Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akipiga ngoma kwa furaha kama ishara ya kuzindua kikundi cha Brigh...
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.
Rehema Nchimbi (katikati) akipiga ngoma kwa furaha kama ishara ya
kuzindua kikundi cha Bright Focus kilichopo chuo cha Uhasibu Singida,
kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe. Elias Tarimo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.
Rehema Nchimbi akihutubia wanakikundi cha Bright Focus (hawapo pichani).
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.
Rehema Nchimbi, (katikati) akipiga ngoma kwa furaha kama ishara ya
kuzindua kikundi cha Bright Focus kilichopo chuo cha Uhasibu Singida,
kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe.Elias Tarimo.
Wanachuo ambao ni wanakikundi cha
Bright Focus kilichopo Chuo cha Uhasibu Singida wakimsikiliza Mkuu wa
Mkoa wa Singida wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho.
Makamu wa rais wa Bright Focus ,
John Gama akiwasilisha malengo ya kikundi hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa
Singida wakati wa uzinduzi katika chuo cha Uhasibu Singida.
………………………….
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.
Rehema Nchimbi ametoa rai kwa vyuo vikuu na vyuo vinavyotoa elimu ya juu
kuwa sehemu ya kuwafundisha na kuwatengeneza wasomi wenye kutambua
fursa na tija za maisha na sio sehemu ya kuendekeza migomo isiyo na
faida katika maisha ya wanachuo hao.
Dkt. Nchimbi ametoa rai hiyo jana
wakati akizindua kikundi cha Bright Focus kilichopo chuo cha Uhasibu
tawi la Singida chenye wana kikundi 89 ambao ni wanachuo, walimu na
walezi wenye malengo ya kutambua fursa za kuboresha maisha.
Amesema wakati akizindua kikundi
hicho anatambua kuwa kikundi hicho kitasaidia kubuni mawazo yenye tija,
fursa, na mwelekeo wa kuboresha uchumi huku akiwasisitiza kuelekezana
namna bora ya matumizi ya rasilimali walizonazo hususani rasilimali
fedha.
Dkt Nchimbi amekitaka kikundi
hicho kuwa chachu ya mabadiliko ya tabia na mienendo yote mibaya iwe
mizuri kutokana na baadhi ya wanachuo katika vyuo mbalimbali kuhusishwa
na tabia zisizo njema.
Amesema kila mwanakikundi anapaswa
anatakiwa mawazo yake yaendane na malengo ya kikundi cha Bright Focus
kuanzia mwenendo wa maisha yake, ufaulu wake na hata matumizi ya
rasilimali yawe yenye muono wa kutengeneza faida na hasa kujifunza namna
ya kuhifadhi akiba.
Aidha Dkt Nchimbi amekubali ombi
ya wana kikundi hao la kuwa mlezi wao huku akiwaasa kutoegemea kwenye
changamoto bali wazitazame fursa zilizopo huku akiwapongeza kwa
kuanzisha kikundi hicho.
Akiwasilisha malengo ya kikundi
hicho Makamu wa rais wa Bright Focus John Gama amesema kikundi kina
malengo mengi ikiwemo kutoa udhamini kwa wanachuo ambao watashindwa
kulipa ada kutokana na sababu mbalimbali.
Gama ameongeza kuwa kikundi
kitaanzisha miradi ya maendeleo kama vile kilimo, biashara ya bajaji na
pikipiki, ufugaji wa nyuki na kuanzisha makapuni mbalimbali ziku za
baadaye ili wana kikundi waweze kujiongezea kipato.
Amesema kikundi kina lengo la
kutatua changamoto ya ukosefu wa uzoefu hasa linapokuja suala la ajira
kwa kuwaajiri wana chuo katika makampuni watakayoanzisha ili waweze
kupata ujuzi huo pamoja na kuandaa ziara za mafunzo.
Katika uzinduzi wa kikundi cha
Bright Focus kulikuwa na mdahalo wa nani ana umuhimu zaidi kati ya
mwanamke na mwanaume ambapo wana kikundi walichangia hoja, kila upande
wa mwanamke na mwanaume ukijitahidi kuthibitisha yale wanayoamini.
Dkt Nchimbi alihitimisha mdahalo
huo kwa kusisitiza kuwa thamani ya mwanamke na mwanaume iko sawa kwakuwa
katika jamii hakuna maendeleo yanayoletwa na mwanaume peke yake au
mwanamke peke yakena hivyo kuwataka wazitambue thamani walizonazo na
kuzienzi.
COMMENTS