MAAFISA WATENDAJI WA HALMASHAURI YA MUFINDI NI MAJIPU NITAWATUMBUA TUKIANZA KUAJIRI-MH FESTO MGINA

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi mhe Festo Mgina akizungumza na Mwandishi wa habari juu ya maafisa watendaji wa vij...Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi mhe Festo Mgina akizungumza na Mwandishi wa habari juu ya maafisa watendaji wa vijiji vyote vya halmashauri ambao si waadilifu katika kufanya kazi walizopewa.


Na Fredy Mgunda,Mufindi

Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa inakabiliwa kuwa na watendaji wa vijiji na kata ambao sio waanilifu kutokana na matumizi mabaya ya fedha za wananchi katika vijiji kitu kinachosababisha migogoro mingi huko vijijini.

Akizungumza na blog hii mwenyekitii wa halmashauri ya wilaya ya mufindi Festo Mgina alisema kuwa halmashuri inakabiliwa na watendaji wa vijiji ambao wanatumia vibaya pesa za wananchi na ndio sababu inayosababisha kutoitisha mikutano ya hadhara.

“Mimi kama mwenyekiti wahalmashauri hii ni muumini mkubwa wa utawa bora hasa kwa kuzingatia dhana ya uwazi na uwajibikaji kwasasababu nikizangatia dhana hii basi kila kitu kitaenda vizuri tatizo watendaji wangu hawataki kabisa dhana ya uwazi na uwajibikaji yaani watendaji wangu wa vijiji wengi wao ni mizigo tu kwangu” alisema Mgina

Mgina alisema kuwa wamekuwa wakiwawajibisha pamoja na kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji hao wa vijiji ili kuepuka migogoro kwa wananchi.

“Wananchi wanachanga pesa za maendeleo lakini unakuta mtendaji ametoka alikotoka na kuanza kuzitafuna pesa za wananchi hiyo sio haki jamani niseme ukweli maafisa watendaji wangu wa vijiji si waadilifu na nitatizo kubwa linalosababisha migogoro mingi huko vijijini”alisema Mgina

Aidha Mgina amekiri kuwa na ubungufu wa maafisa watendaji wa kata na vijiji na ndio sababu inayosababisha kukaimisha viongozi wengine wa serikali kushika nafasi za kuwa maafisa za watendaji.

“Saizi tunawatumia waajiliwa wa serikali hasa maafisa kilimo kuwa watendaji wa vijiji kutokana na kuwa uhabari wa wanayakazi wa kada hiyo na labda niseme ukweli nimepiga marufuku waalimu kukaimishwa nafasi hiyo kwa kuwa hata walimu wengi wamekuwa wakisababisha migogoro kutokana n wao kutokujua nini cha kufanya” alisema Mgina

Mgina alisema endapo Rais wa Jamhuri wa muungano Dr John Pombe Magufuli akitoa ruhusa za kuanza kuajili tutajili watendaji wengi na kuwafukuza watendaji wote ambao sio waandilifu kwa kuwa wanaitia doa halmashauri ya Mufindi.

“Waandishi wa habari mkoani Iringa mmekuwa mashaidi kwa kutoa habari mbaya za utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji wa vijiji na kata sasa njia sahihi ni kufukuza kazi tu maana tumekuwa tukiwaonya mara kwa mara lakini hawabadiliki bora kuwafukuza tu angalia radio Ebony fm,Nuru fm, magazeti,tv na blogs mbalimbali zinatoa habari mbaya za halmashauri ya Mufindi zinazosababishwa na maafisa watendaji” alisema Mgina

Lakini Mgina aliwashukuru shirika la LEAT kwa jitihada zao za kutoa elimu ya utawala bora kitu kilichowasaidia wananchi kuwa na uelewa mkubwa wa kuhoji kwa viongozi wao ambao si waadilifu ndio maana mara kwa mara tumeona viongozi wakifukuzwa katika nafsi zao za kiungozi.

Kwa upande wake afisa habari wa shirika la LEAT Edina Tibaijuka alimtaka Mwenyekiti huyo kuwasimamia vilivyo watendaji wa vijiji ili kuzitunza Maliasili walizonazo kwa kuwa wao ndio wanajukumu hilo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAAFISA WATENDAJI WA HALMASHAURI YA MUFINDI NI MAJIPU NITAWATUMBUA TUKIANZA KUAJIRI-MH FESTO MGINA
MAAFISA WATENDAJI WA HALMASHAURI YA MUFINDI NI MAJIPU NITAWATUMBUA TUKIANZA KUAJIRI-MH FESTO MGINA
https://1.bp.blogspot.com/-qilZoxkpDMU/WTfbHXxzI7I/AAAAAAAADWA/Gq2YCf2kXrsE2AtkublwDwE4sm8HDNbCwCLcB/s640/IMG_20170526_151712.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-qilZoxkpDMU/WTfbHXxzI7I/AAAAAAAADWA/Gq2YCf2kXrsE2AtkublwDwE4sm8HDNbCwCLcB/s72-c/IMG_20170526_151712.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/maafisa-watendaji-wa-halmashauri-ya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/maafisa-watendaji-wa-halmashauri-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy