MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA NGAZI ZA JUU WA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Kim...

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa  wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Rais wa zamani wa nchi ya Georgia Mhe. Mikheil Saakshvili akihutubia na kutoa uzoefu wa nchi yake dhidi ya mapambano dhidi ya rushwa wakati wa ufunguzi Mkutano wa Kimataifa  wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassanakiangalia kitabu kinachoelezea mapambano dhidi ya rushwa na Rais wa zamani wa nchi ya Georgia Mhe. Mikheil Saakshvili (kushoto) wakati Ufunguzi Mkutano wa Kimataifa  wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa , Rais huyo wa zamani alitoa uzoefu wake na wa nchi yake katika kupambana na rushwa.
Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa  wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa , Rais huyo wa zamani alitoa uzoefu wake na wa nchi yake katika kupambana na rushwa.
                                         ................................................................ 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa  Serikali haitarudi nyuma kamwe katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi nchini mpaka hapo vitendo hivyo vitakapokoma.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua Mkutano wa Kimataifa wa ngazi ya Juu wenye lengo la kubadilishana uzoefu katika mapambano dhidi ya Rushwa katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa vita ya kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi ni kipaumbele cha kwanza katika Serikali ya awamu ya Tano na wale wote wanaowezesha, kunufaika na kuhusika na vitendo hivyo wataendelea kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo nchini.
“Kupambana na rushwa ni jambo la msingi na muhimu kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo endelevu katika nchi yeyote Duniani,” Amesisitiza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya awamu Tano chini ya Uongozi Shupavu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli inaendelea kukaza kamba katika mapambano dhidi ya rushwa ambayo kwa muda mrefu sasa yamechangia kurudisha nyuma juhudi za Serikali za kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
Amesema Serikali ya Tanzania inalenga kufikia kipato cha kati na kuimarisha uchumi wa viwanda hadi ifikapo mwaka 2015 hivyo malengo hayo yatafanikiwa  haraka iwapo tu vitendo vya rushwa vitakomeshwa katika ngazi zote nchini.
Rushwa ni baya na imeharibu sana maisha ya watu na maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii hivyo ni lazima ikomeshwe  ili jamii iishi maisha mazuri“Ameeleza Makamu wa Rais.

Amesema kuwa hakuna nchi yeyote ambayo haijagushwa na misukosuko ya vitendo vya rushwa Duniani lakini Bara la Afrika limeendelea kuteseka sana na vitendo hivyo kwa miongo kadhaa sasa hivyo jitihada za pamoja zinatakiwa katika kutokomesha vitendo hivyo.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa wizara yake itaendelea kupambana na vitendo vya rushwa ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali kwa watumishi wa umma watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa kwenye maeneo yao ya kazi.

Naye, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia bi Bella Bird amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano za kupambana na vitendo vya rushwa na kusisitiza kuwa Benki hiyo ataendelea kutoa mchango wake wa hali na mali katika kuisaidia Tanzania katika uimarishaji wa mapambano hayo.
Mkutano huo wa Kimataifa wa ngazi ya Juu wenye lengo la kubadilishana uzoefu katika mapambano dhidi ya Rushwa unaofanyika nchini unahudhuriwa na viongozi mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchi wenye uelewa na uzoefu katika mapambano dhidi ya rushwa.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA NGAZI ZA JUU WA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA NGAZI ZA JUU WA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg6EqweYXIyG84AokKfSrlxgzA7F68k4N3_CTKqtJGUTrEIqPPm38i7mXhLTSfOdJpmzDM0SlEXdC6l8ggjOzUaun87KxR7bazVNqG74hqBZGItJzgMa3yLgj4Qk6JYaOtpvzzLgiRj34Q/s640/41.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg6EqweYXIyG84AokKfSrlxgzA7F68k4N3_CTKqtJGUTrEIqPPm38i7mXhLTSfOdJpmzDM0SlEXdC6l8ggjOzUaun87KxR7bazVNqG74hqBZGItJzgMa3yLgj4Qk6JYaOtpvzzLgiRj34Q/s72-c/41.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/makamu-wa-rais-mhe-samia-afungua.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/makamu-wa-rais-mhe-samia-afungua.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy