MAJALIWA ASHIRIKI SALA YA IJUMAA KWENYE MSIKITI WA AL - GADDAF

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Sheikh Nurdin Kishik ambaye ni Mhadhiri wa Kimataifa wa Dini ya Kiislamu (kulia) na uju...






Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Sheikh Nurdin Kishik ambaye ni Mhadhiri wa Kimataifa wa Dini ya Kiislamu (kulia) na ujumbe wake, ofisini kwake bungeni mjini Dodoma  Juni  2, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki katika sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa  Al- Gadaf mjini Dodoma Juni 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU: KILA MTANZANIA ASHIRIKI KUTUNZA AMANI 
           
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kuliombea Taifa ili liendelee kudumu katika hali ya amani na utulivu.

Amesema suala la kudumisha amani na utulivu ni jukumu la kila mmoja, hivyo kila mwananchi kwa imani yake ahakikishe anashiriki kutunza hali hiyo.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Juni 2, 2017) baada ya kumaliza kuswali sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Gadaf, mjini Dodoma.

Amesema ni vema kila mwananchi akajivunia hali ya amani na utulivu iliyoko nchini kwa kuwa ndiyo inayowezesha kufanyika kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo. “Tuendelee kudumisha amani, tufanye ibada kila mtu kwa imani yake. Serikali inaheshimu dini zote kwa sababu ndizo zinazojenga amani na mshikamano,” amesema.

Pia amewataka wazazi wahakikishe wanawalea watoto wao katika mazingira ya kidini ili wanapokuwa watu wazima waje kuwa raia wema. “Tuendelee kuhamasisha watoto wetu wasikilize mahubiri ya dini; ni jukumu letu sisi kama wazazi kuwahimiza wahudhurie mahubiri ya viongozi wa dini ili waweze kujijenga vyema kimaadili na kiimani pia.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewakumbusha Waislamu wahakikishe wanautumia vizuri mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kuzidisha ibada na kusaidia watu wenye mahitaji. “Leo ni Ijumaa ya kwanza katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, nawaomba tutumie vizuri mwezi huu ili tupate baraka,” amesema.

Ibada hiyo ya sala ya Ijumaa iliongozwa na Sheikh Nurdin Kishki ambaye ni Imamu wa Msikiti wa Vetenari, wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam.

Sheikh Kishki katika hotuba yake, aliwasisitiza Waislamu waendelee kufanya mambo mema yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu ikiwemo kuwatunza wazazi wao, kumswalia Mtume Mohammed (S.A.W) na kufunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
40480 - DODOMA.            
IJUMAA, JUNI 2, 2017.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAJALIWA ASHIRIKI SALA YA IJUMAA KWENYE MSIKITI WA AL - GADDAF
MAJALIWA ASHIRIKI SALA YA IJUMAA KWENYE MSIKITI WA AL - GADDAF
https://i.ytimg.com/vi/PsTDmIM_59o/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/PsTDmIM_59o/default.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/majaliwa-ashiriki-sala-ya-ijumaa-kwenye.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/majaliwa-ashiriki-sala-ya-ijumaa-kwenye.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy