BALOZI WA ISRAEL NCHINI MHE. YAHEL VILAN AWAAGA WAFANYAKAZI WA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) BAADA YA KUMALIZA MUDA WAKE WA KUFANYA KAZI HAPA NCHINI

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimshukuru  Balozi wa Israel nchini mweny...


Picha no. 1
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimshukuru  Balozi wa Israel nchini mwenye  makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan (kulia) kutokana na nchi yake kuisaidia Taasisi hiyo kuwapatia mafunzo madaktari, wauguzi   na kutoa matibabu kwa  watoto. Katikati ni Daktari Bingwa wa Moyo kwa watoto na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo Sulende Kubhoja.
Picha no. 2
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na   Balozi wa Israel nchini mwenye  makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo kuwaaga wafanyakazi baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini. Israel imekuwa ikiisadia JKCI kwa kutoa mafunzo kwa madaktari, wauguzi  na matibabu kwa watoto.
Picha no. 3
Balozi wa Israel nchini mwenye  makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo kuwaaga wafanyakazi baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini. Israel imekuwa ikiisadia JKCI kwa kutoa mafunzo kwa madaktari, wauguzi  na matibabu kwa watoto.
Picha no. 4
Mwanamuziki kutoka nchini Israel Maestro Nir Brand akiwaimbia wimbo watoto wanaotibiwa katika   Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati balozi wa nchi hiyo Mhe. Yahel Vilan alipotembelea Taasisi hiyo kuwaaga wafanyakazi baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.
Picha no. 5
Balozi wa Israel nchini ambaye makazi yake yapo Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan (watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi  pamoja wa wafanyakazi wa Taasisi hiyo na wageni kutoka nchini Israel.
Picha no. 6
Daktari Bingwa wa Moyo kwa watoto na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo Sulende Kubhoja wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akizungumza na Daktari Bingwa wa mfumo wa chakula kwa watoto Cohen Shlomi kutoka nchini Israel wakati wa ziara ya balozi wa nchi hiyo alipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwaaga wafanyakazi.
Picha no. 7
Baadhi ya watoto wanaotiba  katika  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Balozi wa Israel nchini ambaye makazi yake yapo Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan alipokuwa akiwaaga wakati wa ziara yake aliyoifanya leo katika Taasisi hiyo. Serikali ya Israel kupitia Taasisi ya Save Child Heart (SACH) imegharamia matibabu ya watoto 40 tangu Novemba 2015 hadi sasa ambao walitibiwa nchini humo.
Picha no. 8
Balozi wa Israel nchini ambaye makazi yake yapo Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan akizungumza na wafanyakazi pamoja na watoto wanaotibiwa katika  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wakati wa ziara yake ya kuwaaga aliyoifanya leo baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini. Israel imekuwa ikiisadia Taasisi hiyo kutoa mafunzo kwa madaktari, wauguzi  na matibabu kwa watoto.(Picha na  JKCI)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BALOZI WA ISRAEL NCHINI MHE. YAHEL VILAN AWAAGA WAFANYAKAZI WA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) BAADA YA KUMALIZA MUDA WAKE WA KUFANYA KAZI HAPA NCHINI
BALOZI WA ISRAEL NCHINI MHE. YAHEL VILAN AWAAGA WAFANYAKAZI WA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) BAADA YA KUMALIZA MUDA WAKE WA KUFANYA KAZI HAPA NCHINI
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/07/Picha-no.-1-3.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/balozi-wa-israel-nchini-mhe-yahel-vilan.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/balozi-wa-israel-nchini-mhe-yahel-vilan.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy