SERIKALI YAONDOA TOZO ZISIZO ZA LAZIMA KATIKA ZAO LA KOROSHO

Na Daudi Manongi-MAELEZO,DODOMA. Serikali kupitia Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvivu imesema imeshughulikia malalamiko  ya wakulima wa ...




Na Daudi Manongi-MAELEZO,DODOMA.
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvivu imesema imeshughulikia malalamiko  ya wakulima wa Korosho kwa kuondoa makato yasiyokuwa muhimu katika zao hilo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Wizara hiyo Mhe.William Ole Nasha wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge leo Mjini Dodoma.
“Serikali imekwisha fanyia marekebisho maeneo ambayo wakulima walikuwa wanalalamikia kwa kuondoa kabisa makato hayo katika zao hilo”, Aliongeza Mhe.Ole Nasha.
Amesema kuwa Serikali imefuta ushuru wa shilingi 20 kwa kilo kwa ajili ya chama kikuu cha Ushirika,Shilingi 50 za usafirishaji wa Korosho,Shilingi 10 kwa kilo ajili ya mtunza ghala na pia shilingi 10 kwa kilo kwa ajili ya kikosi kazi cha Masoko. Aidha Sekta ina utaratibu maalum wa kupanga bei dira kwa kutumia vigezo vinavyokubaliwa kwa pamoja na wadau wote.
Kwa upande wa manunuzi ya pembejeo za korosho amesema hufanywa kwa pamoja na vyombo rasmi ndani ya Tasnia ambapo awali ilikuwa ikisimamiwa na mfuko wa Maendeleo ya Korosho na sasa Bodi ya korosho Tanzania.
Aidha ameeleza changamoto zinazojitokeza katika kufikisha pembejeo hizo kwa wakulima wa korosho na hatua zimechukuliwa kwa kushirikisha vyama vya ushirika ili kudhibiti mianya ya pembejeo kwenda kwa wasio lengwa.
Pia Serikali imeweka mfumo wa usambazaji wa pembejeo wenye lengo la kuhakikisha kwamba pembejeo hizo zinawafikia walengwa pekee.
“Utaratibu huu unazingatia kutambua wakulima wenye uhitaji na pembejeo na hununuliwa kwa kutumia utaratibu wa ununuzi wa pamoja n akusambazwa kwa wakulima kwa kutumia wakala  walioteuliwa na kudhibitishwa na Halmashauri husika”, Alisisitiza Mhe.Ole Nasha.

Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha akijibu swali Bungeni mjini Dodoma leo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SERIKALI YAONDOA TOZO ZISIZO ZA LAZIMA KATIKA ZAO LA KOROSHO
SERIKALI YAONDOA TOZO ZISIZO ZA LAZIMA KATIKA ZAO LA KOROSHO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi44VwyVMxEMUXQmNs8ioWo8o9rja4-zx2AvR3FDRLIFTspexsgV_Q2JCerpZrzrVfpzjddfuiM0vnXU6WiN2TtGsSe03Ot986a_nYiFZgXCPF8HZteNn_ID9B0qXdYOt6luNHMAUT-hfk/s640/Pix+6.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi44VwyVMxEMUXQmNs8ioWo8o9rja4-zx2AvR3FDRLIFTspexsgV_Q2JCerpZrzrVfpzjddfuiM0vnXU6WiN2TtGsSe03Ot986a_nYiFZgXCPF8HZteNn_ID9B0qXdYOt6luNHMAUT-hfk/s72-c/Pix+6.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/serikali-yaondoa-tozo-zisizo-za-lazima.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/serikali-yaondoa-tozo-zisizo-za-lazima.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy