MWANARIADHA ALPHONCE FELIX SIMBU KUTINGA BUNGENI; KUWA MGENI MAALUM WA MWAKYEMBE

Mwanariadha Alphonce Simbu aliyeshika nafasi ya tano katika mashindano ya London Marathon anatarajia kutembelea bunge la Jamhuri ya Muung...


Mwanariadha Alphonce Simbu aliyeshika nafasi ya tano katika mashindano ya London Marathon anatarajia kutembelea bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhamisi April 27 akiwa ni mgeni maalum wa Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni Harisson Mwakyembe. Baada ya kutembelea bumge hilo Simbu pia atakuwa na mazungumzo na Waziri Mwakyembe.



 
Mwanariadha Alphonce Simbu akilakiwa na Meneja Uhusiano wa Multchoise Tanzania, Johnson Mshana (kulia) na Meneja wa mwanariadha huyo, Francis John alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).



Simbu ataambatana na muwakilishi wa wadhamini wake DStv pamoja na maafisa waandamizi wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT.

 

Akizungumzia mualiko huo, mwanariadha huyo amesema kuwa amefurahi sana kupata mualiko wa Waziri anayehusika na sekta ya michezo kwenda bungeni kama mgeni wake maalum. Amesema hii inaonyesha kuwa serikali inatambua jitihada zake anazozifanya katika kuiwakilisha vyema nchi katika mashindano ya kimataifa. “Nimefurahi sana kualikwa na muheshimiwa Waziri kumtembelea bungeni, bila shaka hii itakuwa fursa nzuri ya hata wabunge kutambua jitihada tunazofanya vijana wao katika kuliletea taifa sifa. Natumaini pia nitapata fursa ya kuongea ana kwa ana na Waziri” alisema Simbu na kuongeza kuwa atatumia fursa hiyo kumueleza Waziri changamoto nyingi wanazokabiliana nazo wanamichezo hapa nchini.

 

Amesema kuna mengi ya kuongea na Waziri na kwamba anaamini mazungumzo yao yatakuwa na tija na manufaa si kwake tu, bali kwa wanamichezo wote kwa ujumla.

 

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana, ambaye anaandamana na Simbu, amesema kuwa anaamini kuwa ziara hiyo na mkutano na Waziri utakuwa na manufaa makubwa kwani pia itakuwa ni fursa nzuri ya kujadili namna bora zaidi ya Serikali kushirikiana na wadau katika kuimarisha na kuendeleza michezo hapa nchini. “sisi kama wadhamini wa mwanariadha huyu tunaamini kuwa kitendo cha Waziri kutualika ni ishara tosha kuwa kweli anadhamiria kushirikiana na sisi wadau wa michezo ili kuongeza nguvu za pamoja za kuimarisha michezo hapa nchini” alisema Mshana

 

Multichoice Tanzania kupitia DStv imekuwa ikimdhamini Simbu tangu mwaka jana na udhamini huo pia umewanufaisha wanariadha wengine ambao wamekuwa kambini kwa muda sasa pamoja na simbu. “Kambi ya mazoezi ya Simbu ambayo ilidhaminiwa na DStv pia ilikuwa na wanariadha wengine ambao wote walinufaika moja kwa moja na udhamini huo. Tunaamini kuwa pia kati ya hao tutapata wanariadha watakaofanya vizuri siku zijazo”.

 

Alphonce Simbu, ambaye pia ni mshindi wa medali ya dhahabu katika mashindano ya Mumbai Marathon ni miongoni mwa wanariadha wa timu ya Taifa itakayoshiriki katik mashindano ya Dunia yatakayofanika jijini London  mwezi Agosti mwaka huu

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MWANARIADHA ALPHONCE FELIX SIMBU KUTINGA BUNGENI; KUWA MGENI MAALUM WA MWAKYEMBE
MWANARIADHA ALPHONCE FELIX SIMBU KUTINGA BUNGENI; KUWA MGENI MAALUM WA MWAKYEMBE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEii2wsMtsiJPiD0kmc0sjF-dmmIKMmpMBu90gFfsE-hjeKLbol_Y9iwsTAFjN7meUFTNU4Pz-i6AhN58H3vYZ6pRWfc46ktHS4WBH6DY__g-ZHpSH4dUS4QKoKjr3g8PDWqWvDFi4NLbCU/s640/Simbu+1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEii2wsMtsiJPiD0kmc0sjF-dmmIKMmpMBu90gFfsE-hjeKLbol_Y9iwsTAFjN7meUFTNU4Pz-i6AhN58H3vYZ6pRWfc46ktHS4WBH6DY__g-ZHpSH4dUS4QKoKjr3g8PDWqWvDFi4NLbCU/s72-c/Simbu+1.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/mwanariadha-alphonce-felix-simbu.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/mwanariadha-alphonce-felix-simbu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy