Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Taifa, Mh. Freeman Mbowe Na Anthony John, Globu ya Jamii Chama cha Demokra...
Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Taifa, Mh. Freeman Mbowe
Na Anthony John, Globu ya Jamii
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesitisha shughuli zote za maandamano na mikutano nchi nzima,kwa kudai kuwa ukuta ni fikra endelevu na si mpango wa siku moja.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa,Mh.Freeman Mbowe wakati akizungumza na Waandishi wa Habari,Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam.
Mbowe amesema kuwa wataendelea Kujipanga katika kulinda Haki yao ya kidemokrasia kama ambavyo katiba ya vyama vya siasa inavyosema,kuwa ni haki yao ya kidemokrasia.
‘’Mapambano ya kisiasa si tukio la siku moja ni tukio endelevu na kwa hiyo tarehi Mossi ,Oktoba ambayo ilikuwa ni siku mbadala ya maandamano maalum,hivyo kwa niaba ya kamati kuu imeona kuna umuhimu wa kusimamisha maandamano maalumu na mikutano nchi nzima ilikupisha mbinu nyingine mbalimbali’’amesema Mbowe
COMMENTS