TIMU YA EVERTON YARIDHISHWA NA UTOAJI HUDUMA YA AFYA KWA WAGONJWA WA MATENDE NA MABUSHA NCHINI

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Vida Mmbaga akisisitiza ju...Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Vida Mmbaga akisisitiza juu ya baadhi ya juhudi zilizofanywa na Serikali kupitia Mpango wa taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mbele ya viongozi kutoka timu ya Everton na mwakilishi kutoka Liverpool katika zoezi lililofanyika leo jijini Dar Es salaam.
Mratibu wa Mpango wa taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt Upendo Mwingira akibadilishana Mawazo na Mwakilishi kutoka Liverpool wakati wa tukio la kusaidia waliokuwa wagonjwa wa mabusha na matende liliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam. picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Mmoja ya Viongozi kutoka timu ya Everton iliyopo ligi kuu nchini Uingereza na aliekuwa mchezaji wa timu hiyo Leon Osman akigawa zawadi kwa waliokuwa wagonjwa wa Matende na Mabusha katika zoezi lakuwasaidia lililofanyika leo jijini Dar Es salaam.
Picha ya pamoja ya Viongozi kutoka timu ya Everton iliyopo ligi kuu nchini Uingereza, Viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na waliokuwa wagonjwa wa Matende na Mabusha katika zoezi lakuwasaidia lililofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

NA WAMJW-DAR ES SALAAM

UONGOZI wa timu ya mpira wa miguu ya Everton kutoka nchini Uingereza imeridhishwa na huduma inayotolewa kwa wagonjwa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwemo mabusha na matende hapa nchini.

Hayo yamezungumzwa na mmoja wa viongozi wa Everton Bw. Darren Griffiths ambao ni washiriki katika kuchangia huduma ya magonjwa hayo hapa nchini ambaye ameongozana na timu yake ili kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Gor Mahia kutoka chini Kenya.

“Tunayo furaha kuona wagonjwa wengi waliokuwa wanaumwa mabusha na metende nchini Tanzania kwa sasa wamepona kabisa na tunahaidi kuwa na Wizara ya afya bega kwa bega katika kutokomeza magonjwa haya” alisema Bw. Darren Griffiths

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kinga Wizara ya Afya Dkt. Vida Mmbaga amesema kuwa kutokana na ushiriki wa Everton katika kuchangia utoaji wa Huduma ya kutibu ugonjwa huo wamefanikiwa kupata ujuzi wa upasuaji hasa kwa wagonjwa wa mabusha na matende hapa nchini.

Aidha Dkt. Vida amesema kuwa Serikali ikishirikiana vyema na wananchi na mashirika mbalimbali ya afya magonjwa hayo yatatokomea kwa kiasi kikubwa hapa nchini mpaka kufikia mwaka 2025.

Mbali na Hayo Dkt. Vida amesema kuwa anawashukuru watu wa Everton kwa kupitia ushirikiano wao katika sekta ya afya kwa kutoa huduma pamoja na mafunzo kwa wataalamu ambapo imesaidia kuwafanyia upasuaji wagonjwa elfu moja.

Kwa upande wake Bw. Yahya Ally Kidege mkazi wa pugu stesheni amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwajali wananchi wake kwani amepata upasuaji wa ugonjwa wake wa busha na amepona kabisa kwan alikua na ugonjwa huo takribani miaka 20.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TIMU YA EVERTON YARIDHISHWA NA UTOAJI HUDUMA YA AFYA KWA WAGONJWA WA MATENDE NA MABUSHA NCHINI
TIMU YA EVERTON YARIDHISHWA NA UTOAJI HUDUMA YA AFYA KWA WAGONJWA WA MATENDE NA MABUSHA NCHINI
https://2.bp.blogspot.com/-6zKZR5Gy6Yw/WWeh4-TlwJI/AAAAAAADiyI/I-o1fRRV7QMq2zEKeqmG5DTflXcmshDfQCLcBGAs/s640/1.JPG
https://2.bp.blogspot.com/-6zKZR5Gy6Yw/WWeh4-TlwJI/AAAAAAADiyI/I-o1fRRV7QMq2zEKeqmG5DTflXcmshDfQCLcBGAs/s72-c/1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/timu-ya-everton-yaridhishwa-na-utoaji.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/timu-ya-everton-yaridhishwa-na-utoaji.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy