MKURUGENZI WA SENSA YA WATU NA TAKWIMU ZA JAMII ATOA TAARIFA YA MFUMUKO WA BEI WA MWEZI MEI 2017

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WAPUNGUA HADI ASILIMIA 6.1 Na Benjamin Sawe Maelezo MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Mei, 2017 umepungua had...

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WAPUNGUA HADI ASILIMIA 6.1
Na Benjamin Sawe
Maelezo
MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Mei, 2017 umepungua hadi asilimia 6.1 kutoka asilimia 6.4 ilivyokuwa mwezi Aprili, 2017.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo amesema kupungua kwa mfumuko wa bei kunatokana na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwezi Aprili, 2017.
“Mfumuko wa Bei wa Taifa umepungua kutoka asilimia 6.4 kwa mwezi Aprili, 2017 hadi kufikia asilimia 6.1 kwa mwezi Mei , 2017 kutokana na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Mei, 2017,” amesema Kwesigabo.
Kwesigabo amesema Mfumuko wa Bei wa mwezi Mei, 2017 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.2 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.5 ilivyokuwa mwezi Aprili, 2017.
Amesema Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 109.26 kwa mwezi Mei, 2017 kutoka 109.04 mwezi Aprili, 2017 kutokana na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.
Kwesigabo ametaja bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi kuwa ni pamoja na mahindi yaliyoongezeka kwa asilimia 4.2, maharage mabichi kwa asilimia 2.9, maharage ya soya kwa asilimia 2.2, unga wa mtama kwa asilimia 1.5, viazi mviringo kwa asilimia 2.0, mihogo mikavu kwa asilimia 2.3, na magimbi kwa asilimia 2.5.
Aidha bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na mkaa ulioongezeka kwa asilimia 2.5.
Ameongeza kuwa Mfumuko wa Bei kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Mei, 2017 umepungua hadi asilimia 11.8 kutoka asilimia 12.0 mwezi Aprili, 2017. Aidha, badiliko la Fahirisi za Bei kwa bidhaa zisizo za vyakula umepungua hadi asilimia 3.0 mwezi Mei, 2017 kutoka asilimia 3.4 mwezi Aprili, 2017.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo  akiongea na wanahabari kuhusu Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Mei  2017 jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo  akiongea na wanahabari kuhusu Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Mei  2017 jijini Dar es Salaam leo.COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MKURUGENZI WA SENSA YA WATU NA TAKWIMU ZA JAMII ATOA TAARIFA YA MFUMUKO WA BEI WA MWEZI MEI 2017
MKURUGENZI WA SENSA YA WATU NA TAKWIMU ZA JAMII ATOA TAARIFA YA MFUMUKO WA BEI WA MWEZI MEI 2017
https://2.bp.blogspot.com/-7-FVMh2ovi4/WTv0Cs-8cZI/AAAAAAAA9Ns/d0FytTO6Ons9MZVtbaQgUERv47JS_xfbwCLcB/s640/NBS%2B3.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-7-FVMh2ovi4/WTv0Cs-8cZI/AAAAAAAA9Ns/d0FytTO6Ons9MZVtbaQgUERv47JS_xfbwCLcB/s72-c/NBS%2B3.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/mkurugenzi-wa-sensa-ya-watu-na-takwimu.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/mkurugenzi-wa-sensa-ya-watu-na-takwimu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy