Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi akimkabidhi vitabu vya sayansi, Maria Edward, mwanafunzi wa Shule ya sekondari y...
Suala
la uhaba wa vitabu vya masomo ya Sayansi, maabara pamoja na walimu wa
masomo hayo limekuwa likisababisha baadhi ya wananfunzi kushindwa kumudu
na hivyo kuyaepuka masomo hayo, licha
ya serikali na wadau mbalimbali kuhamasisha wanafunzi kuchukua masomo
hayo.
Kutokana
na hali hiyo Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel imetoa msaada wa
Vitabu vya Masomo ya Sayansi vyenye thamani ya Shilingi Milioni Tatu
katika Shule ya Sekondari Vianzi
iliyopo Mkuranga Mkoani Pwani ambayo ina zaidi ya wanafunzi 400 ikiwa
na walimu watatu kwa masomo yote ya Sayansi (biolojia, fizikia, kemia na
hesabu). Hatua hiyo ni mwendelezo wa Kampuni hiyo kusaidia katika
elimu shule mbalimbali hapa nchini ili kuinua
kiwango cha elimu katika masomo ya Sayansi.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari Vianzi Mwl. Ashura Manaki amesema kuwa shule yake
imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu, maabara za
kutosha pamoja na vitabu hali ambayo
imekuwa ikisababisha wanafunzi kukimbia masomo ya Sayansi.
“Tunaishukuru
sana Airtel kwa msaada huu wa vitabu ebu fikilia tuna upungufu wa
walimu,sasa likija tatizo la ukosefu wa vitabu unadhani wanafunzi
watayapenda masomo ya sayansi,lakini
kwa sasa nina matumaini tutaweza kusonga mbele,”alisema Manaki.
Kwa
upande wa Meneja wa Huduma kwa Jamii kutoka Airtel Hawa Bayumi ameleeza
kuwa licha ya Kampuni hiyo kujikita katika mambo mbalimbali ya Kijamii
wameona umuhimu wa kuisaidia shule
hiyo ambayo inachangamoto ya walimu wa sayansi lakini wakakuta hata
vitabu navyo ni changamoto wakaamua kutoa msaadahuo.
”Licha
ya Airtel kusaidia mambo mbalimbali ya kijamii tumeona kuna umuhimu
mkubwa kuisaidia vitabu vya sayansi shule hii kutokana na kukabiliwa na
changamoto ya uhaba wa walimu wa
sayansi pamoja na vitabu vya sayansi tuna matumaini vitaweza kusaidia
shule hii kujenga wataalamu wa sayansi hasa ukizingatia serikali inaweka
juhudi kufikia Tanzania ya viwanda ni muhimu kuwekeza katika rasilimali
watu na kujenga watanzania weny weledi. Lengo
letu ni kuendelea kuwezesha vijana kufikia malengo yao kupitie elimu na
ujasiriamali,”alisema Bayumi.
Zamda
Said ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo amesema kuwa shule hiyo bado
ina mahitaji ya walimu wa sayansi lakini kwa kupatiwa vitabu hivyo
vitasadia hata wanafunzi kuweza kujisomea
huku akiwaasa wanafunzi kutumia fursa hiyo kufaulu masomo ya sayansi.
“Ni
kweli tatizo la uhaba wa walimu pamoja na ukosefu wa vifaa vya
kujifunzia na kufundishia ni changamoto kwa shule hii lakini nawaombeni
wanafunzi kutumia fursa hii kuweza kujisomea
maana vitabu gharama yake ni kubwa,”alisema Said.
COMMENTS