Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeboresha ofisi zake za kanda za ardhi zilizopo nchini ili kuongeza ufanisi katika...
Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeboresha ofisi zake za kanda
za ardhi zilizopo nchini ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma za
ardhi karibu zaidi na wananchi.
Wizara
imegawa magari katika kanda zake zote ili kurahisisha utekelezaji wa
kazi za ardhi na kuharakisha huduma za sekta nzima ya ardhi katika
maeneo yote ya nchi badala ya wananchi kuja ofisi za Dar es Salaam
ambazo kwa sasa zinahamia makao Makuu ya Nchi Dodoma.
Hatahivyo,
huduma nyingine za kisekta kama vile za malipo ya kodi ya pango la
ardhi, kituo cha huduma kwa mteja na ofisi za kanda za Dar es Salaam
zitaendelea kufanyika kama ilivyokuwa awali.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati
akitangaza kuhamia rasmi kwa Wizara yake mkoani Dodoma amesema kuwa
Wizara imepanga kuwaweka wataalam wa sekta nzima ya ardhi katika ofisi
za kanda ili kuondoa usumbufu uliokuwepo wa kufuata huduma za hati,
usajili, Uthamini upimaji na ramani na mipango miji na vijiji – Dar es
Salaam na Dodoma.
Katika
kutekeleza hili kila Kanda itakuwa na viongozi wake walio na mamlaka za
utoaji wa huduma za ardhi na kuidhinishwa kwa nyaraka mbalimbali za
ardhi na hata utoaji wa hati miliki kutolewa katika kanda.
Viongozi
ambao watakuwepo katika kanda hizo ni pamoja na Kamishna na Kanda
Msaidizi wa Ardhi, Msajili Msaidizi wa Hati wa Kanda, Mthamini Mkuu
Msaidizi wa Kanda, Mkurugenzi Msaidizi wa Upimaji na Ramani wa Kanda,
Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Miji na Vijiji wa Kanda na Msajili
Msaidizi wa Baraza la Ardhi na Nyumba wa Kanda.
Aidha
jumla ya kanda ni nane ambazo ambazo zimeboreshwa na kuundwa upya. Kanda
hizo ni; Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, ambayo itahusika na mikoa ya
Dar es Salaam na Pwani, na Dar es Salaam ndio makao makuu ya kanda.
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini; itahusika na mikoa ya Mbeya, Njombe,
Rukwa na Songwe, ambapo Mbeya ndio makao makuu ya kanda. Kanda ya Kati;
ni pamoja na mikoa ya Dodoma, Singida, Iringa na Morogoro na Dodoma ni
makao yake makuu.
Aidha,
Kanda ya Kaskazini; ni mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara,
ambapo makao yake makuu ni Arusha. Kanda ya Ziwa; Ni mikoa ya Mwanza,
Geita na Kagera, ambapo Mwanza ndio makao yake makuu. Nyingine ni Kanda
ya Magharibi; yenye mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi na Tabora ndio
makao makuu ya kanda. Kanda ya Kusini; Ni mikoa ya Mtwara, Lindi na
Ruvuma na Mtwara ndio makao makuu ya kanda, na kanda ya nane ni Simiyu;
yenye mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara na Simiyu ndio makao makuu.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi, Naibu
wake Mhe. Dkt. Angeline Mabulla, Katibu Mkuu; Dkt Yamungu Kayandabila na
Viongozi wengine wakuu wa wizara wakikagua magari ya kuhudumia ofisi za
ardhi za kanda nchini.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akikabidhi
funguo ya gari kwa Kamishna wa kanda ya Dar es Salaam; Matthew Nhone.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi, Naibu
wake Mhe. Dkt. Angeline Mabulla, Katibu Mkuu; Dkt Yamungu Kayandabila na
Viongozi wengine wakuu wa wizara wakikagua magari ya kuhudumia ofisi za
ardhi za kanda nchini.
COMMENTS