IDARA YA HABARI (MAELEZO) YAPOKEA KAMUSI KUU KUENZI KISWAHILI

Na Lilian Lundo - MAELEZO Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi leo amekabidhi Kamusi Kuu ya Kiswahili kwa watumishi...

Na Lilian Lundo - MAELEZO
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi leo amekabidhi Kamusi Kuu ya Kiswahili kwa watumishi wa Idara ya Habari (MAELEZO) katika ofisi za Idara hiyo zilizopo Jijini, Dar es Salaam.
Dkt. Abbasi amesema mojawapo ya jukumu la idara hiyo ni kuhabarisha Umma, hivyo kamusi hiyo itakuwa msaada mkubwa katika uandishi wa habari za kila siku.
“Kamusi hii ina maneno mpaka yaliyoaanza kutumika hivi karibuni, kama vile bajaji. Pia ina misamiati mingi ambayo haitumiki, hivyo kwa kuitumia kamusi hii kutaongeza idadi ya misamiati ya Kiswahili kwa watumiaji wa lugha ya Kiswahili,” amesema Dkt. Abbasi.
Ameitaka Idara ya Habari kuitumia Kamusi hiyo kama nyenzo muhimu katika kutangaza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi pamoja na kutumia misamiati mipya.
Hata hivyo, Dkt. Abbasi alitoa ufafanuzi wa neno Mbashara kuwa ndio neno sahihi lenye maana ya inayorushwa hewani moja kwa moja au kuonwa kwa wakati huohuo kupitia redio na televisheni na sio Mubashara kama ambavyo limekuwa likitumika na vyombo vingi vya habari.
Aidha alitoa mfano wa misamiati mingine iliyopo katika kamusi hiyo kuwa ni neno sharubati linalomaanisha kinywaji laini ambacho hutengenezwa kwa maji ya matunda au sukari na kisha kutiwa rangi. Neno lingine ni mnyange ambalo linamaana ya mtu mwenye mwonekano mzuri, maridadi, mtanashati, mrembo, mlimbwende.
Dkt. Abbas amewataka watumishi wa idara hiyo kuwa chemchem ya kutumia misamiati iliyoko katika kamusi hiyo ili kukuza lugha ya Kiswahili.
Kamusi Kuu ya Kiswahili ilizinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Juni 19, mwaka huu, Bungeni Mjini Dodoma.
 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Kamusi Kuu ya Kiswahili toleo la pili kwa Maafisa Habari wa Idara hiyo leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi huyo amenunua Kamusi hizo ili kuwajengea uwezo maafisa hao kutumia maneno sahihi ya lugha ya Kiswahili kama njia ya kuhamasisha matumizi sahihi ya lugha hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Sehemu ya Huduma za Habari na Picha, Rodney Thadeus.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya hiyo Sehemu ya Huduma za Habari na Picha, Rodney Thadeus wakionyesha nakala za Kamusi Kuu ya Kiswahili toleo la pili kwa Maafisa Habari wa Idara hiyo (hawapo pichani) mara baada ya makabidhiano ya Kamusi hizoyaliyofanyika katika Ofisi za Idara hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kamusi hizo zimekabidhiwa na Dkt. Abbasi kwa lengo la kuwajengea uwezo Maafisa hao katika matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya hiyo, Sehemu ya Huduma za Habari na Picha, Rodney Thadeus (kulia) wakisoma nakala za Kamusi Kuu ya Kiswahili toleo la pili mara baada ya makabidhiano ya Kamusi hizo yaliyofanyika katika Ofisi za Idara hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kamusi hizo zimekabidhiwa na Dkt. Abbasi kwa lengo la kuwajengea uwezo Maafisa hao katika matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Sehemu ya Huduma za Habari na Picha, Rodney Thadeus akiwasisitizia Maafisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) kutumia Kamusi Kuu ya Kiswahili toleo la pili alizokabidhiwa na Mkurugenzi wa Idara ya hiyo Dkt. Hassan Abbasi leo Jijini Dar es Salaam ikiwa ni njia ya kuhamasisha matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili. (Picha zote na Frank Shija - MAELEZO)




 

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: IDARA YA HABARI (MAELEZO) YAPOKEA KAMUSI KUU KUENZI KISWAHILI
IDARA YA HABARI (MAELEZO) YAPOKEA KAMUSI KUU KUENZI KISWAHILI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj3xZ9poH0kjUhZ1fijYPLclW6kI7Vq4OqNeA55-F-rPRycXLkA-IWSJT_CaOA4_602Cbznysny0wZVcAehGUZiAhQj6F0TRGVFo2pO86ApPWyzkcQgVRzFRAa9Zfgey9ntBcMQlgZ59x0/s640/PIX0.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj3xZ9poH0kjUhZ1fijYPLclW6kI7Vq4OqNeA55-F-rPRycXLkA-IWSJT_CaOA4_602Cbznysny0wZVcAehGUZiAhQj6F0TRGVFo2pO86ApPWyzkcQgVRzFRAa9Zfgey9ntBcMQlgZ59x0/s72-c/PIX0.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/idara-ya-habari-maelezo-yapokea-kamusi.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/idara-ya-habari-maelezo-yapokea-kamusi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy