WATU WATATU WASHIKILIWA KWA KOSA LA UVAMIZI WA MKUTANO WA CUF JUZI

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kushiriki tuki...

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kushiriki tukio la uvamizi wa Mkutano wa wanachama wa CUF uliofanyika Vinna Hotel Mabibo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa Habari jijini hapa. Amesema kuwa. Aprili 22 mwaka huu majira ya mchana, walipokea taarifa ya kuwa watu wasiofahamika wakiwa na silaha walivamia mkutano huo na kujeruhi baadhi ya watu.


Kamanda Sirro ameongeza kuwa, mpaka sasa watuhumiwa watatu waliokamatwa wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika hatua za kisheria zitafuatwa juu yao na amewasihi watu kutii sheria bila shuruti kwani hakuna mtu au kikundi chochote cha watu wanaoweza kuwa na mamlaka ya kushambulia wengine.


"Kama unamalalamiko pitia polisi, au mahakamani siyo kuvamia kundi la watu wengine kama wako juu ya sheria, tunafuatilia wale wote waliohusika katika kufanya shambulio hilo na mtu mmoja aliyejeruhiwa sana anataja watu walioshambulia" amesema Sirro.


Kamanda Sirro, amesema jeshi la polisi linaamini kuwa watu waliofanya uvamizi huo walifanya kwa utashi wao wenyewe na kwamba pindi upelelezi ukikamilika watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kupelekwa mahakamani.


Aidha amewaonya baadhi ya viongozi wa CUF waliotangaza kuwafuata watu fulani na kuwawajibisha ni vema wakumbuke kuwa hakuna mtu aliyeko juu ya sheria kwani hakuna mtu aliyeko juu ya mamlaka.


Mapema wiki iliyopita, watu wasiojulikana wakiwa na bastola walivamia mkutano wa wanachama wa CUF ambao wanamuunga mkono, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad na kuwapiga wanachama wa CUF pamoja na waandishi wa habari ambao walikuwepo eneo hilo.


Mkutano huo ambao ulikuwa na lengo la kumtambulisha Katibu Mkuu wa CUF , ulivurugika baada ya vurugu kubwa zinazodaiwa kufanywa na wanachama wa CUf ambao wanamuunga mkono Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.


katika vurugu hizo, Mtu mmoja ambaye bado hajafahamika jina lake miongoni mwa waliovamia mkutano wa wanachama wa CUF ameshambuliwa na wananchi wakati akijaribu kutoroka.

Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini leo, kuhusiana na tukio la uvamizi wa Mkutano wa wanachama wa CUF uliotokea mwishoni mwa wiki hii.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WATU WATATU WASHIKILIWA KWA KOSA LA UVAMIZI WA MKUTANO WA CUF JUZI
WATU WATATU WASHIKILIWA KWA KOSA LA UVAMIZI WA MKUTANO WA CUF JUZI
https://1.bp.blogspot.com/-ikXyunn0fMQ/WP4GfPKD4II/AAAAAAAAYNY/-6jdjy34EKcKooc_GAtJLv4nFJK1Jja2QCLcB/s640/WhatsApp%2BImage%2B2017-04-24%2Bat%2B07.04.51.jpeg
https://1.bp.blogspot.com/-ikXyunn0fMQ/WP4GfPKD4II/AAAAAAAAYNY/-6jdjy34EKcKooc_GAtJLv4nFJK1Jja2QCLcB/s72-c/WhatsApp%2BImage%2B2017-04-24%2Bat%2B07.04.51.jpeg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/watu-watatu-washikiliwa-kwa-kosa-la.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/watu-watatu-washikiliwa-kwa-kosa-la.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy