Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii Utafiti unaonesha kuwa jamii ya wafugaji wamekuwa wakikumbwa na ugonjwa wa malale, hali ambayo...
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Utafiti
unaonesha kuwa jamii ya wafugaji wamekuwa wakikumbwa na ugonjwa wa
malale, hali ambayo usipodhibitiwa mapema unaweza kusababisha vifo
katika jamii hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya
Maendele ya Jamii , Jinsi, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibayila amesema
kuwa mradi wa utafiti huo kama serikali kutafuta namna ya kuweza
kudhibiti ugonjwa huo.
Amesema
kuwa mradi wa utafiti wa ugonjwa wa marale ulifanywa kuangalia
mabadiliko Tabia ya Nchi na matumizi ya ardhi kwa jamii ya wafugaji wa
Wilaya ya Simanjiro na Monduli.
Dk.Neema
amesema utafiti huo utasaidia kwa watunga sera wa Wizara ya Afya
Maendele ya Jamii , Jinsi, Wazee na Watoto pamoja Wizara ya Maendeleo ya
Kilimo na Uvuvi kuweza kuangalia namna ya kudhibiti ugonjwa huo ili
usiwe tatizo kwa jamii ya wafugaji.
Nae
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR),
Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa mradi huo umefanywa na NIMR pamoja na
Chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela katika kuangalia ugonjwa marale.
Amesema
ugonjwa wa Marale kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la sahara zimekuwa
zikikumbwa na ugonjwa huo hasa katika jamii za wafugaji.
Kwa
upande wa Mkuu wa Mradi wa Utafiti wa Ugonjwa wa Marale , Profesa Paul
Gwakisa amesema kuwa mradi huo ni wa miaka mitatu ambapo wamekuja kutoa
matokeo juu ya utafiti walioufanya.
Amesema ugonjwa wa marale ni tatizo kwa jamii ya wa wafugaji ambapo unahitaji kudhibitiwa kabla ya tatizo hilo halijawa kubwa.
Mkurugenzi
wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya Maendele ya Jamii , Jinsi, Wazee
na Watoto, Dk. Neema Rusibayila akizungumza wakati kuzindua majadiliano
ya utafiti wa ugonjwa wa marale katika Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya
Binadamu (NIMR) leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa
Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Profesa Yunus Mgaya.
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Profesa
Yunus Mgaya akitoa neno katika majadiliano ya ugonjwa wa marale
uliofanywa kati ya NIMR na Chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela leo
jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Mkuu
wa Mradi wa Utafiti, Profesa Paul Gwakisa akizungumza jinsi
walivyofanya utafiti wa ugonjwa marale katika jamii ya wafugaji kwa
Wilaya Simanjiro na Monduli mkoani Arusha leo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya Maendele ya Jamii , Jinsi, Wazee
na Watoto, Dk. Neema Rusibayila akiwa katika picha ya pamoja na Watafiti
, Watendaji Wizara na Taasisi leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja
COMMENTS