Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya leo amekabidhi Bendera ya Taifa kwa wan...
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya leo
amekabidhi Bendera ya Taifa kwa wanafunzi saba wanaosoma masomo ya
sayansi wanaokwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya First Global
Challenges nchini Marekani. Makabidhiano hayo yamefanyika katika shule
ya Sekondari ya wasichana Jangwani.
Katika
makabidhiano hayo Mhandisi Manyanya amewataka wanafunzi wote nchini
kusoma kwa bidii masomo ya sayansi, teknolojia na ubunifu ili
kuhakikisha ndoto ya Tanzania ya kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda
na biashara inafanikiwa na kwamba wizara tutaendelea na jukumu lake la
kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ili wanafunzi wote
waendelee kufanya vizuri katika masomo ya sayansi.
Shule
zilizotoa wanafunzi watakaoshiriki katika mashindano hayo ni pamoja na
Jangwani, Azania, Jamhuri, Benjamini Mkapa, Feza na Kisutu.
Naye
mratibu wa mashindano hayo kwa upande wa Tanzania ndugu Mkufu Shabani
Tindi alisema mashindano haya yameanzishwa na kufadhiliwa na shirika
lisilokuwa la kiserikali la Marekani liitwalo FIRST yenye maana ya for
inspiration and recognition of science and technology lenye lengo la
kuhamasisha ulimwenguni kote vijana wanaosoma masomo ya sayansi,
uhandisi, teknolojia na hesabu kuweza kutatua changamoto mbalimbali
ulimwenguni
Wanafunzi
watakaoshiriki wanatarajia kuondoka kesho Juni 12, 2017 na watakuwa
nchini Marekani kwa ajilia ya mashindano hayo makubwa kiulimwengu ambapo
zaidi ya nchi 170 zitashiriki.
Naye
mmoja wa washiriki Raymond Benedict kutoka Shule ya Sekondari Jamhuri
amesema yeye wenzake wamejiandaa vizuri katika kuhakikisha
wanaiwakilisha nchi katika mashindano hayo vizuri na kwa ufahari.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya
akikabidhi Bendera ya Taifa kwa wanafunzi watakaoshiriki katika
mashindano ya First Global Robotic Challenges nchini Marekani.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya pamoja
na baadhi ya wanafunzi watakaoshiriki katika mashindano ya First Global
Robotic Challenges wakiwaonyesha wanafunzi wa shule ya wasichana
Jangwani (Hawapo pichini) Roboti walioibuni.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi. Mhe. Mhandisi Stella Manyanya
akipata maelezo kutoka kwa mwanafunzi Raymond Benedict kutoka shule ya
sekondari Jamhuri ya namna roboti iliyobuniwa inavyofanya kazi.
COMMENTS