Mgeni Rasmi Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (wanne toka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadh...
Mgeni
Rasmi Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis
Juma (wanne toka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji
na Mawakili wapya mara baada ya kuwaapisha mapema hii leo Juni 29, 2017 katika
viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kushoto waliokaa ni Rais wa Chama Cha Mawakili Tanzania,
(TLS), Tundu Lissu.(PICHA NA ELIPHACE MARWA –MAELEZO)
NA ELIPHACE MARWA – MAELEZO
KAIMU Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka
Mawakili wapya kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma ya uwakili na
kutumia taaluma zao kwa kutoa msaada wa kisheria kwa jamii.
Aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za 56 ya
kuwapokea na kuwaapisha Mawakili wapya 248 iliyofanyika katika viwanja vya
Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Aidha
Kaimu Jaji Mkuu amewahimiza Mawakili wapya kujiendeleza kitaaluma kwa sababu
kuwa wakili sio mwisho wa taaluma kwani wanahitajika kusoma sheria za nchi
mbalimbali Duniani ili kuweza kuingia mikataba ya kimataifa.
Alisema
mawakili wapya wanatakiwa washiriki katika kutoa haki, wawe waaminifu kwa mahakama
na wateja kwani wakienda kinyume haki itapotea.
“Mawakili wote wanatakiwa kuwa waaminifu kwa wateja wanaowahudumia
na kushirikiana na mahakama katika kutoa haki na wasiwe mawakala wa rushwa bali
wawe mawakala wa kutenda haki,” alisema Kaimu Jaji Mkuu Prof. Ibrahim.
Aidha
Kaimu Jaji Mkuu aliwataka mawakili hao kufika maeneo ya nje ya mji ili wasaidie
upatikanaji wa haki kwani kumekuwa na changamoto kubwa ya mawakili katika
maeneo ya nje ya miji.
Naye Rais wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) Tundu Lissu
amewataka Mawakili hao kutumia taaluma hiyo katika kuisaidia jamii kujua haki
zao na utawala wa sheria japo kuna changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia
ya sheria nchini.
“Napenda kuwatakia kila la kheri mawakili hawa wapya ila niwaombe
watumie taaluma hii kwa kuisaidia jamii kujua haki zao pamoja na utawala wa
sheria,” alisema Mh. Tundu Lissu.
Idadi ya mawakili walioapishwa leo imepelekea Tanzania kuwa na
idadi ya zaidi ya mawakili 6300.
Mgeni
Rasmi Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis
Juma (katikati) akifuatilia jambo wakati wa sherehe za 56 za kuwakubali
na kuwasajiri, Mawakili wapya 248 mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama
Kuu jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya ndugu wa Mawakili wapya wakisubiri zoezi la kuapishwa kwa ndugu zao mapema hii
leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
COMMENTS