SERIKALI YAWEKA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA MAZIWA NCHINI

Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA. Serikali kupitia Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi imeweka mikakati mbalimbali ili kukabiliana...


Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi imeweka mikakati mbalimbali ili kukabiliana na upungufu wa maziwa nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba wakati akijibu swali la Mbunge wa Wete Mbarouk Salum Ali leo Bungeni Mjini Dodoma katika Kikao cha thelathini na sita cha bunge la 11.

“Nakubaliana na Mhe.Mbunge kuwa Tanzania ina idadi kubwa ya mifugo lakini bado kuna upungufu wa maziwa,ambapo takwimu za makadirio za mwaka 2016 zinaonyesha lita bilioni 2.09 za maziwa zilizalishwa na unywaji wa maziwa kwa mtu kwa mwaka ulifikia lita 47 ukilinganisha na lita 200 zinazopendekezwa na Shirika la chakula Duniani (FAO)”,Alisema Mhe.Tizeba

Aidha kati ya Ngombe milioni 28.4, Ngombe rasmi wa maziwa ni 782,995 tu sawa na asilimia 3 ya Ng’ombe wote.Aidha kati ya mbuzi milioni 16.7 ni mbuzi rasmi takribani 50,000 ndio wa maziwa ambao ni asilimia 0.3 ya mbuzi wote.

Amezitaja jitihada ambazo Serikali imechukua ili kukabiliana na upungufu wa maziwa nchini ni pamoja na kumarisha mashamba ya kuzalisha mifugo ya Serikali (LMU’s) ili kuongeza idadi ya Ng’ombe wenye uwezo wa kuzalisha maziwa kwa wingi.

Aidha Serikali imeanzisha vituo vya uhimilishaji katika kanda 6 hapa nchini ambazo ni kanda ya Ziwa (Mwanza), Kanda ya Magharibi (Katavi), Kanda ya kati (Dodoma), Kanda ya Mashariki (Kibaha), Kanda ya Kusini (Lindi) na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya) kwa lengo la kutoa huduma ya uhilimishaji wa Ng’ombe wa Maziwa walioko kwenye maeneo hayo pamoja na Ng’ombe wa Asili ili kuzalisha idadi kubwa ya Ng’ombe wa Maziwa.

Amehimiza kuwa Jitihada hizi zitawezesha idadi ya Ng’ombe wa Maziwa kufikia milioni 2.9 ifikapo mwaka 2021/22 ambao pamoja na ng’ombe wa asili wataweza kuzalisha lita bilioni 3.8 za maziwa.

“Serikali inaendelea kuhamasisha sekta binafsi na wadau wengine wa maendeleo kuwekeza katika uzalishaji wa mitamba ya maziwa na mashamba ya ng’ombe wa maziwa kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa maziwa hapa nchini”, Aliongeza Tizeba

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SERIKALI YAWEKA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA MAZIWA NCHINI
SERIKALI YAWEKA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA MAZIWA NCHINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgcSJBmQbExyBuldCCCL5AUoa3X2qC9gqYi0iLVEoWogc9MwdH80Cg1hmCIHr3EYjan5CRG6aU3A5qWmvBX18pICMfyajWhjVkc2wxHZsdlDXsmWKAKlFueOWpsVqDHMtCN7oDtm92W5mE/s320/unnamed+%25281%2529.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgcSJBmQbExyBuldCCCL5AUoa3X2qC9gqYi0iLVEoWogc9MwdH80Cg1hmCIHr3EYjan5CRG6aU3A5qWmvBX18pICMfyajWhjVkc2wxHZsdlDXsmWKAKlFueOWpsVqDHMtCN7oDtm92W5mE/s72-c/unnamed+%25281%2529.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/serikali-yaweka-mikakati-ya-kukabiliana.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/serikali-yaweka-mikakati-ya-kukabiliana.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy