F HIVI NDIVYO COCO BEACH ILIVYOFURIKA JIONI YA JANA JIJINI DAR | RobertOkanda

Wednesday, June 28, 2017

HIVI NDIVYO COCO BEACH ILIVYOFURIKA JIONI YA JANA JIJINI DAR


Hivi ndivyo Ufukwe wa Coco (Coco Beach) ulivyofurika watu wa aina mbalimbali hapo jana jioni, katika kusherehekea sikukuu ya Iddi pili,Mabasi/Daladala kutoka kona kadhaa za jiji la Dar zilionekana zikishusha watu kwa wingi katika ufukwe huo ambao ulisheheni pia vyakula vya kila aina ikiwemo Mihogo, Chips mayai na wengine walikutwa na Camera ya Blogu ya jamii wakiwa wemebeba vyakula vyao na kujibweda kando kando ya ufukwe,ama kwa hakika ilikuwa burudani kwa wakazi wa jiji la Dar. (Picha na Michuzi Jr)Kuhakikisha ulinzi na usalama wa kutosha unakuwepo,Jeshi la Polsi lilipiga kambi kabisa eneo hilo,kwa idadi ya watu ilikuwa ni kubwa.
Sehemu za kupaki magari zikaonekana hazitoshi kabisa
Foleni ya kuingia kando kando ya ufukwe nayo ilikuwa kubwa kiasi ambacho magari mengine yalipita kwa taabu kuendelea na safari zake.

Chopa ya Jeshi la polisi nayo ilikuwa na kazi ya ziada kama hivi ya kukagua meneo mbalimbali yaliyokuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu,Pichani chini Chopa ikionekana kwa mbali ilipokuwa ikikatiza maeneo hayo

0 comments:

Post a Comment