (UNConvention on the Rights of the Child -UNCRC), Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto (African Charter on the Rights and Welfare of the Child-ACRWWC). Mikataba mingine ni ule wa United Nations Standard Minimum Rules for the Administration of Juvenile Justice (Beijing Rules) na United Nations Guidelines for the Prevention of JuvenileDelinquency (The Riyadh Guidelines).

Matokeo Ya Kutungwa Kwa Sheria Ya Mtoto ya mwaka 2009

Tanzania ilitunga Sheria ya Mtoto Namba 21 ya 2009 kwa ajiliya haki, ulinzi na ustawi wa mtoto. Aidha, Sheria hii imekusanya mapendekezo yoteya ndani yanchi, ya kikanda naya kimataifa kuhusu maboresho ya haki na maslahi mapana ya mtoto na kutoa nguvu yakisheria. Baada yakutungwakwaSheria hii, mihimili yadolaimepewa majukumu ya kutekeleza na kuwajibika. Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania anasema kwa upande wa mhimili wa Mahakama, inategemewa Mahakama ya Watoto isaidie kuwajibika na kutekeleza Sheria ya Mtoto.
Alisema kuna maeneo kadhaa katika Sheria ya Mtoto ambayo yanasimami wa na mamlaka nyingine. Pamoja na ukweli huo, bado Mahakama ya Watoto inaweza kutoa ushirikiano kwa mamlaka hizo au amri za mahakama zikasaidia utendaji wa mamlaka hizo, kwa mfano; mazingira mbalimbali ambayo yameainishwa na SheriaNamba 21 ya 2009 kuwa ni hatarishi kwa mtoto kama vile uyatima, kutelekezwa, kuteswa, kuzurura, kukinzanana sheria ambapo alisema Mahakama ya Watoto inaweza kutoa tafsiri nakupanua wigo wa “mazingira hatarishi”. Mahakama ya Watoto inaweza kutoa tafsiri na kupanua wigo wa Ulinzi na wajibu wa wazazi kwa matunzo ya mtoto, matibabu na elimu, sifa za mtu kuwa mlezi na uasili wa mtoto; namna gani Mahakama itawasilisha taarifa mbali mbali au kutumia rejista ya watoto walioasiliwa kwa Msajili wa Vizazi na Vifo pamoja na uzuiaji wa kazi za udhalilishaji kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka18.


Prof. Juma alisema Mahakama ya Watoto inaweza kutakiwa kutoa miongozo kuhusu mafunzo ya kazi (apprenticeship) kwa watoto chiniya miaka 18 na kuchunguza mikataba ya mafunzo ya kazi ambayo ni kandamizi au yasiyozingatia maslahi ya mtoto. Mahakama ya Watoto pia inaweza kutoa maamuzi ambayo yatazikumbusha Serikali za Mitaa wajibu wao wakuboresha ustawi wa watoto walio ndani ya mamlaka za Serikali ya Mtaa husika. Mahakama inaweza kuitahadharisha Serikali Kuu na Serikali za Mitaa na Halmashauri wajenge shule maalum za watoto za kutosha. Hii itasaidia Mahakama ya Watoto kuwa, badala ya adhabu ya vifungo gerezani, watoto waliopatikana na hatia watapelekwa. Kwa kuanzisha na kuendesha Shule, Mihimili mingine nayo itakuwa inaisaidia mahakama na magereza kutekeleza wajibu wao kwamujibu wa Sheria Namba 21 ya 2009.


Aidha Serikali za Mitaa na Serikali Kuu zitakapoanzisha vituo vya kutunzia na kulelea watoto wenye shida ya malezi na Bunge kutoa fedha za kutosha kuendesha vituo hivyo zitaisadia Mahakama kwa kiasi kikubwa, alisema Kaimu Jaji Mkuu na kuongeza kuwa Mahakama za watoto pia zinaweza kugundua mapungufu katika sheria na kupendekeza kuwa Waziri mwenye dhamana ya watoto atunge kanuni stahiki.

Sheria ya mtoto shirikishi na ina taka Ushirikiano.
Akizungumzia ushiriki na ushirikishwaji wa Sheria ya mtoto, Kaimu Jaji Mkuu alisema sheria kuwa sheria hii imesimamakatika misingi ya ushirikiano baina ya mihimili yote, ushirikianona wadau mbali mbali kama UNICEF na NGOs, taasisi ambazo zinashughulika na masuala ya haki za watoto. Alisema, Sheria hii pia inaitaka Mahakama ichukue uongozi na kunamasuala ambayo mihimili mingine imepewa nafasi ya uongozi hivyo Mahakama inayo nafasi nzuri ya kuipa uhai sheria hii kwa kuwa kwanza, haki zote stahili zilizoainishwa ndani ya Sheria hii zinamfaidisha mtoto, pili, Sheria hii inapotafsiriwa, pale ambapo wanaona kuna “kutofahamika, “utata” wawe na ujasiri wa kuielekeza sheria kufikia malengo mazuri yaliyowekwa na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa kuhusu haki ya watoto.


Mahakama pia inayo nafasi nzuri ya kuipa uhai Sheria hii kwa sababu Mahakimu katika Mahakama ya Watoto watakuwa na nafasi ya karibu kabisa kuona na mna vifungu mbali mbali vya Sheria hii vinavyofanya kazi, hivyo Kaimu Jaji Mkuu aliwaagiza Mahakama wanaosikiliza kesi za Watoto kuorodhesha mapungufu ya Sheria hii na kuhyawasilisha kwenye kamati ya Kanuni ya Jaji Mkuu kwa ajili ya kupendekezakwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu mabadiliko yaSheria.


Akisisitiza juu ya kulinda haki za Watoto, kaimu Jaji Mkuu aliwataka mahakamu wanaosikiliza kesi za Watoto wasome taarifa za Utekelezaji zinazowasilishwa na Tanzania na pia zile zinazowasilishwa na mataifa mengine kuhusu Tanzania ili waweze kugundua mapungufu yetu ya kiutekekezaji ili tuweze kupanga namna ya kuboresha utekekezaji. Mahakimu hao pia wametakiwa kufuatilia haki za Watoto pindi wanapofanya ukaguzi kwenye Magereza.

Ujenzi wa Jengo la Mahakama ya Watoto Mbeya
Jengo la Mahakama ya Watoto jijini Mbeya lililojengwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na UNICEF limegharimu kiasi cha shilingi za kitanzania

Milioni 415 ambapo Mahakama imechangia kiasi cha shilingi milioni 214 na UNICEF shilingi milioni 201. Jengo hili lilianza kutumika April 18, 2017 na linaofisi mbili za Hakimu, Ofisi ya Wakili wa Serikali, ofisi ya Afisa Ustawi wa Jamii na chumba cha Mawakili wa Kujitegemea.


Sababu za Mahakama kujengwa Mbeya Jengo hili ambalo ni la pili la Mahakama ya Watoto nchini limejengwa jijini Mbeya kwa kuzingatia upatikanaji wa wadau na huduma zote muhimu za haki kwa mtoto. Huduma hizo ni pamoja na uwepo wa shule ya maadilisho (approved school) ikiwa ni pekee nchini, kuwepo kwa Mahabusu ya watoto mkoani humo, na kuwepo kwa dawati la jinsia la watoto lenye viwango vinavyotambulika lililoanzishwa na Jeshi la polisi. Mahakama hii pia ilianzishwa kutukana na uwepo wa timu ya ulinzi na usalama wa mtoto (child protection team) na kuwepo kwa mfumo wa marekebisho ya tabia kwa watoto (community rehabilitation programme).

Ushirikiano wa Mahakama na UNICEF katika masuala ya haki ya Mtoto Katika kipindi cha takribani miaka mitano yaani tangu mwaka 2012, UNICEF na Mahakama walishirikiana katika kutengeneza kanuni za Mahakama yaWatoto ikiwa ni matakwa ya kifungu cha 99(1) cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 ambacho kinamtaka Jaji Mkuu kutengeneza kanuni za kutumika katika uendeshaji wa kesi katika Mahakama za Watoto.


UNICEF ilitoa msaada wa kitaaluma (technical support) na fedha katika kuandaa kanuni ambazo zilitangazwa katika Gazeti la Serikali No 182/2016. Uandaaji wa kanuni hizo ulihusisha wadau mbalimbali wa haki za watoto kama Majaji, Mahakimu, Mawakili wa Serikali, Maafisa Ustawi wa Jamii, na Mashirika yasiyo ya kiserikali vinayotoa msaada wa kisheria na vyombo vingine vinavyohusika na masuala ya mtoto.


Aidha, UNICEF imeshirikiana na Mahakama katika kuandaa mafunzo kwa wakufunzi (TOT) juu ya uendeshaji wa kesi za watoto kwa mujibu wa Sheria na kanuni za watoto.Wakufunzi walitoka Mahakamani, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Idara ya Ustawi wa Jamii.

UNICEF pia imeshirikiana na Mahakama kutoa mafunzo kwa Mahakimu, Mawakili, wa Serikali na Waendesha Mashtaka, Maafisa Ustawi wa Jamii, taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na Taasisi zisizo za Kiserikali katika Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani, Mbeya, na Iringa. Aidha mafunzo kwa wadau wote yanaendelea kufanyika katika wilaya mbalimbali kwa kutumia wakufunzi waliopata mafunzo yaliyotolewa na UNICEF na Mahakama.

Kwa sasa Mahakama na UNICEF watashirikana katika kutengeneza rejista za maalum mashauri ya watoto, kupitia mwongozo wa mafunzo (Training Manual) kwa kushirikiana na Chuo cha Mahakama Lushoto na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo (Law School of Tanzania).


Sambamba na hilo kwa mwaka huu wa fedha UNICEF wataendelea kushirkiana na Mahakama katika mpango endelevu wa kutoa mafunzo kwa wadau wote wa haki za Watoto. Pia UNICEF imeonyesha nia ya kushirikiana na Mahakama katika ukarabati mdogo wa Mahakama ili kuziweka katika mazingira rafiki kwa watoto.

Hata hivyo, bado iko haja ya kuongeza idadi ya Mahakama za watoto nchini kutokana na kuwepo kwa kesi za watoto na nyingine ambazo kwa namna moja au nyingine zinawahusisha watoto katika mikoa mbalimbali nchini ili kutekeleza azma ya kulinda na kutetea haki za Mtoto.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mahakama ya watoto jijini Mbeya, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali aliiomba UNICEF kuangalia uwezekano wa kujenga majengo mengine manne ya Mahakama za watoto katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma na Tabora ili kuwapatia Mahakimu fursa ya kujifunza kwa vitendo namna Mahakama za watoto zinavyofanya kazi.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAHAKAMA YAIMARISHA HAKI ZA WATOTO KWA VITENDO
MAHAKAMA YAIMARISHA HAKI ZA WATOTO KWA VITENDO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgHE7E2-y4eP2rgGj_cHalA7iZEZIGvWnTrQ7OPanBgIEcJyp9Haw0VAg9kuPWp1IcF8zunWjnZ5NjTusPUY2jIuFknF5dlJ2cU-3D2FLiZhOwE-YEGYsM1BeKCgCijcBkA2BARXjk_Uww/s640/DSC071131.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgHE7E2-y4eP2rgGj_cHalA7iZEZIGvWnTrQ7OPanBgIEcJyp9Haw0VAg9kuPWp1IcF8zunWjnZ5NjTusPUY2jIuFknF5dlJ2cU-3D2FLiZhOwE-YEGYsM1BeKCgCijcBkA2BARXjk_Uww/s72-c/DSC071131.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/mahakama-yaimarisha-haki-za-watoto-kwa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/mahakama-yaimarisha-haki-za-watoto-kwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy