Mkurugenzi wa TIC Geoffrey Mwambe (kushoto) akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi katika...
Mkurugenzi
wa TIC Geoffrey Mwambe (kushoto) akipokea zawadi ya saa
kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi katika kikao cha kumuaga, Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias
Tarimo na Mkuu wa Wilaya Mkalama Jackson Masaka.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini Geoffrey Mwambe akiwashukuru
viongozi wa Mkoa wa Singida kwa ushirikiano katika kikao kifupi cha
kumuaga.
Mkurugenzi
wa TIC Geoffrey Mwambe (kushoto) akipokea zawadi ya saa
kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wa kwanza Kulia)
katika kikao cha kumuaga. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias
Tarimo na Mkuu wa Wilaya Mkalama Jackson Masaka.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi na Mkuu wa Wilaya ya
Singida Elias Tarimo wakifungua zawadi ya saa ambayo ina picha ya mazao
ya alizeti na vitunguu ambavyo huzalishwa kwa wingi na ubora Mkoani
Singida.
Mkuu
wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akimpongeza Mkurugenzi Mpya wa TIC
kwa uteuzi, Geoffrey Mwambe ambaye alikua Mkuu wa Wilaya ya Manyoni,
kulia kwake ni mkurugenzi Mwambe na kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya
Mkalama Injinia Jackson Masaka.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) Geoffrey Idelphonce Mwambe
ametoa tahadhari kwa wawekezaji wote wa nje na ndani ambao hawana nia
njema na maendeleo ya taifa kuwa hawana nafasi nchini na kwamba
hawatapata fursa yoyote Tanzania.
Mwambe
ametoa tahadhari hiyo jana jioni katika kikao kifupi kilichoandaliwa na
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kwa ajili ya kumuaga rasmi
Mkurugenzi huyo mara baada ya uteuzi wake ambapo hapo awali alikuwa
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni.
Amesema
kituo cha uwekezaji kitashirikiana na wawekezaji wenye nia njema tu ila
wale ambao wanataka kujinuafiasha wao na kuliacha taifa bila faida
yoyote hawatapewa fursa yoyote ya kuwekeza nchini.
Mwambe
ameongeza kuwa atahakikisha kuwa wawekezaji wenye ubora na ambao
uwekezaji wao unamgusa mtanzania moja kwa moja wanapatikana hasa wale
ambao watasaidia kutoa ajira kwa wananchi na kukuza uchumi.
“Nina
imani na wawekezaji wadogo ambao nitajitahidi kuwaunganisha na
wawekezaji wakubwa ili wakue na wajenge uchumi wa taifa itawasaidia pia
hao wawekezaji wadogo watapata uzoefu na hivyo kuwa wawekezaji wakubwa”,
amesema.
Mwambe
ameongeza kuwa hatausahau Mkoa wa Singida kwenye fursa za uwekezaji na
kuongeza kuwa mkoa wa Singida una fursa nyingi hasa vitunguu ambavyo
vimekuwa vikisafirisha nje ya nchi na kufungashwa kwa jina la nchi hiyo
ya jirani.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkta Rehema Nchimbi amempongeza Mkurugenzi
Mwambe kwa kuendelea kuaminiwa na Mheshimiwa Raisi kutokana na
uchapakazi na uadilifu wake.
Dokta
Nchimbi amesema Mkoa wa Singida umekuwa ukizalisha bidhaa nzuri na
zenye ubora pamoja na kuzalisha watendaji waadilifu na wachapakazi na
hivyo uteuzi wake utaendelea kuwapa hamasa vijana na watumsihi wengine
waendelee kuwa waadilifu.
Ameongeza
kwa Singida ina fursa za kutosha kuleta maendeleo ya Mkoa huu pamoja na
taifa kwa ujumla pia unajivunia fursa hizo ambazo baadhi yake ni kilimo
cha alizeti, vitunguu na asali bora.
Dokta
Nchimbi amemuasa Mkurugenzi Mwambe kuiwakilisha Singida katika majukumu
yake na pia kutumia uchapakazi wake katika kuboresha mazingira ya
uwekezaji ili yawavutie wawekezaji wa nje na ndani ili kufikia lengo la
tanzania ya Viwanda.
Aidha
amemkaribisha tena Singida na kumuahidi kuwa Mkoa uko tayari kwa ajili
ya uwekezaji wowote wenye tija kwa wananchi na pia Singida iwe sehemu ya
viwanda na kuipa nafasi Dodoma kuwa makao makuu ya nchi.
COMMENTS