MBUNGE WA VITI MAALUMU CATHERINE MAGIGE AWAKUMBUKA WATOTO YATIMA NA WALE WAONAOISHI KATIKA MAHABUSU YA WATOTO ARUSHA

 Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Catherine Magige akimkabidhi mkurugenzi na watoto wa kituo cha kul...





 Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Catherine Magige akimkabidhi mkurugenzi na watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Faraja  orphance kilichopo jijini hapa,kituo hichi cha watoto yatima kina jumla ya watoto 200 na kati ya watoto hao watoto 30 wanaishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi.


wa pili kushoto  mbunge wa  viti maalumu akiwa anateta jambo na katibu wa UWT mkoa wa Arusha Fatuma Hassan ,wakwanza kulia ni katibu wa kanda ya kaskazini msikiti wa  Twariqatul  ndugu Abdi Ramathani




 mbunge wa viti maalumu akiwa anamkabidhi zawadi za iddi mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha Samaritan villege Jospephat Mmnyi


 mbunge wa viti maalum akiwa pamoja na baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima na wasiojiweza cha Faraja ,mkurugenzi wa kituo hicho pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha.
 mbunge wa viti maalumu akiwa amembeba moja ya mtoto aliotelekezwa na mama yake akiwa mdogo anaeishi katika kituo cha watoto yatima cha Faraja kilichopo jijini hapa wakati alipowapelekea zawadi ya iddi


 mbunge wa viti maalumu akimkabidhi msaada wa chakula mmoja wa kijana wa kito cha Zawiani wakati alipotembelea kutoa zawadi za  sikukuu ya iddi
 mbunge wa viti maalumu Catherine Magige akiwa anapewa maelezo mafupi katika maabusu ya watoto Arusha ,Ambapo aliaambiwa mahabusu hiyo inauwezo wa kubeba watoto 50 wakike wakiwa 10 na wakiume wakiwa 40  lakini kwa sasa ina jumla ya mahabusu 12 tu na wote wakiwa ni wanaume (picha na Woinde Shizza,Arusha )
 Mbunge wa viti maalumu Catherine Magige akiwa anamkabidhi mbuzi ,mchele na mafuta kiongozi wa kituo cha mahabusu Arusha Mussa Mapunda ikiwa ni zawadi ya idi kwa watoto hao
 vijana wa kituo cha Zawiani wakisala kabla ya msaada kutolewa wakiwa na mbunge wa viti maalumu pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi


 Habari picha na  Woinde shizza,Arusha
 Mbunge wa Viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Catherine Magige leo amekabidhi  msaada wa mbuzi watano ,chakula  na mafuta kwa vituo vinne vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu pamoja watoto wanoishi katika mahabusu ya watoto mkoani hapa ili kusherekea sikukuu ya idi .

Akikabidhi msaada huo kwa katika vituo hivyo alisema kuwa watoto hao wanapaswa kusherehekea sikukuuu  ya iddi  kama wengine wanaoishi na wazazi wao majumbani kwao .

Alisema kuwa vitu vyote hivyo alivyovigawa katika vituo vyote alivyo vitoa ametoa kwa moyo wake  wote ,ambapo alisema kuwa yeye kama mama ameguswa na akaamua kwenda kuwapa watoto hawa msaada huo ili nao wakisherekea sikukuu hii wajisikie nao wapo na wazazi wao. 

"napenda kuwasihi wananchi wajijengee tabia ya kusaidia watoto hawa yatima pia wajifunze kutembelea hata hawa watoto mahabusu ata kama awana watoto katika mahabusu hizi lakini wanaweza wakatoka na misaada na kuamua kupelekea watoto hawa yatima au hawa watoto walioko mahabusu kwani ni watoto na wanahaki ya kupendwa kama watoto wengine"alisema Magige

Alivitaja vituo ambavyo vimepewa msaada kuwa ni pamoja na Faraja ophas,Samaritan villege,kituo cha watoto yatima  na wasio jiweza cha Zawiani pamoja na Mahabusu ya watoto  Arusha

 Wakati huohuo, Ofisa Msimamizi wa kito hicho , Mussa Mapua  aliiomba Serikali
kujenga uzio katika mahabusu hiyo ili kuzuia watu wenye nia mbaya
kuingiza dawa za kulevya au wale watoto ambao ni wakorofi kutoroka.

Aidha  alisema kuwa pia  wanahitaji wanasheria wa watoto hao ili kesi zao zilizoko
mahakamani ziishe kwa muda mfupi, tofauti na hali ilivyo sasa huku akisema kuwa mahabusu hiyo kwa sasa inawatoto wa kiume 12 wote wakiwa ni wanaume

"unajua  kesi zinachelewa kutokana na kukosekana kwa wanasherisa wa kuwatetea watoto  hivyo tunaomba serikali ijitaidi kutuletea mwanasheria wa kutetea watoto hawapia napenda kutumia nafasi hii kuliomba  Jeshi la Polisi kuwa makini katika upelelezi wa kesi
mbalimbali ikiwamo kuzingatia umri wa watoto ili kuepuka kuwapeleka
wakubwa katika mahabusi hiyo "alisema Mapua



COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MBUNGE WA VITI MAALUMU CATHERINE MAGIGE AWAKUMBUKA WATOTO YATIMA NA WALE WAONAOISHI KATIKA MAHABUSU YA WATOTO ARUSHA
MBUNGE WA VITI MAALUMU CATHERINE MAGIGE AWAKUMBUKA WATOTO YATIMA NA WALE WAONAOISHI KATIKA MAHABUSU YA WATOTO ARUSHA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjy-3282zXw1ASqRBVKIAigD4dioH0XB1iiH1edwDDMk2-fOb3ekg5dZrNOzJ4QnYJY4OCbUBxwSyqOFtGAn1bQz3PM1ja3zRVHYHyvUbNz3qdtq6KVxQqc_JR4ywV39tKy0z_2cGhupGRj/s640/DSC00299.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjy-3282zXw1ASqRBVKIAigD4dioH0XB1iiH1edwDDMk2-fOb3ekg5dZrNOzJ4QnYJY4OCbUBxwSyqOFtGAn1bQz3PM1ja3zRVHYHyvUbNz3qdtq6KVxQqc_JR4ywV39tKy0z_2cGhupGRj/s72-c/DSC00299.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/mbunge-wa-viti-maalumu-catherine-magige.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/mbunge-wa-viti-maalumu-catherine-magige.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy