WANASIASA MSITUMIE MSIBA WA WANAFUNZI 32 WA LUCKY VICENT KAMA NJIA YA KUJINUFAISHA

Mwakilishi wa chama cha wamiliki wauza mafuta rejareja  Kanda ya kaskazini  Deipyen Bameda  (TASDOA ) katikati ni Katibu mkuu  TASDOA T...



Mwakilishi wa chama cha wamiliki wauza mafuta rejareja  Kanda ya kaskazini  Deipyen Bameda  (TASDOA ) katikati ni Katibu mkuu  TASDOA Tinno Mmasi akiwa anafafanua jambo mara baada ya
kumkabidhi mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo Rambirambi zao za vifo vya wanafunzi 32 wa Lucky Vicent
 Dar es Salaam Independent School (DIS) Anna Msangi akiwa anakabidhi kiasi cha shilingi milioni tatu kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ikiwa ni mchango wao kwa wanafunzi wa Lucky Vicent.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akifafanua jambo ofisini kwake kabla ajapokea rambirambi hizo

(Picha na  Woinde Shizza, Arusha)



Baadhi ya wanasiasa  wametakiwa kuacha  mara moja kuchulia tukio la vifo vya wanafunzi 32 wa Lucky Vicent kama sehemu yao ya
kujinufaisha  kisiasa, pamoja na baadhi yao kupotosha jamii kupitia  mitandao ya kijamii .




Hayo yamebainishwa jana  na mkuu wa mkoa wa Arusha  Mrisho Gambo wakati alipokuwa akipokea rambirambi za wanafunzi  32 wa Lucky Vicent,zilizotolewa na chama  cha wamiliki  wauza mafuta rejareja (TASDOA) pamoja  na uongozi wa shule binafsi ya Dar es Salaam
Independent School (DIS) ambapo alisema kuwa anasikitishwa sana na baadhi ya
viongozi kuchukulia swala hili kama ni sehemu ya kujijengea umaarufu.



Alisema kuwa swala hili sio tukio la kisiasa bali ni mtihani na changamoto kubwa iliyozikumba familia za wananchi wa Arusha ,hivyo
linatakiwa kuheshimika na kuchukuliwa kama ni tatizo kubwa lililowakumba
wananchi wa mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kwani kuwapoteza watoto hawa
ni jambo  la kusikitisha sana kwani walikuwa
wanategemewa kuwa viongozi wa baadae.





“Pia napenda kuchukuwa fursa hii kuwashukuru kwa kuleta
michango yenu kwa ajili ya wanafunzi hawa 32 ila napenda pia kuwakumbusha
kuwa  jumla ya watu wote waliopata tatizo
walikuwa 38 lakini kati yao waliokufa ni 35 na
na wingine watatu ni majeruhi hivyo napenda kuwasihi wananchi na
mashirika ambayo wanaleta msaada wasiangalie waliopoteza maisha tu bali
wawakumbuke na wale majeruhi watatu ambao wapo nje kwa matibabu kwani wao pia
ni binadamu”alisema Gambo





Alisema kuwa japo kuwa majeruhi wale waliopelekwa nje kutibiwa wanaudumiwa bure lakini kuna wale watu ambao wameenda nao pamoja ya kuwa wanahudumiwa chakula na malazi lakini kwa binadamu waka waida anatakiwa kujitegemea kwa vitu vidogovidogo hivyo ni vizuri kama watu wanaotoa msaada
wata wakumbuka na hawa majeruhi .





Kwa upande wake katibu mku u wa  chama cha wamiliki wauza mafuta rejareja (TASDOA) Tino Mmasi alisema kuwa wao kama wamiliki wawauza mafuta wadogowadogo wameguswa sana na msiba huu na ndio maana walioamua kukaa kama wanachama na kuchanga fedha hizi kiasi cha shilingi millioni saba laki saba
ili ziwafariji wafiwa hawa 35 na pia wameaidi
kwend a kujichanga tena  kwa ajili ya
kuwachangia majeruhi ambao wapo Marekani





“Tumetoa hiki kidogo lakini kwa jinsi  tulivyoguswa tutaenda kuchanga fedha
zingine kwa ajili ya majeruhi waliopo marekani na tunapenda kukuaidi mkuu wa mkoa
tutakuwa nanyi bega kwa bega hadi majeruhi hawa wote wapone na warudi hapa
nchini”alisema  Mmasi





Katika michango hii shule ya  shule binafsi ya Dare salaam Independent School (DIS) ilichanga kiasi
cha shilingi  milioni tatu  laki moja na nusu  huku
chama cha wamiliki wa uzamafuta rejareja
wakiwa wamechangia shilingi milioni saba laki saba  huku wote wakiaidi kwenda kukusanya fedha
nyingine kwa ajili ya majeruhi.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WANASIASA MSITUMIE MSIBA WA WANAFUNZI 32 WA LUCKY VICENT KAMA NJIA YA KUJINUFAISHA
WANASIASA MSITUMIE MSIBA WA WANAFUNZI 32 WA LUCKY VICENT KAMA NJIA YA KUJINUFAISHA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi-GE_9FdUDqME9d_C3OHX3r7HW_N4VaH3Ki81CF2bCXn8OKB1KJgjOG_vD4Afw4gvaD601iJktnS6nmsenVAD93bNRfsCAhLuBH1kidppEb86a-r8yBFEYQ7PxNuOaHkEpIfBZYmfkzuN8/s640/DSC00067.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi-GE_9FdUDqME9d_C3OHX3r7HW_N4VaH3Ki81CF2bCXn8OKB1KJgjOG_vD4Afw4gvaD601iJktnS6nmsenVAD93bNRfsCAhLuBH1kidppEb86a-r8yBFEYQ7PxNuOaHkEpIfBZYmfkzuN8/s72-c/DSC00067.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/wanasiasa-msitumie-msiba-wa-wanafunzi.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/wanasiasa-msitumie-msiba-wa-wanafunzi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy