DKT. NCHIMBI AZITAKA KAMATI ZA MAJI KUSIMAMIA KIMAMILIFU MIRADI YA MAJI MANISPAA YA SINGIDA

Kamati za maji za visima kumi vya maji katika manispaa ya Singida zimekuwa sababu ya miradi hiyo iliyokamilika kwa asilimia miamo...


Kamati za maji za visima kumi vya maji katika manispaa ya Singida zimekuwa sababu ya miradi hiyo iliyokamilika kwa asilimia miamoja kutofanya kazi na kuwanufausha wananchi huku ikiwa imegharimu fedha nyingi za serikali na wahisani hasa benki ya dunia.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mwishoni mwa wiki hii mara baada ya kukagua miradi hiyo na kujiridhisha kuwa miradi hiyo imekamilika licha ya kutofanya kazi.

Dkt. Nchimbi amesema sababu kubwa ya kutofanya kazi miradi hiyo ni udhaifu wa kamati za maji na wanasiasa katika maeneo ya miradi kutojali shida ya wananchi ya kukosa maji na hivyo kuitelekeza miradi hiyo badala ya kuisimamia.

Amesema lengo la miradi hiyo ni wananchi wapate maji safi na salama kwa umbali usiozidi kilometa nne kama ilivyoagizwa na serikali.

“Katika ukaguzi wangu nimebaini mifumo katika miradi hii ya maji ipo vizuri sana. Baadhi inaendeshwa kwa umeme na mingine kwa mafuta ya dizel. Makubaliano yalikuwa baada ya kukamilika miradi hii iendeshwe na kamati za maji kwa asilimia mia moja”, amesema.

Dkt. Nchimbi amesema wajibu wa kamati hizo ni pamoja na kukusanya fedha zinazotokana na kuuza maji kwa wateja pamoja na matengenezo ya miundombinu ya visima hivyo ili miradi hiyo iwe endelevu.

“Fedha zinazopatikana ndizo zitakazoendesha mradi husika ikiwemo kugharamia matengenezo ya mashine, pampu, miundombinu, kununulia dizel, umeme na kumlipa mhudumu wa mradi. Makubaliano ni miradi ikikamilika inabaki mikononi mwa wananchi kupitia kamati zao za maji. Serikali na wafadhili hawatahusika tena”, amesisitiza Dkt. Nchimbi.

Dkt. Nchimbi amesema serikali na benki ya dunia imegharamia fedha nyingi kwenye miradi hiyo hivyo haiwezi kuendelea kuona miradi inabaki kuwa mapambo badala ya kuwaondolea wananchi kero ya maji.

“Naagiza wananchi wajipange upya chini ya kamati zao wachague jumuiya za watumiaji maji. Kwenye jumuiya hizo za maji wanaweza kuwepo pia wale waliokuwa kwenye kamati za awali za maji. Jumuiya hizi ziwajibike kikamilifu zihakikishe zinapata fedha kutokana na mauzo ya maji ili waendeleze miradi hiyo kwa ufanisi”, amesema Dkt. Nchimbi.

Akiijengea nguvu hoja yake hiyo amesema kuanzia mei mwaka huu anataka kuona kila wananchi wa manispaa ya Singida,anapata maji safi na salama kwa umbali mfupi.

“Rasilimali maji ni msingi kwa maisha ya viumbe hai wakiwemo binadamu. Maji yakiwepo tena kwa umbali mfupi mambo yote yatakwenda vizuri. Maji yanasaidia kuweka mazingira safi na afya za wananchi zinaboreka. Maji yana mchango mkubwa kwa jamii inayoelekea kwenye Tanzania ya viwanda”, amesema.

Wakati huo huo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa wanatarajia baadhi ya miradi na hasa ile ya umeme kuibinafisha kwenye mamlaka ya maji safi na maji taka (SUWASA) kwa ajili ya kuiendesha. Mingi itaendelea kumilikiwa na wananchi wenyewe.

Awali mhandisi wa maji manispaa ya Singida Max Hassan Kaaya amesema wanaendelea kuelimisha jamii kuwa miradi hiyo ya maji ni mali yao hivyo jukumu la kuiendesha ni lao. Pia wanapaswa kuilinda na kuitunza vizuri.

Naye mkazi wa kijiji cha Mtamaa Hongoa Bunka amesema elimu zaidi itolewe ili kubadilisha fikiri potofu ya baadhi ya wananchi kuwa jukumu la kuendesha miradi ya maji ni la serikali. Wabadilike na kutambua kuwa ni mali yao na wao ndio watakaoiendesha.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DKT. NCHIMBI AZITAKA KAMATI ZA MAJI KUSIMAMIA KIMAMILIFU MIRADI YA MAJI MANISPAA YA SINGIDA
DKT. NCHIMBI AZITAKA KAMATI ZA MAJI KUSIMAMIA KIMAMILIFU MIRADI YA MAJI MANISPAA YA SINGIDA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgmUhRLCNVdpy8uttdIO71QIsLm8nyWnNFYnc_6DG1HW3KUFatIZfviag41Ao5s7m2dt90ycU9xk_G8Bjf8TPbVigTm-KXc15jjZ7640_hp7R2aHXLakKpooROY1q10xnYfM9V6a8Sy4D8/s400/index-23.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgmUhRLCNVdpy8uttdIO71QIsLm8nyWnNFYnc_6DG1HW3KUFatIZfviag41Ao5s7m2dt90ycU9xk_G8Bjf8TPbVigTm-KXc15jjZ7640_hp7R2aHXLakKpooROY1q10xnYfM9V6a8Sy4D8/s72-c/index-23.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/dkt-nchimbi-azitaka-kamati-za-maji.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/dkt-nchimbi-azitaka-kamati-za-maji.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy