“MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA HOIMA NCHINI UGANDA HADI BANDARI YA TANGA WAIVA”

  Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale kulia akimueleza jambo Waziri wa Viwanda, Biashar...





 Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale kulia akimueleza jambo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage (kushoto) wakati alipofungua maonyesho ya tano ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.

 Mwanasheria Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini Tanzania (TPDC), Kelvin Gadi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao ambalo lipo eneo la mwahako jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya
biashara kimataifa.


 Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale akizungumza na waandishi wa habari.





MRADI wa Bomba la Mafuta Mkoani Tanga umefikia kwenye hatua ya wataalamu kukagua njia itakayopitisha miundombinu ya bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi
Bandari ya Tanga.


Hatua hiyo imekuja baada ya serikali ya Tanzania na Uganda kutiliana saini ya mkataba baina ya nchi na nchi (Iga) kukamilika.





Hayo yalisemwa na Mwanasheria Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini Tanzania
(TPDC), Kelvin Gadi jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao ambalo lipo eneo la mwahako jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya biashara kimataifa.


Alisema tayari wameshafanya maamuzi yameshakamilika wataalamu wanafanya tathimi ya udongo
katika njia ambayo bomba hilo litapita kwa taarifa ya awali njia iliyopatikana upana mita 200 na baadae watalaamu wataipunguza mpaka 100.


Awali akizungumza kuhusiana na mradi huo, Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Augustino Kasale alisema mradi huo utapita katika mikoa nane ya Tanzania na kuzalisha ajira 10000 za
kudumu na muda mfupi.


Alizitaja fursa ambazo zitakuwa moja kwa moja ni hutoaji huduma wakati wa ujenzi, ajira za muda mfupi na moja kwa moja, fursa za usafirishaji ikiwemo kuufungua mkoa wa Tanga kiuchumi.


“Hivyo hivi sasa wananchi wa mkoa wa Tanga wanapaswa kujiandaa na ujio wa Bomba la Mafura ghafi kutoka hoima
nchini Uganda hadi Mkoani Tanga “Alisema.


(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: “MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA HOIMA NCHINI UGANDA HADI BANDARI YA TANGA WAIVA”
“MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA HOIMA NCHINI UGANDA HADI BANDARI YA TANGA WAIVA”
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiCAF7rQnx4Z_QetTe2J6hDqaohnra6R3jT5WtwsCypM0prepFpO53gl9oB2rWbWRYKCaO8r_q7hUrfJVBmAsowAqEsVaxIhGLckyB_yH1GaVdoRfKli9MOJ3Z0e7JnIge1FwfAHjF-TA42/s640/IMG_3144.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiCAF7rQnx4Z_QetTe2J6hDqaohnra6R3jT5WtwsCypM0prepFpO53gl9oB2rWbWRYKCaO8r_q7hUrfJVBmAsowAqEsVaxIhGLckyB_yH1GaVdoRfKli9MOJ3Z0e7JnIge1FwfAHjF-TA42/s72-c/IMG_3144.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/mradi-wa-bomba-la-mafuta-kutoka-hoima.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/mradi-wa-bomba-la-mafuta-kutoka-hoima.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy