Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya wi...
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Serengeti
inayojengwa makao makuu ya wilaya Mugumu.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiangalia mfano wa majengo ya hospitali ya wilaya ya Serengeti
inayojengwa makao makuu ya wilaya Mugumu kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa
Wilaya hiyo Dkt. Kisaka.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya
Mbuzi Mugumu Serengeti ikiwa sehemu ya kukamilisha ziara yake ambapo
alitumia fursa hiyo kuwashukuru wakazi wa Serengeti na kuwapongeza kwa
kutunza mazingira. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
ameuagiza uongozi wa wilaya ya Serengeti na wa mkoa Mara kukamilisha
haraka awamu ya kwanza ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo ili kuondoa
adha ya wananchi kusafiri kwenda mikoa ya jirani ya Arusha na Mwanza
kwenda kupata huduma afya.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo leo 6-June-2017 kwenye
mkutano wa hadhara mjini Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara mara
baada ya kutembelea ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya na kuweka jiwe
la msingi.
Makamu
wa Rais amesema kutokana na wilaya ya Serengeti kupata wegeni wengi
kutoka nje ya nchi ambao wanaenda kutembelea Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti hivyo ni muhimu kwa viongozi wa wilaya na mkoa kwa
ushirikiano na wadau wa maendeleo kukamilisha ujenzi huo haraka ili
wananchi waweze kupata huduma za afya za uhakika katika wilaya yao.
Makamu
wa Rais amesema kukamilika kwa ujenzi huo wa awamu ya kwanza kutaondoa
taabu kubwa wanayopata wananchi wa wilaya ya Serengeti katika kupata
huduma ya afya karibu na maeneo yao.
Katika
kuunga mkono jitihada hizo za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya
Serengeti, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameahidi kuchangia
kiasi cha shilingi milioni Tano na amewaahidi wananchi wa wilaya ya
Serengeti kuwa atakikisha fedha kutoka Serikalini ambazo zinatakiwa
kupelekwa wilayani humo zinapelekwa haraka ili kukamilisha ujenzi huo.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pia amewataka wananchi kote nchini
kuunga mkono jitihada za Serikali za kupambana na rushwa na ufisadi ili
kuhakikisha miradi inayotekelezwa inakuwa na manufaa kwa wananchi wote.
Amewaomba
wananchi nchini wasirudi nyuma katika mapambano dhidi ya rushwa bali
waendelee kubaini watu wanaofanya vitendo hivyo ili Serikali iweze
kuwachukulia hatua kali za kisheria .
Kuhusu
tatizo la mimba mkoani Mara, Makamu wa Rais ameonyesha kuchukizwa na
vitendo hivyo na kuomba vyombo vya dola na wananchi kwa ujumla
kushirikiana katika kukomesha mimba za utotoni mkoani Mara.
Kwa
upande wake, Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa amemhakikishia
Makamu wa Rais kuwa maelekezo yote anayoyatoa katika ziara yake
yatafanyiwa kazi ipasavyo ili kuondoa kero na changamoto zinazowakabili
wananchi.
Mkuu
huyo wa mkoa wa Mara ameomba wananchi wa Mkoa wa Mara kuwepa pembeni
tofauti zao za kisiasa bali washirikiane na Serikali katika utekelezaji
wa miradi yao ya maendeleo.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan bado anaendelea na ziara yake ya kikazi
mkoani Mara ambapo hapo kesho atafanya ziara katika wilaya za Butiama
na Musoma mkoani Mara
COMMENTS