Na. Catherine Sungura, WAMJW Ujumbe wa wawekezaji toka nchini Misri wamewasili nchini hapa na kufanya mazung...
Na. Catherine Sungura, WAMJW
Ujumbe
wa wawekezaji toka nchini Misri wamewasili nchini hapa na kufanya
mazungumzo na serikali ya Tanzania kwa nia ya kujenga viwanda vya dawa
za binadamu zikiwemo za majimaji pamoja na zile za antibiotic.
Ujumbe
huo ulikutana jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Ummy Mwalimu pamoja na wawakilishi toka wizara Viwanda,Biashara
na Uwekezaji na Kituo cha Uwekezaji cha Taifa (TIC) kwenye ofisi ndogo
ya wizara ya afya,maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto iliyopo
jijini Dar es Salaam
Ujumbe huo ulisema kuwa kiwanda
walichokusudia kujenga nchini hapa kitazalisha dawa za majimaji yaani
“IV Fluids” pamoja na “antiobiotics” za aina mbalimbali ikiwemo
"Paracetamol IV” na dawa za kutibu Malaria
Aidha, walisema
lengo lao ni kujenga kiwanda kikubwa ambacho kitakuwa na uwezo wa
kuzalisha dawa ambazo zitawahudumia watanzania pamoja na nchi za Afrika
Mashariki na ya kati.
Katika mazungumzo hayo,wawekezaji hao
pia wanatarajia kusaidia Tanzania katika uzalishaji wa chanjo ya ugonjwa
wa homa ya Ini (Hepatics B na C)
Kwa upande wake Waziri
Ummy amewaahidi wawekezaji hao kuwasaidia katika mipango ya ujenzi huo
na kutoa ushirikiano wa dhati katika kufanikisha viwanda hivyo vinajenga
nchini kwa muda uliopangwa.
“Naelekeza kwa taasisi zote
zitakazoguswa na uanzishwaji wa viwanda hivi watoe ushirikiano wa hali
ya juu ili lengo hili lifikiwe, soko la dawa hapa nchini lipo naomba
niwahakikishie hili”alisema waziri Ummy.
Waziri Ummy aliwaomba
wawekezaji hao kuharakisha ujenzi wa viwanda huo na kujengwa ndani ya
miezi kumi na nane kama walivyoahidi ili watanzania waanze kunufaika
mapema.
COMMENTS