Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) imesema zoezi la ubomoaji wa majengo yaliyomo katika hifadhi ya reli linaloendelea nchi...
Kampuni
Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) imesema zoezi la ubomoaji wa
majengo yaliyomo katika hifadhi ya reli linaloendelea nchini
limezingatia taratibu na
sheria za uendeshaji wa reli na kwamba matangazo ya notisi ya
kuwataarifu waanchi waliovamiwa hifadhi hizo zilizotolewa mapema ili
wananchi hao waweze kuhama.
akiongea
leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mtendaji RAHCO Bw. Massanja
Kadagosi amesema Ubomoaji huo unaoendelea haupo kwa ajili ya kumuonea
mtu bali upo kwa ajili ya kulinda miundombinu ya reli ikiwemo pia kujali
usalama wa wananchi waliojenga kwenye hifadhi ya reli. ‘’Sheria ya Reli
Na.4 ya mwaka 2002,kifungu cha 57 (2) kinabainisha kuwa mtu yoyote
haruhusiwi kufanya ujenzi wowote katika hifadhi ya njia ya reli pasipo
kibali cha RAHCO, kwani sheria hii inatamka wazi kuwa mtu yeyote
harusiwi kufanya ujenzi wowote katika eneo lilopangwa na mamlaka husika”
Madagosi
amesema kabla ya kuanza kuzibomoa nyumba hizo walitoa notisi mbali
mbali ikiwemo tangazo la kuwataarifu wavamizi hao kupitia kwenye vyombo
vya habari vya tarehe 25/4/2016, pamoja na kutoa barua kwa mkurugenzi wa
Manispaa ya Ilala ya kuwajulisha wananchi hao kuanza kuhama kabla
yauvunjaji kuanza.
Mbali
na Barua hizo, amesema Bw. Kadagosi tarehe 9 hadi tarehe 10 /2/2017
waliziweka nyumba alama ya X kwa wavamizi hao, analosema kuwa watu
wanaosema wananchi hao wanaovunjiwa hakuwapata taarifa za kutakiwa
kuvunjiwa nyumba si za kweli kwani taarifa zilitolewa.
Bw.
Kadagosi amewataka wananchi waliovamia maeneo hayo kuhama mara moja
kwani kukaa kwenye maeneo hayo sio tu ni kosa la jinai bali pia
linahatarisha usalama wao.
Mkurugenzi
mtendaji Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Bw. Masanja
Kadogosa akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam
kuzungumzia zoezi la ubomoji wa nyumba zilizopo kwenye hifadhi ya reli
Afisa
Uhusiano wa RAHCO,Catherine Moshi akitoa maelezo kwa waandishi wa
habari waliokuwepo kwenye mkutano huo leo jijini Dar es Salaam
Waandishi
wa habari na watendaji wa RAHCO wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji
Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa.
COMMENTS