Na Greyson Mwase, Njombe Kaya 1600 katika vijiji kumi mkoani Njombe zinatarajiwa kupata umeme wa uhakika mara baada ya kuka...
Na Greyson Mwase, Njombe
Kaya
1600 katika vijiji kumi mkoani Njombe zinatarajiwa kupata umeme wa
uhakika mara baada ya kukamilika kwa mradi wa uzalishaji wa umeme kwa
kutumia maporomoko ya maji wa Luponde Hydro Ltd unaotekelelezwa na
kampuni ya Rift Valley Energy.
Hayo
yalielezwa leo na Meneja Mradi wa Luponde Hydro, Mugombe Maxwell katika
ziara ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini
katika mkoa wa Njombe ili kujionea maendeleo ya miradi midogo ya umeme
wa maporomoko ya maji na nishati jadidifu inayotekelezwa katika mkoa
huo.
Maxwell
alisema kuwa kampuni ya Rift Valley Energy ina miradi miwili ambayo ni
Mwenga Hydro Grid wenye uwezo wa Megawati 4.1na Luponde Hydro Ltd
utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 3 mara baada ya kukamilika kwa
ujenzi wake hivyo kuwezesha vijiji kumi katika mkoa huo kupata umeme wa
uhakika ifikapo mwakani.
Akielezea
mradi huo wa Luponde Hydro Ltd, Maxwell alisema kuwa mradi ulianza
mwaka 2016 na kuongeza kuwa mradi huo upo katika maeneo mawili ambayo ni
Luhololo na Igola yote yakiwa mkoani Njombe.
Akielezea
ujenzi wa mradi huo, Maxwell alieleza kuwa mradi umegawanyika katika
awamu mbili na kuendelea kusema kuwa awamu ya kwanza inahusisha
usambazaji wa umeme wa uhakika katika vijiji saba vyenye kaya 1120,
shule tisa na vituo vya afya vitano
Aliongeza kuwa, awamu ya pili inahusisha usambazaji wa umeme wa uhakika katika vijiji vitatu vyenye kaya 180.
Akielezea
hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa mradi huo, Maxwell alisema kazi
katika eneo la Luhololo imekamilika kwa asilimia 60 kwa kazi za kawaida
na asilimia 40 katika ujenzi wa mitambo.
Aliongeza
kuwa katika eneo la Igola mradi umekamilika kwa asilimia 40 na
kusisitiza kuwa kampuni itahakikisha kuwa ujenzi katika maeneo yote
unakamilika ifikapo mwakani ili wananchi wapate umeme wa uhakika.
Alisisitiza
kuwa lengo la mradi ni kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na umeme wa
uhakika na kuchangia ukuaji wa uwekezaji kwenye viwanda hususan katika
maeneo ya vijijini, hivyo kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi
wa nchi.
Mtaalam
kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi
Stephan Kashushura (kulia) akibadilishana mawazo na Sister Richardis
Chiwinga katika ziara ya wataalam wa nishati jadidifu katika mradi wa
kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Benedict Sisters of Saint Agnes
Chipole, Mbinga mkoani Ruvuma.
Sister
Richardis Chiwinga kutoka katika mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia
maji wa Benedict Sisters of Saint Agnes Chipole (katikati) akielezea
hali ya maji katika bwawa la mradi huo kwa wataalam wa nishati jadidifu
kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Sehemu
ya bwala la maji katika mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa
Benedict Sisters of Saint Agnes Chipole, Mbinga mkoani Ruvuma.
Sister
Richardis Chiwinga kutoka katika mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia
maji wa Benedict Sisters of Saint Agnes Chipole (kushoto) akiongoza
watalam kutoka Idara ya Nishati Jadidifu, Wizara ya Nishati Jadidifu
katika ziara kwenye eneo la mradi.
Moja
ya mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji katika mradi wa
kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Benedict Sisters of Saint Agnes
Chipole.
Meneja
Uendeshaji kutoka kampuni ya kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko
madogo ya maji ya kampuni ya Rift Valley Energy, Joel Gomba (kulia)
akionesha sehemu ya kuchepushia maji katika mradi wa Luponde Hydro Ltd
uliopo katika hatua ya ujenzi mkoani Njombe kwa mtaalam kutoka Sehemu ya
Nishati Jadidifu, Wizara ya Nishati na Madini, Emillian Nyanda
(kushoto).
COMMENTS